PreGE2025 Peter Kibatala: Nitawaalika Mabalozi na Jumuiya za Kidiplomasia kwenye Kesi ya Lissu Aprili 24, 2025

PreGE2025 Peter Kibatala: Nitawaalika Mabalozi na Jumuiya za Kidiplomasia kwenye Kesi ya Lissu Aprili 24, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
..hudhani kama kungekuwa na wepesi katika kuwapatia Chadema fomu za mawakala maandamano yangeepukwa, na mauaji yasingetokea?

..mambo mengi huanza na dhuluma dhidi ya Chadema, halafu wakilalamika, au wakipinga, wanajikuta ktk mikono ya vyombo vya dola, na mahakama.
Sikumbuki vizuri lile sakata muda umeenda.

Iła hata kwa opaque memory, CDM ndio walikuwa wakorofi from outset.
 
Hebu jitahidi kuwapa huo ushauri wa kutotafuta misaada; hilo litatusaidia sana kuondokana na wakoloni hawa mapema sana.
Kwa viongozi wote waliomo ndani ya serikali ile sasa hivi, sioni kiongozi wa kusimamia nchi kujitosheleza kwa lolote. Wote ni ombaomba tupu!
Hapo sasa watafute vijana wenye uwezo, wengi wao kwa sasa huko serikalini tia maji tia maji.
 
..kesi ya uhaini inayohusisha mtuhumiwa mmoja!!
Anaye Pinga mifumo kandamizi ya uchaguzi

Wanahubiri amani kumbe watu wameamua kunyamaza wengine kunyamazishwa

Jamii kunyamaza siyo amani bali kusalimu amri majukumu ya kijamii

Silence surrenders public responsibilities
 
Kwani wewe mwenzetu ujaona bado US Aid hadi mabango ya ofisi huko marekani Elon Musk keshayatoa.

Sasa hivi US itatumia soft powers zipi Tanzania. IMF and WB hazipo directly chini ya serikali zao.

CDM ijifunze kupambana vita yake sio kukimbilia viongozi wa dini, mabalozi, kulaumu Simba na Yanga etc.

Sasa sijasema mahakamani Lissu asitendewe haki.
Kwahisi misaada yote inayopekelewa na Tz inatoka USA tu?.

Chadema itakimbilia popote ambapo inaona itasaidia kutendewa haki na sio kupendelewa, nilitegemea hata CCM na Serikal yake nao waombe haki itendeke mahala popote na ionekane imetendeka.

Rostam ni mwana CCM na mwanamtandao wa huko CCM anafahama namna gani Serikali ya CCM Ina operate juu ya utoaji haki. Inatisha mpaka majaji huko mahakamani.
 
Sioni kama anaogopa hilo. Watu majasiri hawaogopi matokea ya maamuzi yao, na mara zote hupata matokea ya wakitakacho hata kama sio kwa 100%.
Nadhani ni mtu wa calculated risks tu, lakini uoga anao. Vinginevyo asingekuwa analilia kuhakikishiwa usalama wake kabla ya kurudi.

He just tasting ‘bi-tozo’ patient and tolerance level. Mama nae katoa vijikucha vyake soon ataanza kuparura akiendelea kumtishia nyau.
 
Hapo sasa watafute vijana wenye uwezo, wengi wao kwa sasa huko serikalini tia maji tia maji.
Hiyo "...tia maji, tia maji..." ndiyo maana ya haya yote tunayo shuhudia leo hii. Watu hata wasiojuwa kipimo cha mambo gani yanastahili kumfungulia kesi ya uhaini mpinzani.
 
Kwahisi misaada yote inayopekelewa na Tz inatoka USA tu?.

Chadema itakimbilia popote ambapo inaona itasaidia kutendewa haki na sio kupendelewa, nilitegemea hata CCM na Serikal yake nao waombe haki itendeke mahala popote na ionekane imetendeka.

Rostam ni mwana CCM na mwanamtandao wa huko CCM anafahama namna gani Serikali ya CCM Ina operate juu ya utoaji haki. Inatisha mpaka majaji huko mahakamani.
Rostam is entitled to his opinion

Huko Russia au kwengineko kwenye dictatorship kesi ya serikali na wanasiasa wa upinzani. Wanasheria wao hawana ata jeuri ya kuongea wanayoongea wanasheria wa Lissu publicly. Na hearing ni private unafungwa tu.

