PreGE2025 Peter Kibatala: Nitawaalika Mabalozi na Jumuiya za Kidiplomasia kwenye Kesi ya Lissu Aprili 24, 2025

PreGE2025 Peter Kibatala: Nitawaalika Mabalozi na Jumuiya za Kidiplomasia kwenye Kesi ya Lissu Aprili 24, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Cha msingi katika kulalamika kwakwe kuhamasisha vurugu sheria inatafsiri huo ni uchochezi.

Kazi kwake huko mbeleni achague maneno yake kwa makini au kila siku atajikuta yupo lupango.
Uchochezi ni incitement. Uhaini ni treason. Tuhuma mbili tofauti kabisa.
 
Halafu ata wakienda watasaidia nini.

Donald Trump ameshakata mirija ya nyonyo Tanzania.

Nchi kama US hana tena tools za kutumia ‘soft powers’ Tanzania ku-influence government behaviour.

Sisemi huko mahakamani haki isitendeke, ila hao wazungu wenu hawana kitu cha kuitishia nacho serikali tena kama misaada washakata tayari.
Umesoma sheria?
 
Halafu ata wakienda watasaidia nini.

Donald Trump ameshakata mirija ya nyonyo Tanzania.

Nchi kama US hana tena tools za kutumia ‘soft powers’ Tanzania ku-influence government behaviour.

Sisemi huko mahakamani haki isitendeke, ila hao wazungu wenu hawana kitu cha kuitishia nacho serikali tena kama misaada washakata tayari.
Uongo misaada bado inatolewa
 
Mamluki wanaendelea kutekeleza mipango ya waajiri wao. Hamtafanikiwa ninyi na wanaowatuma. Dkt. Samia ni mpango wa Mungu. Alieletwa kuiponya nchi.
Hii nchi inaumwa saratani au,mbona ni miaka 4 sasa na nchi haijapona.
 
usiwasahau TEC gentleman na itapendeza zaidi. binafsi nitakuepo kabla sijaelekea Rome Italy:pulpTRAVOLTA:
Wajibu wa kuwaalika TEC sio wako sio wa washitaki isipokuwa washtakiwa ili jumuiya hiyo na zingine zione namna nchi inavyoendesha mambo haya nje ya utaratibu wa sheria na taratibu zingine za kibinadamu!

Jukumu lako wewe ni kuwaeleza wanaohusika na jambo hili kutambua kuwa wameendelea kufanya mambo bila kutumia walau % hata 2 ya Akili ya kawaida isiyohitaji darasa hata moja!!
 
Mamluki wanaendelea kutekeleza mipango ya waajiri wao. Hamtafanikiwa ninyi na wanaowatuma. Dkt. Samia ni mpango wa Mungu. Alieletwa kuiponya nchi.
Toa huo u dr wa mchongo,kilaz.a huyo!
 
Mama anaingizwa chaka kizembe sana na hii inaakisi tu uwezo wake na wa washauri zake. Hivi hawa watu wanaelewa maana halisi ya kesi ya Uhaini?
 
Kamanda Muliro ambaye ni polisi mwenye elimu ya sheria ya uchochoroni anabweka hovyo.
 
Hofu imetajwa kuibuka kuhusu uwezekano wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kutofikishwa mahakamani kama ilivyopangwa Aprili 24, 2025, katika kesi ya uhaini inayomkabili, hali iliyosababisha wito wa wazi kutoka kwa wakili Peter Kibatala, akisisitiza kuwa jaribio lolote la aina hiyo litakumbana na upinzani mkali wa kisheria.

Akizungumza kupitia taarifa maalum aliyoichapisha katika kurasa za mitandao yake ya kijamii, Kibatala amesema wanahofia mipango isiyo rasmi ya kuzuia au kuchelewesha kufikishwa kwa Lissu mahakamani, jambo ambalo litakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za kisheria na uhuru wa kikatiba wa kusikilizwa kwa wazi mbele ya umma.

“Jaribio lolote la kutomfikisha Mahakamani Antipas Tundu Lissu Mughwai tarehe 24 Aprili 2025 litakumbana na upinzani mkali wa kisheria. Tunaamini wale wanaohusika hawatajihusisha na mipango ya kipumbavu ya aina hiyo,” amesema Kibatala.

Katika hatua ya kuhakikisha uwazi wa mchakato wa kisheria, Kibatala amesema kuwa kesho Aprili 22, 2025 ataandika rasmi kwa Mabalozi wa Kundi la Kidiplomasia nchini Tanzania kuwaalika maafisa wao kuhudhuria mahakamani na kushuhudia mwenendo wa kesi hiyo.

“Kesi hii ina athari za Kitaifa na Kimataifa, tunahitaji uwazi wa hali ya juu. Dunia nzima ishuhudie namna Jeshi la Polisi na mahakama zetu zitakavyoshughulikia haki ya kisheria ya umma ya kuhudhuria mashauri ya jinai ya umuhimu kama huu,” ameongeza.

Mbali na mabalozi, Wakili Kibatala pia amesema atauandikia viongozi wa madhehebu makuu ya kidini na taasisi mbalimbali, kuwaalika kushiriki na kushuhudia mwenendo wa kesi hiyo, kama sehemu ya kulinda haki na kudumisha uwazi wa kidemokrasia.

“Viongozi wa dini na taasisi za kijamii wana nafasi kubwa ya kushuhudia na kushirikiana na wananchi kuona haki inatendeka bila upendeleo wala vitisho,” amesema.

Kibatala amesisitiza kuwa CHADEMA na watetezi wa haki za binadamu nchini wanataka kesi hiyo ifanyike mbele ya umma kwa uwazi, ili aibu ibaki kwa upande unaopaswa kubeba jukumu la hali hiyo.

“Tunataka Antipas Tundu Lissu Mughwai afikishwe mahakamani mbele ya umma kwa uwazi kabisa; aibu ibebwe na upande unaostahili — bila shaka tunajua ni upande upi huo,” aView attachment 3311381mesema Kibatala.
 

Attachments

  • FB_IMG_1745260357639.jpg
    FB_IMG_1745260357639.jpg
    24.9 KB · Views: 21
Mhaini lazima aonekane kwenye mahakama ya wazi, wasikilze na kuona jinsi Jamhuri ilivyoweza kubaini uhaini, na wananchi bila wasiwasi kuweza kufuatilia uchunguzi wa kesi hii nzito .
 
Hapo mashahidi wa Kipolisi wajiandae na dawa mfukoni,U.T.I zitaibuka baada ya maswali ya Kibatala kukolea
 
Rostam is entitled to his opinion

Huko Russia au kwengineko kwenye dictatorship kesi ya serikali na wanasiasa wa upinzani. Wanasheria wao hawana ata jeuri ya kuongea wanayoongea wanasheria wa Lissu publicly. Na hearing ni private unafungwa tu.

Bado hatujui udikteta unafananaje.

I need a breather 👋
Haya mkuu lakini nikuambie tu kitu kimoja, shetani Hana dini naamini na wewe utafikiwa kwa njia Moja au nyingine.
 
Back
Top Bottom