Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Tukisema JPM KAULIWA NA TEAM MSOGA WANASEMA SISI NI WACHOCHEZI WAKATI HAYA YANAYO TOKEA NI USHAHIDI KAMILI WA WAHUNI WALIO NDANI YA CCM NA SERIKALI, na ninaposema kuwa jpm alikuwa mpole sana alitakiwa kuteketeza kizazi kichafu yeye akakiacha...sasa kimeshika uongozi tena .....wanatuambia SABAYA NI JAMBAZI SASA HAPA NI NANI JAMBAZI SABAYA KAMWAGA DAMU YA NANI ? MBONA HAPA TUNAONA DAMU TUPU .....MAJUZI ZIMEMWAGWA SUMU MTONI WATU WAMEPATA MAAFA SERIKALI INATAKA TUAMINI KUWA NI MAJI KUCHAFUKA KWA KINYESI WAKATI UKWELI UNAJULIKANI
 
Hili suala la Ngorongoro lina utata mkubwa sana ambapo hadi sisi wenye akili nyingi tunashindwa tusimamie wapi..🤔. Hapo Ngorongoro kuna makundi manne yanayoleta utata mtupu; wamasai, serikali, mwekezaji wa Loliondo na wanaharakati.

Serikali ina hoja za msingi sana kwanini watu wahame Ngorongoro. Ile hoja ya kulinda wanyama na hifadhi ya Ngorongoro isipotee ni hoja yenye nguvu sana. Kinacholeta utata ni kuaminika kwa serikali kwamba tayari imewajengea nyumba za kuhamia huko Handeni. Je ni kweli? Je, yale makubaliano ya Arusha yalihusisha wamasai wa Ngorongoro kweli au kuna mamluki waliowasemea wenzao wa Ngorongoro?

Wamasai wao hawana hoja zenye nguvu sana za kung'ang'ania kubaki Ngorongoro ila haki za binadamu zinawalinda. Huwezi kuwatoa kama unatoa mifugo porini. Lakini na wao wanafuata sheria za kukaa hifadhini? Tumeona wengine tayari washajenga mijengo ya balaa ndani ya hifadhi kitu ambacho sio sahihi.

Huyu mwekezaji wa Loliondo nae ni kero kubwa kwa wamasai. Ninawalaani wote waliompa hilo eneo kwa mkataba mbaya kuwahi kutokea hapa nchini. Inasemekana yupo nyuma ya huu mgogoro. Wanaharakati walioko against serikali wengi wao sio wazalendo zaidi ya kuwatumia wamasai kupiga hela za mabeberu.
 
Haisaidii, dunia ya siku hizi hata wakifungia vyombo vya habari juu ya hili bado taarifa zitasambaa tu.
 
Huna macho makali boya wewe, umeangalia kwa mrengo wa kisiasa. Sasa watakula kichapo non stop, ambianeni mapema.
Eti boya hahaha......unaongea as if una una uwezo wa kutembeza kichapo....
Sasa nikuambie tu...Serikali itakaa nao na wataondoka bila ugomvi wowote sawa wewe dada....

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Hamna sababu za msingi kuwahamisha hawa watu, anyway madhira haya ni mwanzo wa kujua dhima za watawala
 
Hiki ndicho wanaharakati walikuwa wanakitafuta, wameshapata pa kuanzia na watapata pesa sana kwa kupitia hii.

..Na aliyesababisha wanaharakati kupata walichokuwa wanakitafuta ni nani?

..Kwanini hazikufanyika jitihada kuhakikisha wanaharakati hawapati hicho walichokuwa wakikitafuta?
 
Kati ya viongozi wa hovyo hii nchi ni huyo PM.
Huyu mwamba sijui anatumiwa na mamlaka au niaje aisee, hiyo ishu ya ngorongoro yeye keshamwagiwa zigo la nnya tayari na hana jinsi ya kutoka.

Ikiwa ni kweli hayo yanaendelea huko umasaini na madhara yakatokea aisee huyu PM atadhihirisha huo uhovyo wake tangu alipoudanganya umma mbele ya madhabahu kua mtu mzima kumbe kafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…