Bado hatujui udikteta unafananaje.

I need a breather 👋
 
Jaribio lolote la kutomfikisha Mahakamani Antipas Tundu Lissu Mughwai tarehe 24 Aprili 2025 litakutana na upinzani mkali wa kisheria. Tunaamini kuwa wale walio na dhamana hawatajishughulisha na mipango ya kipuuzi ya aina hiyo.

Tunataka Antipas Tundu Lissu Mughwai ashtakiwe hadharani kabisa; aibu iwabebe wanaostahili. Bila shaka tunafahamu upande upi utabeba mzigo huo. Kama kawaida, muda ndio mwamuzi wa mwisho.

Kesho, tarehe 22 Aprili 2025, nitaandika rasmi kwa Mabalozi wa Jumuiya ya Kidiplomasia waliopo Tanzania, nikiwaalika maafisa wao kuhudhuria kesi ya Bw. Lissu iliyopangwa, ili wajionee kwa macho yao jinsi haki inavyotendeka nchini Tanzania.

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Aidha, nitaandika kwa Viongozi Wakuu wa Madhehebu Makuu ya Dini, nikiwaalika pia kuhudhuria na kushuhudia kinachofanyika kwa jina la Taifa.

Kesi hii ina athari za Kitaifa na Kimataifa; na tunahitaji uwazi wa hali ya juu.

Tunataka Dunia nzima ijionee jinsi Jeshi la Polisi la Tanzania litakavyoshughulikia haki ya Kikatiba ya Umma kuhudhuria mashauri ya jinai ya aina hii yenye uzito mkubwa; na wajifunze kwa dhahiri maana halisi ya kosa la uhaini.



Jaribio lolote la kutomfikisha Mahakamani Antipas Tundu Lissu Mughwai on 24th April 2025 will be met with stiff legal resistance;We trust that those responsible will not partake in any such hare-brained schemes.

We want Antipas Tundu Lissu Mughwai to be tried in full Public view; let the burden of shame be carried by the deserving side, of course we know which side that will be. Time is,as always,the final victor.

Tomorrow, 22nd April 2025, I will officially write to the Embassies of the Diplomatic Corp in Tanzania;inviting their Officers to attend Mr. Lissu's scheduled case,and witness Tanzanian Justice at play.

I will also write to the Heads of all major religious denominations:similarly inviting them to witness what is being done in the name of the Nation.

The case has intra-National, and International implications;and we require complete apparency.

We wish the whole World to witness how the Tanzania Police Force will be dealing with the statutory right of the Public to attend such momentous criminal proceedings;and learn for themselves what Treason actually entails.
Mwafrika bawnaa! hata akisoma kazi bureeeeh, kumbe bado tuna mentality ya mambo yetu mpaka wazungu tuwaweke mbereee! Poor AFRICA Shithole
Shame on you KIBATALA
 
Sikumbuki vizuri lile sakata muda umeenda.

Iła hata kwa opaque memory, CDM ndio walikuwa wakorofi from outset.

..ukiona CDM wanakuwa wakorofi ujue kuna dhuluma wametendewa. CDM sio vichaa kwamba waanze kufanya fujo bila kuwa provoked.

..maandamano yaliyosababisha Polisi wakamuua Aquilina Akwilini chanzo chake ni Mkurugenzi kuwanyima Chadema fomu za kiapo cha mawakala ktk uchaguzi mdogo wa Kinondoni.

..tena unaweza kusema balaa lile lilianza na Maulidi Mtulia kuamua kuunga mkono juhudi kwa kuacha ubunge wa CUF na kujiunga CCM. Baada ya hapo ukaitishwa uchaguzi mdogo wa kumchagua upya Maulidi Mtulia.

..Binafsi sijui Maulidi Mtulia na alioshirikiana nao wanajisikiaje katika nafsi zao. Maulidi mwenyewe hivi tunavyozungumza yuko nje ya siasa. Sijui lini Ccm watamkumbuka.

