Peter Kibatala: Barua ya kulifungia Kanisa la Askofu Gwajima si halali na haitambuliki na Wizara
Yani aliyeleta barua kanisani na kusambaa mitandao huku waziri wa mambo ya ndani kufungia ila baada ya kuona maji shingoni wanasema hii barua kutotamburika wizarani.

Na aliyepost Mirrad Ayo
Tukirudi nyuma kidogo kabla ya barua ni yake au si yake, hivi ile video ya uzinifu ni yeye au ni yeye halafu mkono ndio wa baunsa?🐒
 
Akisoma majibu ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka kwa Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo ambayo yanaonesha kuna “hali ya sintofahamu” kuhusu barua iliyotumika kulifungia Kanisa la wateja wake, Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Ameyazungumza hayo leo Jui 13, 2025 Jijini Dodoma baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo Kanisa hilo linaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya Serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.

Wakili Kibatala amesema "Barua inayodaiwa ndio msingi wa rufaa ni barua ambayo sio halali na haitambuliki na Wizara hasa kwa kuzingatia kuwa barua hiyo haijasainiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia."

"Barua ile vyovyote ilivyo imesainiwa au haijasainiwa imeelekezwa kwa watu ambao wanaitwa Glory Of Christ Church ilipaswa ipelekwe kwa bodi ya wadhamini lakini ukiona pale imeandikwa Bishop Josephat Gwajima, hata kama ni sahihi kisheria kwa sababu yeye ndio mkuu wa kanisa lakini kanisa lililotajwa sio la kwetu"

Zamani nilikuwa namuona kibatala ni mtu wa maana ila kumbe ni kilaza tu kelele nyingi hamna kitu kabisa hapo anawajaza upepo hao wachungaji njaa wakapigwe kesho yeye akiwa kwake anakula mbususu


USSR
 
Hii nchi ina uonevu sana, siamini hata wanaccm wapo wanaunga mkono hili. Tusijekukuta Hii nchi kuna kikundi cha matajiri wa Dubai na Oman ndo wanaongoza hii nchi (FUTUNGO) , usikute Samia na CCM pale ni wawakilishi tu, mana haiingii akilini kabisa, kabisa yani, sijawahi kuiona tanzania ya namna hii, hii nchi haipo mikononi mwa Watanzania
Pole Pole Aliwahi Kusema Genge Linaweza Kupiga Copy Serikali Halafu Likaanza Kuiongoza Kumbe Ni Bandia
 
Hii nchi ni vituko kila kukicha yaa kama wizara hawatambui Hilo Wala hakuna mamlaka iliyotoka kulisemea Hilo
Nawaza hivi inawezekana siku moja akaamka mlevi mmoja wa mbege akaandika barua na kuwapelekea police juu ya amri fulan na police wakachukua hatua bila ya kuwa na hakika ya kile wanachokitenda
 
Zamani nilikuwa namuona kibatala ni mtu wa maana ila kumbe ni kilaza tu kelele nyingi hamna kitu kabisa hapo anawajaza upepo hao wachungaji njaa wakapigwe kesho yeye akiwa kwake anakula mbususu


USSR
Mmekuja kuhamisha magori; na kupunguza kasi, namuona mwenzio tlaatlaa nae anavyovizia kupunguza upepo,
 
Kwa kutumia ile barua feki leo ungekuta Gwajima amevunjwa kiuno au ameuwawa serikali ndio ingesema kwamba hai tambui ile barua.Na kama ni feki kwa ninj hadi leo wame zuia makanisa yasi funguliwe waumini waka endelea kusali
 
Kwahio waumini wameruhusiwa na mahakama kuendelea kusali? Nataka nijue Kama niendelee na mfungo au nirudishe shukrani kwa BWANA wa vita
 
Yani aliyeleta barua kanisani na kusambaa mitandao huku waziri wa mambo ya ndani kufungia ila baada ya kuona maji shingoni wanasema hii barua kutotamburika wizarani.

Na aliyepost Mirrad Ayo
Hivi wafungiaji watachukuliwa hatua kama wengine kwa kuzua taharuki??
 
Ikiwa hivyo basi Tanzania ipo hatarini sana sana kwa maana mpaka askari waenda kuzingira jengo na kukamata waumini kisha Barua sio halali je hao Askari walipata mafunzo ya aina gani kwenye kufuatilia na kuhakiki nyaraka!!????


Hii ni wazi Tanzania yetu kuna kikundi cha watu wanafanya watakavyo kwa kila mwenye kuenda kinyume na fikra za kikundi hicho.
 
Back
Top Bottom