Picha hii inasema sana kuhusu siku zijazo kwa siasa na uongozi wa Tanzania

Picha hii inasema sana kuhusu siku zijazo kwa siasa na uongozi wa Tanzania

Picha husema bila maneno. Tunakoelekea ndio huko picha hii inavyotueleza. Yaliyopita pia yameoneshwa kwenye background ya picha hii.

Tanzania tunayoelekea ni Tanzania ya mazungumzo na maelewano, Tanzania ya demokrasia na sio Tanzania ya kiburi na maamuzi binafsi.

Demokrasia itang’ara zaidi kuliko uhafidhina. Wasiopenda demokrasia wataachwa nyuma na hawatakuwa na marafiki. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Tufafanulie wengine vilaza,naona suti gwanda,suti Kaunda na suti tai 🦅.Pia kama wakati wakati umerudisha saa yako nyuma kadiri ya miongo mmoja,🤔Ila binafsi umeniacha sijui wadau wengine 🤔
 
Tufafanulie wengine vilaza,naona suti gwanda,suti Kaunda na suti tai 🦅.Pia kama wakati wakati umerudisha saa yako nyuma kadiri ya miongo mmoja,🤔Ila binafsi umeniacha sijui wadau wengine 🤔
Mbona iko clear sana? Hebu soma tena uzi upya.
 
Picha husema bila maneno. Tunakoelekea ndio huko picha hii inavyotueleza. Yaliyopita pia yanaonekana kwenye picha hii.

Tanzania tunayoelekea ni Tanzania ya mazungumzo na maelewano, Tanzania ya demokrasia na sio Tanzania ya kiburi na maamuzi binafsi.

Mwanga utajadiliana na giza, na demokrasia itang’ara zaidi kuliko uhafidhina. Wasiopenda demokrasia wataachwa nyuma pamoja na tai zao hawatakuwa na marafiki, watafifia.

Atakayetuongoza miguu yake imetangulia wengine, kavaa kama askari wa demokrasia, atasikiliza hekima za watangulizi wake kwa unyenyekevu na ni mwingi wa fikra na atatuvusha! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Na hakuna haja ya kuwa na vyama vya upinzani mana kila kitu watakuwa wanakubali tu.
Jana mwamba kaalikwa tena kula futari Ikulu....Kuna haja gani kiongozi wetu wa mapambano anashinda na adui yetu wa maendeleo analamba tu Asali?
 
Mbowe hatakuja kuwa Raisi wa Nchi hii. Hilo, uwe nalo katika mawazo yako.


Katiba hairuhusu mtu aliyeshitakiwa kwa Ugaidi kuwa Raisi.

Hakika tutaona picha nyingi tu.
 
Mkuu picha hiyo inatafakarisha sana.
Picha husema bila maneno. Tunakoelekea ndiko huko picha hii inakotuelekeza. Yaliyopita pia yanaonekana kwenye picha hii.

Tanzania tunayoelekea ni Tanzania ya mazungumzo na maelewano. Ni Tanzania ya demokrasia na sio Tanzania ya kiburi na maamuzi binafsi.

Mwanga utajadiliana na giza, na demokrasia itang’ara zaidi kuliko uhafidhina. Wasiopenda demokrasia wataachwa nyuma na hawatakuwa na marafiki, watafifia na kusahaulika.

Angalia, atakayetuongoza miguu yake imetangulia wengine, kavaa kama askari wa demokrasia, anajua siasa si uadui.

Alivyosimama, anaonekana ni mwamba anayewategemeza wengine. Anasikiliza hekima za watangulizi wake kwa unyenyekevu, ataongeza na hekima zake mwenyewe na atatuvusha! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Tena inaweza kuangaliwa sambamba ni hii nyingine hapa chini
JamiiForums1887435011.jpg
 
Back
Top Bottom