Peter Madeleka: Kutishia watu kuwapeleka Magereza ili wateseke ni Ushamba na ulimbukeni. Kuuza bandari za Watanganyika ni ufisadi

Siamini usemacho bila proof,

Na hata kama usemacho ni Kweli,

Jambazi aliyekubali kuacha ujambazi na kuchagua kuwa police, huzuia uhalifu na mianya yake vizuri kuliko police wa kawaida.
 

Lema apewe heshima ya kuwa mtabiri wa taifa kisiasa​

 

Attachments

  • 5475778-7cbee36af811d0f80109e6743290bd35.mp4
    5.1 MB
Siamini usemacho bila proof,
Proof ya Nini, mbona watu walisema patrobas ni double agent mapema kabisa ila baadae ikawa dhahihiri. Ni muhimu sana chama kujiweka mbali na Hawa moles kutoka TISS hata huyo Mwabukusi wafanye naye kazi ila akiwa huko huko NCCR sio tena aingizwe CHADEMA.

Nimeona hata kina Mwamakula sijui Askofu Maxmillian yaani watu sketchy sketchy wanakaribishwa Hadi jikoni. Lazima chama ki separate mambo ya jamii na harakati za chama. Ni ajabu sana Lissu anaenda ngorongoro alafu anasindikizwa na watu ambao sio wanachama!!

This should stop otherwise tutakuja malizwa kizembe.
 
Alikuwa jeshi la uhamiaji ,kabla yakuamua aachane na kazi malipo kiduchu

Kama
Ndg yake mwabukusi aliyeacha KAZI serikali ndani ya masaa 24 kwahiyali yake
 
Askofu Maxmillian... Loh, nimemzooooom!!

Umesema Kweli, Umakini uongezeke, bt mengine ni ya kumwachia Mungu, maana ndani ya chama pia wapo wa kutosha.
 
Aib
Aibu kabisa kubambikia wananchi kesi ili kuficha ufisadi unanavanywa na walioaminiwa maofisini.
 
Madeleka ni fisadi fulani tu ambaye alikuwa Polisi na mke wake alikuwa ofisa Ujamiaji Arusha.

Madeleka alipoacha Upolisi akawa wakili. Na wateja wake wakubwa walikuwa wahamiaji haramu ambao mkewe alikuwa anawakamata halafu anaacha "mwanya" wa kutokea kwenye ushahidi.

Hivyo Madeleka akiwa wakili wao, na mkewe akiwa prosecutor wa Immigration, walikuwa wanapiga hela ndefu kutoka kwa wahamiaji haramu.

CG Makakala akalitambua hilo ndipo akamuachisha kazi mkewe kutokana na hujuma hizo. Kilichofuata ni mashtaka yaliyomtupa ndani hadi akakubali plea bargain.

Chuki yake kwa system na kwa Makakala ilianzia hapo. Siyo msafi hata kidogo
 
Sijui kwanini unaishi maisha ya hofu sana, unachoandika hapa ni kama vile huiamini intelijensia ya Chadema, kitu ambacho binafsi sioni maana yake.

Haya mambo ya siasa siku zote hayapo static, kama hamtaunganishwa kwa sera zenu, lazima kuna mambo yatakayojitokeza yatakayowaunganisha, na pale mnapokuwa na common interest, kujitenga na wenzio ni ujinga tu.

Ni ujinga kwa sababu unapojitenga na wenzio ndio unapeleka ujumbe kwa jamii jinsi ulivyo selfish, na unapigilia misumari zile tuhuma za kusema Chadema hawapendi kujiunga na wengine wakati wa chaguzi, unaonesha vile usiyefaa kupewa nchi uiongoze kwasababu utawatenga wengine utakaowaona hauna maslahi nao, wakati hutakiwi kufanya hivyo.

Sioni ubaya wowote Chadema wanaoufanya mpaka sasa, kila hatua yao naiamini, na sio uaminifu wa mashaka, ni uaminifu wa uhakika kwasababu walishanionesha wako vizuri kuikwepa mitego ya CCM toka wakati ule wa usaliti wa Zitto Kabwe na wenzie, chama makini hakitakiwi kuwatenga watu, kinatakiwa kuishi nao kwa akili.
 