..Tumepata hasara ya kupoteza maisha, na watu kutiwa ulemavu. Pia tumepata hasara ya fedha za umma kuitisha uchaguzi mdogo. Bado sijazungumzia kesi dhidi ya viongozi wa Chadema, na faini walizolazimika kulipa. Baadae mahakama ya Rufaa ikaamua walihukumiwa kwa makosa!!

..Yote hayo chanzo ni UDHALIMU wa Ccm.
 
Halafu ata wakienda watasaidia nini.

Donald Trump ameshakata mirija ya nyonyo Tanzania.

Nchi kama US hana tena tools za kutumia ‘soft powers’ Tanzania ku-influence government behaviour.

Sisemi huko mahakamani haki isitendeke, ila hao wazungu wenu hawana kitu cha kuitishia nacho serikali tena kama misaada washakata tayari.
Kwamba now tunajitegemea kwa 100%, vizuri kama nikweli
 
Uwa hawatoi yote na kila mwaka budget yetu uwa na variance ya kutofikia malengo.

Siurce kubwa ya variance ni ahadi hewa za wazungu, serikali ya Tanzania ishawazoea.
Mkuu nchi kama Denmark miaka mingi wamekuwa waaminifu kulipa ahadi yao 100%
 
Nadhani ni mtu wa calculated risks tu, lakini uoga anao. Vinginevyo asingekuwa analilia kuhakikishiwa usalama wake kabla ya kurudi.

He just tasting ‘bi-tozo’ patient and tolerance level. Mama nae katoa vijikucha vyake soon ataanza kuparura akiendelea kumtishia nyau.
Kutokuwa muoga haimaanishi uwe mjinga. Naona unachanganya uoga na ujinga. Haya yanayomtokea alijua lazima yamkute, lakini ujumbe wake umefika sehemu sahihi.

Huyo mama lazima amchukulie hatua maana ndio sehemu ya madaraka yake. Lakini hatakuwa na ubavu kugomea madai ya Lisu maana ni valid, na bila mashinikizo hayawezi kupatikana. Hizi kelele za kanisa la RC na kuonyesha kuungana na Lisu, kwa vyovyote lazima limeiweka ccm kwenye wakati mgumu, maana sasa inaonekana wanahubiri amani ya mdomoni, na sio haki. Mapambano ya ya haki hayajawahi kuwa marahisi, na ni lazima wawepo wa kujitoa muhanga. Na kwenye hili Lisu amecheza kete sahihi.
 
Rostam is entitled to his opinion

Huko Russia au kwengineko kwenye dictatorship kesi ya serikali na wanasiasa wa upinzani. Wanasheria wao hawana ata jeuri ya kuongea wanayoongea wanasheria wa Lissu publicly. Na hearing ni private unafungwa tu.

Bado hatujui udikteta unafananaje.

I need a breather 👋
LOOOOooh!
Hapa ndipo huwa unanishangaza na kushindwa kabisa kukuelewa mfumo wako wa kufikiri upo vipi!
Kuna udikteta zaidi ya kumnyima mtu haki zake za kuchagua viongozi?
Kama hapa huoni udikteta, unataka uweje? Watu wanauawa kwa kutafuta tu haki ya kuwachagua viongozi au kuchaguliwa kuwa kiongozi; halafu bado unaona huo siyo u-dikteta?
 
Hii kesi ni suala la muda tu, maana kwa mwenendo wake wataabika kama ile ya mbowe ikaishia kwa DPP kuifuta kwa aibu kubwa.....ni aibu kwasababu uliona wapi magaidi wakafutiwa kesi kirahisi rahisi? Yaani ni aibu ya taifa na hii itakuwa ivo ivo haini kufutiwa mashitaka.....itakuwa aibu kwao kuanzisha makesi mazito afu wanayatupilia mbali.....dunia inawaona viongozi hamnazo kabisa
 
Baadhi ya polisi watakua wanachukia sana kwa baadhi ya maagizo ila basi tu.Sasa hapo polisi wataenda wakaaibike,huku waliotoa maagizo wapo tu wanashihudia kupitia luninga.Hii ni intimidation na jeshi la polisi unakuta linasemwa kwa ujumla wake.Inasikitisha sana,huku wakubwa wanasaini posho tu.Pole sana kwa askari ambao wanavumilia mengi.
Kwanini wasiache kazi, kuepuka adha hiyo? Lol
 
Back
Top Bottom