Wakuu kuna habari mbaya Huko Tabata-Dar Es Salaam.
Anasimulia Ndugu wa Marehemu.
Piariz Charles Hizza ni mdogo wangu, alikuwaga humu Friends of Solo Mnamunga kipindi fulani simu yake ilipopata matatizo akatoka sikukumbuka kumrudisha tena.
Leo mida ya mchana nikapokea simu nikaambiwa dogo amejinyonga chumbani kwake, anaishi Tabata.
Lakini, polisi wakafika na wakachukua mwili na wakamchukua na mume wake mpaka staki shari.
Uchunguzi wa awali ukaonyesha Piariz amepigwa probably na mumewe labda na akaamua kumnyonga na kutudanganya amejinyonga ili kutupoteza maboya.
Tumekuta mwili ukiwa hauna nguo sakafuni zaidi ya kufunikwa shuka na una majeraha ya kipigo na ametoboka shingon.
Mumewe anasema amejinyonga kwenye feni, lakini kwa unene wa Piarizi hawez panda akakuta feni ajiue wakati mumewe kalala humo humo chumbani asijue
Dada wa kazi anasema ilipofika saa 1 au 2 akasikia wanagombana chumbani,kufika saa 3 akasikia kimya.
Kufika saa nne mume akatoka chumbani anali anamwambia dada yako amejinyonga..akaingia akakuta mwili sakafuni na watoto wakiwa wanalia. Solo