Nadhani wanashindwa kuzijibu hoja zake ndio upelekea huo msuguano
 
🤣🤣Come back ya verse moja light........
 
huyu si ndie alikimbia mahakamani baada ya kuachiwa
Vyombo vya habari siku hizi vimekuwa vya hovyo sana, vinaandika umbea wa kumfurahisha mtawala tu, ndio maana nimefuta app zote za news kwenye simu yangu, anzia Mwananchi, Ayo wote...

Bora nibaki na Al Jazeera, BBC, na Sky.
 
Huo ushindani wa wazi wa namna ya kuwapata waendeshaji hizo gati wenye tija ya kiuchumi na viwango vya ubora vya mikataba yenyewe hata kama unakodisha ndiyo matatizo yanakoanzia. Huo uchumi wa wapi unaousema?
 
Nani alikuambia sisi hatuwezi? Au kwa kuwa sisi ni wezi!, Kwa nini tusikodishe menejimenti wakati tunajenga uwezo wa kuendesha wenyewe? Kwa utaratibu huo unadhani lini tutakuwa na uwezo wa kuendesha wenyewe? Tusiwe wajinga hao tunaodhani wanaweza Kuna mahali walianzia hapo ndio tunapataka. Zamani tuliambiwa hatuwezi kujenga Barbara ya Rami Leo tunaweza baada ya mkapa kuthubitu,tuliambiwa hatuwezi kujenga BWAWA la Nyerere Magufuli akathubutu tunaelekea kuweza kwa mifano hiyo hakuna tusichoweza.
 

Naona mama ameamua kuwa kama Magufuli.
Ni mwendo wa kuwashughulikia wote wanaokosoa utendaji wa Serikali yake.

Ameamua kuvaa rasmi viatu vya mwendazake
 
Huo ushindani wa wazi wa namna ya kuwapata waendeshaji hizo gati wenye tija ya kiuchumi na viwango vya ubora vya mikataba yenyewe hata kama unakodisha ndiyo matatizo yanakoanzia. Huo uchumi wa wapi unaousema?
Njia ya manunuzi iliyompata DP World ni single source procurement method, ilitumika baada ya TPA kugundua kuwa mwarabu ndio mwenye mzigo kule Rwanda na DRC hivyo hapakuwa na sababu ya kumshindanisha na washindani wengine.

Ni kampuni yenye faida tayari kwa mamlaka ya bandari kwa maana ya kuwa na teknolojia za kisasa za ushushaji na upakiaji wa mizigo, unapomshindanisha unaweza kumpata mwekezaji mwenye mipango tofauti na DP World na ukaikosa tenda kubwa ya mizigo yake anayotarajia kuipitisha kwenye SGR yetu iliyojengwa kwa matrilioni ya pesa.

Hayo magati mengine na bandari nyingine zinatangazwa tenda kwa mtindo tofauti kwa sababu mazingira ya kibiashara na kiuendeshaji yatakuwa tofauti na yale yaliyompa DP World nafasi ya moja kwa moja ya kuendesha sehemu ya bandari yetu.
 
Dunia ya kisasa haikusubiri wewe mpaka uweze kujiendesha mwenyewe. Sababu za mheshimiwa Rais kuamua kuja na mfumo wa kisasa wa Landlord Port ni kuweza kuendana na ushindani wa bandari wa kidunia.

Sisi hao hao tunaolilia kujiendesha ndio hao hao ambao CAG kila kukicha anatoa report chafu anapofanya ukaguzi!.

Kumbuka kuwa mojawapo ya masharti ya kimkataba aliyowekewa DP World ni kuhakikisha anatoa elimu ya masuala ya usafirishaji wa majini kwa vijana wetu. Ni kuhakikisha anaendeleza uwezo wa vyuo vya bandari.

Mawazo ya kijamaa mara nyingi yanakosa mashiko kwenye dunia halisi, ni njozi zenye kudanganya watu kupitia akili za 'sisi tunaweza'.

Si ajabu mwanazuoni mmoja wa Marekani aliwahi kusema Ujamaa huishiwa nguvu pale watoa pesa wanaposhindwa kuendelea kuhudumia uchumi wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…