Hivi,kuna kitu wanaume wengi hawajui. Mwanamke akiamua kukukomoa,utakufa kabla ya siku zako. Je,hakuna wengine wasiopata hata laki 3 na wanaishi? Kama una uhakika biashara aliua mwenyewe, basi jiandae. Ila mi ningekupa tu ushauri. Mtafutie kitu kinachouzika nyumbani hapo hapo,akapate hela ya mboga. Mahitaji mengine ya kukaa mda mrefu,nunua mwenyewe. Si yeye amefeli? Af kwa atakachokuwa anapata,utajua kipi kinaendelea. Wapo wengine hawana uchungu na jasho unalotumia kupata hiyo pesa. Na ukiuliza imefanya kazi gani,hawana majibu. Hapo ikishindikana we lea watoto wako. Japo pia kwa upande mwingine kuna sehemu mnakosea. Unazaa na mtu,watoto wawili,unamuacha unaenda kuoa kwingine. Unategemea nini? Kama si mkeo,lazima nae awe na akili ya kutafuta kianzio cha maisha. Hapo anakusanya mtaji,ili ukizingua ajue anaanzia wapi. Kwa upande mwingine namuelewa. Mi kama naona siwezi kuishi na wewe,hata kugegedana lazima niwe makini. Maswala ya mimba usikopenda,ujue utateseka mpaka unakata upepo. Labda kama watoto huwakubali.