Zanzibar 2020 Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga

Zanzibar 2020 Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga

..wakati wananchi wanadhulumiwa na kunyimwa haki zao hawazungumzi.

..wanakuja kuzungumza baada ya wananchi kuamua kuchukua sheria mikononi mwao.
We naye Pu.n.ga huo msikiti ndio umedhurumu haki yao?
 
Hao ni magaidi wakikamatwa watendewe sawa na Magaidi wengine
 
Wasiojulikana walitafutwa na nani?

IMG_20200918_160410.jpg
 
Tulizisoma ishara ukutani zamani na wahusika hawakujali. Hili ni zao la kutokujali kwao.
 
Huu ni mchezo wameupanga wenyewe kutaka kuhalalisha uvamizi huko kisiwani pemba na si mapya haya kumekuwa kukijitokeza matukio kama hayo katika kipindi cha uchaguzi ikiwemo kuchomewa nyumba zao masheha lakini unakuta hakuna majeruhi ni mipango tu ili kutoa picha mbaya kwa upinzani makini.

ACT hawawezi kuvamia mskitini abadan wenye tabia hizo ni CCM na vyombo vya ulinzi ndio ambao hawana hofu ya Mungu.

Wamewahi kuvamia watu msikitini na kuwatesa huko kisiwani pemba 2005 na huku bara wanahistoria pale mwembe chai. CCM acheni siasa za maji taka.

Leteni majeshi ya nchi nzima pemba lakini mara hii UKHANITHI BASI.
 
Hatutaki vurugu, tunataka amani , Tulaani vishawishi vyote vya vurugu ili vurugu zisianze. Tusifumbie macho upande wowote ule.
Lakini pia tusikuze mambo; kwani kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya tukio hilo na uchaguzi?
 
Watu mnaoanza kuoneshana vidole ktk machafuko haya haifai. Hakuna anayeweza kujua kwa hakika kama ni CCM au ACT Wazalendo au mshenzi mmoja tu hana hata Chama amepewa pesa kulianzisha. Wapeni muda vyombo vya dola vimtafute. Akipatikana atasema yote. Ilipochomwa moto ofisi ya CHADEMA Arusha, watu walisema mengi, lakini walipokuja kukamatwa waliohusika, waliokuwa wanatema cheche aibu imewashika. Hawazungumzii hilo tena.
 
Hakuna nchi inayoitwa Zanzibar. Na nataman Magufuli afanye kama walivyofanya India kwa kashmir
 
Janja ya ccm hii ni kutafuta vijisababu ili wahamishie majeshi ya tanganyika Zanzibar 😂😂😂
 
Pengine ni hasira za waliokatwa/kienguliwa. ZEC jaman angalieni hili kunusulu maisha ya watu. Pemba wenzetu huwa hawatanii ni si waoga. Kumbuka enzi za Mkapa akiwa Rais hali haikuwa nzuri
 
natamani kweli vita kamili ijee kipindi hiki…...
 
Back
Top Bottom