Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Akisoma majibu ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka kwa Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo ambayo yanaonesha kuna “hali ya sintofahamu” kuhusu barua iliyotumika kulifungia Kanisa la wateja wake, Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Ameyazungumza hayo leo Jui 13, 2025 Jijini Dodoma baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo Kanisa hilo linaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya Serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.
Wakili Kibatala amesema "Barua inayodaiwa ndio msingi wa rufaa ni barua ambayo sio halali na haitambuliki na Wizara hasa kwa kuzingatia kuwa barua hiyo haijasainiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia."
"Barua ile vyovyote ilivyo imesainiwa au haijasainiwa imeelekezwa kwa watu ambao wanaitwa Glory Of Christ Church ilipaswa ipelekwe kwa bodi ya wadhamini lakini ukiona pale imeandikwa Bishop Josephat Gwajima, hata kama ni sahihi kisheria kwa sababu yeye ndio mkuu wa kanisa lakini kanisa lililotajwa sio la kwetu"