Peter Kibatala: Barua ya kulifungia Kanisa la Askofu Gwajima si halali na haitambuliki na Wizara
Akisoma majibu ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka kwa Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo ambayo yanaonesha kuna “hali ya sintofahamu” kuhusu barua iliyotumika kulifungia Kanisa la wateja wake, Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Ameyazungumza hayo leo Jui 13, 2025 Jijini Dodoma baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo Kanisa hilo linaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya Serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.

Wakili Kibatala amesema "Barua inayodaiwa ndio msingi wa rufaa ni barua ambayo sio halali na haitambuliki na Wizara hasa kwa kuzingatia kuwa barua hiyo haijasainiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia."

"Barua ile vyovyote ilivyo imesainiwa au haijasainiwa imeelekezwa kwa watu ambao wanaitwa Glory Of Christ Church ilipaswa ipelekwe kwa bodi ya wadhamini lakini ukiona pale imeandikwa Bishop Josephat Gwajima, hata kama ni sahihi kisheria kwa sababu yeye ndio mkuu wa kanisa lakini kanisa lililotajwa sio la kwetu"

Yaani kuna ujinga na upumbavu mwingi sana kwenye serikali ya Chura Kiziwi....

Kama kwenye uandishi wa barua simple tu kama hii wanaweza kufanya makosa ya kijinga na kipumbavu kiasi hiki, vipi kwenye mikataba ya kimataifa yenye maslahi ya nchi?

Nao polisi ikawaje kutekeleza amri isiyo halali tena kikatili vile kwa kuwa harrass na kuwadhalilisha watu waliokuwa kwenye ibada halali kabisa? Kwa tendo ovu na la hovyo itabidi wachague wenyewe adhabu ambayo Mungu angependa awape...

Na kwa uzembe na ulafi wa rushwa huuhuu, tumeuza bandari zetu za Tanganyika zote kwa waarabu...

Lakini viongozi wetu kwenye utetezi wao wanasema eti kuna maslahi kumbe hata hayajasoma mkataba kabisa ili yajue Ts&Cs za mkataba....

Yenyewe ili mradi yameoneshwa pesa tu za rushwa, mate yakawadondoka kama mbwa mwenye njaa kali na kusahau kila kitu, kumbe yanajiuza na kutuuzia nchi na mali zetu kwa wageni wa kiarabu...!!

Shame to all CCMs
 
Wajitie hamnazo hivyo hivyo,barua iko addressed kwa mkuu wa hayo makanisa,na ujumbe umefika...waende juma pili tuone kama kweli wao ni vizibo
 
Nchi yetu imejaa uhuni mwingi sanaa...sijui lini haya mauza uza yatakoma😥
 
Hii nchi ina uonevu sana, siamini hata kuna wanaccm wanaunga mkono jamo hili. Tusijekukuta Hii nchi kuna kikundi cha matajiri wa Dubai na Oman ndo wanaiongoza (FUTUNGO) , usikute pia Samia na CCM yao pale ni wawakilishi tu, mana haiingii akilini kabisa, kabisa yani, sijawahi kuiona Tanzania ya namna hii, hii nchi haipo mikononi mwa Watanzania, Sijui nani atatusaidia nimeanza kukata tamaa
Inatia hasira sanaaa....smtm unatamani jambo fulan yaan baya tu....litokee likomeshe huu uonevu
 
Makanisa yanatengeneza pesa kuliko viwanda mjomba. Huyo kuhani Msa bonge la msanii alikuwa anakula demu miaka minne bila kuoa na wanapigana mapicha mpaka zilivyovuja alafu anahubiri kilaleo kanisani na kutoa maunabii na mapepo dadadadadekiii!
Una ushahidi mkuu?
 
Je waliokuwa wamevamia kanisa na kuweka utepe walikuwa ni watu wasiojulikana? Ama watekaji?
 
Makanisa yanatengeneza pesa kuliko viwanda mjomba. Huyo kuhani Msa bonge la msanii alikuwa anakula demu miaka minne bila kuoa na wanapigana mapicha mpaka zilivyovuja alafu anahubiri kilaleo kanisani na kutoa maunabii na mapepo dadadadadekiii!
Usije ukafuta tu
 
haya ndio madhara ya kuwa na askari wenye uwezo mdogo kiakili walikurupuka kwenda kufunga na kuzuia watu eneo la kanisa bila kujua uhalali wa barua hiyo
Usifanye mchezo na Posho mzee familia zunatutegenea. Ukikaa tu kulinda doria kanisani unaingiza siku
 
Akisoma majibu ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka kwa Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo ambayo yanaonesha kuna “hali ya sintofahamu” kuhusu barua iliyotumika kulifungia Kanisa la wateja wake, Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Ameyazungumza hayo leo Jui 13, 2025 Jijini Dodoma baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo Kanisa hilo linaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya Serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.

Wakili Kibatala amesema "Barua inayodaiwa ndio msingi wa rufaa ni barua ambayo sio halali na haitambuliki na Wizara hasa kwa kuzingatia kuwa barua hiyo haijasainiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia."

"Barua ile vyovyote ilivyo imesainiwa au haijasainiwa imeelekezwa kwa watu ambao wanaitwa Glory Of Christ Church ilipaswa ipelekwe kwa bodi ya wadhamini lakini ukiona pale imeandikwa Bishop Josephat Gwajima, hata kama ni sahihi kisheria kwa sababu yeye ndio mkuu wa kanisa lakini kanisa lililotajwa sio la kwetu"

NRNE - BMHU
 
kwahiyo kiba' kesho tukaliamshe dude?tukafufue zetu watu sio?
Sasa kibata' tufungue Kesi ya madai kanisa limepoteza mapato mengi ya
1.)sadaka za kujimaliza
2.)mafungu ya kumi
3.)zaka
4.)sadaka za shukrani
5.)pesa ya kuonana na watu ana Kwa ana
6.)pesa za kuinua mikono ya askofu
6.)mbegu za kujiungamanisha
7.)pesa za kujimaliza
7.)sadaka za partners
8.)Visitors Toka nje ya nchi
9.)pesa za kuendesha media
10.)sadaka mtandaoni nk.nk
TOTAL NI BILIONI 50 NA CHENJI...WATAJUA HAWAJUI
Uzuri hizo sadaka Zote ni za Hiyari , kuliko kuwafanyia watu maamuzi juu ya Imani Zao kidini... Ni bora tuboreshe elimu yetu kuongeza uelewa ili tupate nafasi kufanya maamuzi sahihi binafsi.
 
Uzuri hizo sadaka Zote ni za Hiyari , kuliko kuwafanyia watu maamuzi juu ya Imani Zao kidini... Ni bora tuboreshe elimu yetu kuongeza uelewa ili tupate nafasi kufanya maamuzi sahihi binafsi.
Hivi ukiambiwa usipotoa mfano fungu la kumi maana yakeke unamuibia Mungu... Bado inabaki kuwa hiari??
 
Back
Top Bottom