Mkuu, umetaja ENEO, pia kujua matumizi ya fedha! Ni sahihi sana!
Tsh 800,000 kwa mwezi, watoto wawili, mama pengine na beki 3, inatosha sana kwa masuala ya maakuli!
Masuala ya sijui Bima, Ada, Bill za umeme, maji na ving'amuzi zisiwe sehemu hiyo ya 800k.
Zaidi, kama huyo mkeo naye ni mtafuta kipato, yaani masaa pengine 9 ya siku anaiacha familia mikononi mwa beki 3 na walimu, basi 800k inatosha sana tu; palipobakiwa atajazia yeye.
- Bima na Ada, mtakaa mezani kuona namna nzuri ya ku-cover
Vyovyote wasemavyo, usiruhusu kipato cha mwanamke kipotelee kusikojulikana, mpe majukumu ya kifamilia, angalau nusu ya kipato chake chote kitumike kwenye familia.