Vladimir Putin, watatu kutoka kushoto, anayemfuatia ni Rais wa zamani wa Msumbiji, hayati Samora Machel, wakiwa pamoja na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Munangagwa. Picha hii ilipigwa Bagamoyo mwaka 1973.
Inaelezwa kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitumia muda wa miaka minne kuishi na kufanya kazi Nchini Tanzania.
Putin ambaye kwa sasa anateka vichwa vya habari kwa maamuzi yake ya kuamuru majeshi ya nchi yake kuishambulia Ukraine, alikuwa mkufunzi wa wanaharakati wa Afrika kutoka nchi kadhaa zilizounda Umoja wa Afrika (AU) katika miaka ya 1970.
Inadaiwa aliishi Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1977. Picha kuonyesha ushahidi wa stori hii ulitolewa miaka kadhaa iliyopita na chombo kimoja cha habari nchini Zimbabwe.
Kwa mujibu wa mtandao wa iHarare wa Zimbabwe ni kuwa bosi huyo wa zamani wa Taasisi ya KGB alifanya mafunzo hayo katika maeneo tofauti lakini hasa yaliwahusu wapigania uhuru katika maneo ya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani.
Wakati huo Tanzania ilikuwa ikitumika kama sehemu ya kupangia mipango mingi kutokana na utulivu, na ilihusika katika kusaidia mataifa kadhaa kwenye harakati za kujikomboa kutoka kwenye ukoloni.
Wapigania uhuru wengi wa Msumbiji na Afrika Kusini walikuwa Tanzania katika Miji ya Morogoro na Bagamoyo.
Zamani pia kulikuwa na wataalamu wengi wa afya kutoka Tanzania ambao walikuwa wakilekea Moscow Nchini Urusi kwa ajili ya kupata mafunzo na elimu zaidi.
Mtu mwingine maamrufu ambaye alitua Tanzania kimyakimya ni mwanaharakati Che Guevara ambaye aliishi Dar es Salaam kuanzia Februari 11 hadi 18, 1965.
Guavara inaelezwa kuwa alitembelea Tanzania mara mbili, ikiwemo kwenda katika Kreta ya Ngorongoro ambapo alionekana hadharani Februari 18, 1965 alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Moja ya majengo ya Bagamoyo, sehemu ambapo Vladimir Putin alikuwa akiwapatia mafunzo wapigania uhuru wa Afrika.
Rais Putin akiwa katika muonekano tofauti.
Source: Tanzania Times