Pep Guardiola, Mwalimu bora wa miaka yote

1.Pep na Mess hakuna mwenzake aliemfanya mwenzake kuwa bora bali wote ni bora.

2.Pep aliwakuta Xavi,na Iniesta wakiwa kwenye peak lakini kwasababu nae yupo bora ndio maana aliweza kuyafanya aliyofanya.

3.Pep kushindwa kuchukua ubingwa wa UEFA Buyern sio kufeli kwa Pep,bali buyern hakupendezwa na mfumo wa ufunfishaji wa Pep ndio maana aliamua aondoke.Kama ambavyo Mo alishindwa kuchukua UEFA akiwa R.Madrid huku akiwa nawachezaji bora duniani.

4.Kuhusu kuchukua EPL hilo liko wazi atachukua sio tu atachukua,atachukua na huku kazinyanyasa timu kuzifunga na kuchezea Mpira anavyotaka.Kuhusu kuchukua EPL msimu ujao kama akiendelea kuwa Man city basi atachukua.

5.Kuhusu kusahau UEFA ungetwambia nikocha yupi wa EPL atachukua UEFA.Mimi siwezi kusema pep hatochukua au atachukua Uefa hata Man utd anaweza kuchukua ingawa ni timu mbovu ukilinganisha na Man city.

Xavi, iniest,Sergio wa Barcelona ndio hawa KDB,Silva(Gurdogan) na Fernadinho.Ndio maana unaona hata sasa ingawa man city ana beki mbovu lkn bado anazisurubu timu zenu za EPL.Maana Pep haamini zaidi ktk uzuiaji bali ushambuliaji kama ilivokuwa barca.

Man city kwa sasa Mendi,Company,stone na Silva wana injury lkn bado wanawasurubu na wataendelea kuwasurubu.
 
Kwahiyo ukatae ukubali pep kafanya uwekezaji mkubwa unaolipa.Ukiangalia wachezaji ambao Mo aliruhusu wauzwe alivyoingia Man u niwachache kuliko Pep.Kwahiyo ukaatae au ukubali pep kwa kipindi chake tangu aanze ukocha yupo mbaalii mno.

Uwekezaji umelipaje? Mwaka jana alitoka kapa! Msimu wa mwaka huu haujaisha! Sasa unasemaje uwekezaji umelipa? Au kuongoza ligi ndiyo kulipa kwenyewe?
 

Si kweli kwamba pep alimkuta Andre Iniesta yupo kwenye pick. Ukweli ni kwamba pep ndio alimpa nafasi Iniesta tena baada ya kumuuza Deco. Kumbuka Xavi na Deco ndio walikuwa viungo bora pale baca. Pep amepandisha vijana kibao toka kule timu b. Pedro, Busquet, Montoya, mark Batra, na winga mmoja hivi jina nimelisahau. Pep ndio alimuuza Keita ili kumpa nafasi Busquet baada ya kujiridhisha kuwa Busquet ni bora kuliko keita. Watu wakatoa povu ooh jamaa ni mbaguzi.

Kaja epl kakuta man city ina magalasa kibao. Kaijenga timu. Kaondoa magalasa na wazee. Kachukua vijana. Sane, Jesus, Sterling,Stone,nk. Eti mchezaji kama Fabian Delph naye kwa sasa ni bonge la mchezaji. Pep kambadilisha kabisa. Alikuwa wa kawaida.

Kingine. Kwa wale ambao mnategemea maajabu mtasubiri sana. Hivi mnajua kuwa mmiliki wa man city ndie anayemiliki club ya Girona iliyopo kule Catalona? Sasa kwa taarifa yenu tu city ina vijana wasiopungua 6 wenye vipaji vya kweli ambao wamesajiliwa na kupelekwa pale Girona kukuza vipaji.

Hawa watakuwa kama ilivyokuwa kwa Lucas Vazquiz na Asensio wa madrid. Walisajiliwa na kupelekwa kwa mkopo kwenye vilabu vingine. Sasa wamerudi na kazi zao mnaziona. Nasema Pep akikaa City kwa miaka 5 itakuwa ni ligi ya timu 1 tu.
 
Uwekezaji umelipaje? Mwaka jana alitoka kapa! Msimu wa mwaka huu haujaisha! Sasa unasemaje uwekezaji umelipa? Au kuongoza ligi ndiyo kulipa kwenyewe?
Mwaka Jana alitoka kapa kwa sababu alikuwa anajenga kikosi na alikuta timu inawazee wengi na asingeweza wabadili kwa pamoja.Ukezaji unamlipa ndio maana mechi 18 kadraw moja.Tena na hizo timu zenu bora kazitembezea vipigo.
 
Mwaka Jana alitoka kapa kwa sababu alikuwa anajenga kikosi na alikuta timu inawazee wengi na asingeweza wabadili kwa pamoja.Ukezaji unamlipa ndio maana mechi 18 kadraw moja.Tena na hizo timu zenu bora kazitembezea vipigo.
Kwa wee team kama Shitty hiyo ni achievement kubwa. Natarajia DVDs zitatoka soon!
 
we jamaa umeua kila kitu
 
Kwa wee team kama Shitty hiyo ni achievement kubwa. Natarajia DVDs zitatoka soon!
Sio mimi tu hata matajiri wa Man city ndio maana wanamuomba Pep aongeze mkataba.Kuhusu kutoa DVDs hiyo nikazi ya washabiki wa Man utd na EPL kwa ujumla.Washabiki hasa wa Man utd hamumpend pep kwa sababu mara nyingi kawaprove wrong.Mlisema kuwa hawezi ligi ya EPl leo mnalia kuwa katumia pesa nyingi.Nyinyi nani aliwakatalia kutumia pesa nyingi?.Wengine eti subiri msimu ujao tuone tena kama atachukua.Najua kuchukua bado hajachukua lkn 81% kombe ni la Pep hata wewe unajua.
 

Bro, ushaona United wanatengeneza DVDs baada ya kuzifunga timu kubwa au kuongoza ligi? Vitimu vidogo ndiyo ufanya hivyo.

Ligi hata nusu haijafika! Hiyo 81% umeikokotoaje?
 
Mkuu ulioleta huu uzi nadhani umeanza kushabikia mpira 2009... Mkuu hivi unajua ile barca ndo ilimuweka juu Pep kuwa na nidhamu kwa mtu kama Sir.Alex ferguson miaka ile alikuwa tishio sana kuliko huyu Pep kikosi kinambeba Pep...ila jamaa ni average trainer
 
Kocha mzuri sababu ya wachezai wazuri, tena wazuri kweli, je akifundisha wachezaji wa kawaida tu kama Leicester City kama Ranieri, na kutwaa EPL angeweza??!!
 
Nimekuelewa mkuu
 
Kwa sasa Zidane Yazidu Zinedine ndo kocha bora,hyo Guadiola hakuweza kutetea Uefa wala kombe la club la dunia,,,,kama siyo Zizzou nani mwingine?
 
leo imeanza hii ya kwamba next season atatoka kapa 😎😎😎 kweli nimeamini watu hawaishiwi maneno haya yetu macho na masikio
 
Pale bayern aliboronga na mbaya zaidi akaitoa bayern kwenye ile falsafa yao ya soka la kigermany na kuleta falsafa ya katalunya kitu ambacho mabosi wa bayern hawakupendezwa nacho ndio maana wakatemana nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…