PICHA: Putin aliishi Tanzania 1973 hadi 1977 akiwa kama mkufunzi kwa wapigania uhuru

PICHA: Putin aliishi Tanzania 1973 hadi 1977 akiwa kama mkufunzi kwa wapigania uhuru

ukweli ambao wengi hawataki kuubali ni kwamba mfumo wa kutafuta elimu tz, kuanzia primary-chuo kikuu, ni time consuming.

miaka 7 primary + miaka 4 olevel + miaka 2 high level + miaka 3 chuo = 16. hayo ni matumizi mabaya ya muda.

mbaya zaidi kuna degree zinaenda mpaka miaka nne mpaka mitano.
Halaf unamaliza bila hata 100.. unaanza tembeza bahasha ubahatishe.. au mtu akuonee huruma akupachike mahala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You have hit someone hard with good arguments and examples. But in the end you have completely ruined it by calling that guy nitwit (a foolish person). If he knew english, he/she would answer you with arguments and examples. The problem with this language is that it comes with canoes, so it's just a matter of tolerance[emoji38][emoji38][emoji38]
Thank you for your good advise and guidance.
Together we stand.
 
Rahisi sana fanya hivi mtoto aanze grade 1 akifika grade 2 kabla ya term ya pili kuisha mpeleke kayumba darasa la 3 then akiingia la darasa 4 baada ya mtihani mwaka unaofata mrudishe English medium tena grade 6 then atamaliza grade 7 kwa miaka 5 tu alafu mpeleke kenya secondary kule wanapiga 4 yrs only alafu then aende technical college kwa 4 yrs tena.Atakuwa amepiga jumla ya miaka 13 tu shuleni plus ni 3 ya kindergarten jumla 16 yrs kama akianza na miaka 3 akiwa na miaka 19 tayari ana professional yake ata akianza na miaka 5 sio mbaya kwani by 21yrs of age ana professional tyr

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
No ujinga tu huo taabu yote ya nni
 
Wanamapinduzi hua hawafi haraka angalia Kagame, Museveni, Putin, nakadhalika
Mbona Che Guevara ambaye naweza sema ndiye mwana mapinduzi kuliko mwana damu yeyote karne ya 20, aliondoka akiwa mchanga sana
 
Zakuambiwa changanya na zako.
Putin alizaliwa 07/10/52 hiyo picha hapo sio ya kijana wa miaka 20.
Lakini pia '73 Putin alikua mwaka wa kwanza chuoni akichukua shahada ya Sheria. Alihitimi '75.
Siku nyingine ukiona kitu, usikimbilie kuposti, nenda Google ukacheki facts Kama Zina tally.
Sawa kilaza?
sawa mhasibu tumepata.
 
Kwahiyo sisi hatuna shida? Mbona wanafunzi wetu huko ukrein wapo kwenye mahandaki!!! Si wajitokeze mbele ya majeshi ya urusi wakipaza sauti zao "Sisi ni wenzenuuuuuu"
 
Hiyo picha siyo Putin wameedit tu. Tujifunze kufuata ukweli.
 
photo-putin.jpg

Vladimir Putin, watatu kutoka kushoto, anayemfuatia ni Rais wa zamani wa Msumbiji, hayati Samora Machel, wakiwa pamoja na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Munangagwa. Picha hii ilipigwa Bagamoyo mwaka 1973.

Inaelezwa kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitumia muda wa miaka minne kuishi na kufanya kazi Nchini Tanzania.

Putin ambaye kwa sasa anateka vichwa vya habari kwa maamuzi yake ya kuamuru majeshi ya nchi yake kuishambulia Ukraine, alikuwa mkufunzi wa wanaharakati wa Afrika kutoka nchi kadhaa zilizounda Umoja wa Afrika (AU) katika miaka ya 1970.

Inadaiwa aliishi Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1977. Picha kuonyesha ushahidi wa stori hii ulitolewa miaka kadhaa iliyopita na chombo kimoja cha habari nchini Zimbabwe.

Kwa mujibu wa mtandao wa iHarare wa Zimbabwe ni kuwa bosi huyo wa zamani wa Taasisi ya KGB alifanya mafunzo hayo katika maeneo tofauti lakini hasa yaliwahusu wapigania uhuru katika maneo ya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani.

Wakati huo Tanzania ilikuwa ikitumika kama sehemu ya kupangia mipango mingi kutokana na utulivu, na ilihusika katika kusaidia mataifa kadhaa kwenye harakati za kujikomboa kutoka kwenye ukoloni.

Wapigania uhuru wengi wa Msumbiji na Afrika Kusini walikuwa Tanzania katika Miji ya Morogoro na Bagamoyo.

Zamani pia kulikuwa na wataalamu wengi wa afya kutoka Tanzania ambao walikuwa wakilekea Moscow Nchini Urusi kwa ajili ya kupata mafunzo na elimu zaidi.

Mtu mwingine maamrufu ambaye alitua Tanzania kimyakimya ni mwanaharakati Che Guevara ambaye aliishi Dar es Salaam kuanzia Februari 11 hadi 18, 1965.

Guavara inaelezwa kuwa alitembelea Tanzania mara mbili, ikiwemo kwenda katika Kreta ya Ngorongoro ambapo alionekana hadharani Februari 18, 1965 alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Bagamoyo.jpg

Moja ya majengo ya Bagamoyo, sehemu ambapo Vladimir Putin alikuwa akiwapatia mafunzo wapigania uhuru wa Afrika.

PUt.jpg

Rais Putin akiwa katika muonekano tofauti.


Source: Tanzania Times
 
Back
Top Bottom