Piariz Hizza adaiwa kunyongwa na mumewe mpaka kufariki dunia

Kuendelea kumuona hasira zitawaka unajiondikea tu, ajira na mengine utapata uendako
 
hapa tstizo ni serikali niulize kwanini? lazima serikali woke sheria kali kwa mtu kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu hata watu wanandoa kujamiana kuwepo na adhabu kali za hapo.kwa papo huu upuuzi utaisha.
Umeona mbali
 
hapa tstizo ni serikali niulize kwanini? lazima serikali woke sheria kali kwa mtu kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu hata watu wanandoa kujamiana kuwepo na adhabu kali za hapo.kwa papo huu upuuzi utaisha.
Ukifumaniwa live na Mke WA MTU unapigwa life sentence hapo mambo yatapungua.

Haiwezekan watu wanauana Kwa MTU mmoja kwenda kusababisha chaos kwenye familia uliyokuwa na amani. Watoto Wanakuja kuteseka!


Please serikali make sure mnakuwa active na sheria zenu don't be that rigid
 
Pole sana mkuu..I feel your pains,baadhi ya wanawake ni pasua kichwa.
Inafikia hatua unajiuliza hivi anatumia akili zake kufanya haya au karogwa!
Mkuu inakuwa ni changamoto kweli kweli. Nikisoma matukio ya wanandoa kudhuriana, huwa nakaa kimya nikikumbuka yote niliyopitia. Niliingia kwenye addiction ya ngumu kumeza na ikakaribia kunipoteza kabisa, lakini inawezekana iliniondelea jangga lingine la kutoa roho ya mtu. Sasa maisha yanasonga salama kabisa, muda ndio unakimbia kwa kasi tu.
 
Umenena vema mkuu
Kila mwenye ndoa anatakiwa aiheshimu ndoa yako. Kwani kuna mwanamme anakulazimisha kuwa naye au tamaa tu. Tujifunze kusema hapana na kukaa mbali na watu wanaorishawishi kusaliti ndoa zetu. Eti wanaume acheni kutembea na wake za watu, ukijirahisisha wanapita na wewe tu. Tamaa haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Hii si hali ya kawaida, zinahatijika jitihada za polisi kufanya utafiti wa haya masuala.
 
Kuna report ya utafiti nimeisoma leo tana JF, kuwa wa Tz 7m wana ugonjwa wa akili.
 
Biblia inasema Mshahara wa dhambi ni Mauti. Mungu ndie ajuwaye yote. Hakuna kifo kinatokea kwa bahati mbaya ipo sababu sisi sote hatuijuwi ila Mungu peke yake.
 
Sheria kali za nini? Mtu mzima na akili yako uwekewe sheria. Ukiona huwezi kuwa muaminifu kaa mbali na ndoa. Yaani mwizi ambaye anaiba afungwe miaka 2-15 halafu watu waliokubal8ana kwa hiyari yao mmojawapo afungwe miaka 30. Huu ni ujinga.
 
Kuna ndugu Yangu ana mke na watoto watatu.

Sasa hivi wapo kwenye mgogoro mkubwa na jamaa kaamua kumuachia nyumba yeye kaenda kupanga Ila mwanamke hataki kakataza watoto kumuita ndugu yetu Baba.

Huyo mama ameenda kubadiri ubini WA watoto kwenye vyeti vya kuzaliwa Hadi shuleni.

Hivi ninavyoongea sidhani jamaa hatafanya tukio la kikatiri Hadi mwaka huu kuisha! Ana mawazo sijapata kuona.



Ujumbe Kwa Dada zangu: Chungeni midomo. Midomo inaweza kuwafanya mmoja akaenda mochwari na mwingine Gerezani. Kuweni na busara kipi cha kuongea na Kwa wakati gani.


Naombeni mumuombee ndugu yangu
 
Mabloo zetu huwa mnaoa Malaya tukiwaambia mnatufokea
 
Wanawake midomo, midomo,midomo na tuna kauli tata mnoo,zinakeraa na zinaumiza mnoo baasi tu!,afu kutukana Mwanaume ni kumdhalilisha mnoo uanaume wake ndo tunapopigwa hapo afu mbele ya watoto
Tatizo kubwa ni kukosa busara. Huwezi kutoleana matusi au maneno ya kukera kwa kwa binadamu mwenzako hata iweje. Ukiwa na hekma hata mtu akuuzi vipi huwezi kumtolea mameno ya machafu. Nilipitia ndoa ngumu kwa miaka 5, na kisa changu niliandika humu. Sikuwahi kumtukana yule mwanaume, niliamua kuondoka ili kupisha shari. Tujifunze kuheshimiana , kuwa waaminifu na kila mmoja aheshimu mipaka yake.
 
Soma alama za nyakati


Utakuja kuwekewa sumu ya panya ndogo ndogo kwenye chakula baada ya miaka 10 figo, maini , mapafu yanaharibika inakuwa imeisha hiyo!

Be careful bro
 
Ndio muone wazazi wanaona mbele zaidi yetu. Mzazi akikupa warning tu ujue kuna jambo. Kaka yangu naye aliambiwaga na mama kuwa huyu unayetaka kumuoa sio, akaona mama naye , kilichompata hatakisahau mpake leo. Karudi hadi kijijini kuanza maisha upya kisa mwanamke
 
Mpeleke kanisani akatibiwe kiimani na kisaikolojia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…