Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
Tetesi zinasema PhD yake ni ya kuunga unga.Hakuna ambaye hajamsikia Rais Samia Suluhu leo alipoagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa kwa chuki vifunguliwe , huyu Hassan Abbass ni nani katika nchi hii hadi amlishe maneno Mh Rais kwamba Kilichoagizwa kufunguliwa ni Televisheni za mitandaoni , liko wapi andiko alilopewa na Mh Rais kuhusu hilo ?
Je amedhamiria kumpinga Mh Rais kwa faida ya nani ? kuna haja gani ya kuendelea kuwa na kiongozi mwenye kiburi kiasi hiki ?
Bila shaka huyu ameshindwa kwenda na kasi ya mama , ameamua kupandisha mabega yake juu kujimwabafai , napendekeza afukuzwe kazi haraka na ikiwezekana akamatwe na kushitakiwa .
View attachment 1745371
Alaf kupindisha maagizo ya Mkuu wako kazi ni dalili ya dharau.
Simuombei mabaya ila akiendelea hivi hafiki mbali ataliwa kichwa hakuna mamlaka inapenda kudharauliwa na aliyeko chini.
Dr. Abbas kuwa na nidhamu kwa Rais vinginevyo utaingia kwenye mfungo ukiwa na majonzi