Pointers kwa wote wanaohofia usalama wa maisha yao kwa sababu ya harakati zao

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Matukio ya watu kuvamiwa majumbani mwao na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi yamezidi sasa.

Cha kushangaza, polisi nao huja kukanusha kuwa haikuwa wao.

Mfano, uvamizi kwenye nyumba ya mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali hapo jana.

Watu hao wakiwa wanavamia, hujitambulisha kama polisi.

Wakishamaliza hiyo kazi yao, Polisi [hivi Kiswahili cha polisi ni nini?] Tanzania hukanusha kuwa hawakuwa wao.

kwa kiasi kikubwa polisi hawana ubunifu wowote ule. Wanachoweza ni kutumia nguvu za silaha. Nguvu za mwili hawawezi kuzitumia maana wengi wao hawana hizo nguvu.

Sasa basi, ili kuwa hatua kadhaa mbele yao, nashauri hivi:

Wanaharakati wote waliopo nchini kufunga kamera kwenye makazi na ofisi zao.

Hizi si zama za ujima. Ni zama zama za kidijitali.

Kuna kamera za kila aina siku hizi. Funga kamera ndani ya nyumba kwenye sehemu-mkakati, funga nje ya nyumba, weka ring doorbell camera pia.

Na wala haigharimu hela nyingi. Kama mtu hali yake ya kiuchumi si nzuri, crowdfund. Nenda GoFundMe huko ukachangishe. Ikibidi weka hata sababu ya uongo.

Cha muhimu ni kuchangisha fedha ili upate hela za kujipatia nyenzo za usalama wako.

Sina hakika, ila sidhani kama nyumba ya Mdude ilikuwa imefungwa kamera.

Kama kungekuwa na kamera, ingekuwa ni rahisi sana kujua kama hao walioenda kumteka na kumpiga, ni polisi kweli au la.

Sura zao zingekuwepo kila mahala na wananchi wangeweza kuwatambua ni akina nani.

Polisi wanakanusha si wao kwa sababu wanadhani hakuna picha za hao watu. Ukosefu wa picha unawarahisishia kazi ya kukana kuwa si wao.

Imagine hapo nyumbani kwa Mdude kungekuwepo na kamera halafu zirekodi tukio lote….halafu baada ya polisi kukana, watu wanatoa video iliyozinasa sura na sauti za hao watu.

CHADEMA na wanaharakati wengine ni lazima muwe wabunifu. Ni lazima muwe hatua nyingi mbele dhidi ya serikali na dola zake.

Hakuna ugumu wowote ule kui outsmart serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya dola kwa sababu ni vilaza.

Muda wa unyonge ukome sasa. Enough is enough.
 
Ndio maana wale wote washenzi idara ya polisi ndio mama kawapa vyeo mpaka mwengine ni IGP.
Huyu mama ana mwisho ambao sio mzuri.

Na kuna tabia ya jeshi la polisi huu mtindo ikitokea wamefanikiwa wanakana kuwa sio wao ila wakishambuliwa au kugundulika usema wanaingiliwa majukumu.
 
Kwa kujazia hapo...
Hizo camera zina DVR ambazo hutunza video zinazorekodi, Polisi wakifika wanaweza kuziharibu kufuta ushahidi, hapo inabidi camera ziwe connected na cloud, muda huo huo taarifa zinakwenda kwenye cloud storage.

Wamiliki pia silaha kama pepper spray na taser.. lakini nzuri zaidi silaha za moto

Waweke na motion sensors light, mtu akisogea taa ziwake..

Hata mawasiliano yao, watumie apps zenye ulinzi (mfano signal) kwa maana maadui wanaweza kufahamu maongezi yote..

Nyumba zao waziandae kwa ajili ya tahadhari kujificha ama kutoroka..
 
Kwa kujazia hapo...
Hizo camera zina DVR ambazo hutunza video zinazorekodi, Polisi wakifika wanaweza kuziharibu kufuta ushahidi, hapo inabidi camera ziwe connected na cloud, muda huo huo taarifa zinakwenda kwenye cloud storage.

Wamiliki pia silaha kama pepper spray na taser.. lakini nzuri zaidi silaha za moto

Waweke na moton sensors light, mtu akisogea taa ziwake..

Hata mawasiliano yao, watumie apps zenye ulinzi (mfano signal) kwa maana maadui wanaweza kufahamu maongezi yote..

Nyumba zao waziandae kwa ajili ya tahadhari kujificha ama kutoroka..
Yes!

Whatever it takes.

Mdude angekuwa na kamera si ajabu tungekuwa tushaziona sura za hao watu.

Na sura zao zikionekana, lazima kuna wananchi watawatambua tu.

Sisi wananchi tukianza kuwajua hao wahalifu, inakuwa rahisi kudili nao huku mtaani.

At some point lazima watu tuheshimiane bana.
 
Matukio ya watu kuvamiwa majumbani mwao na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi yamezidi sasa.

Cha kushangaza, polisi nao huja kukanusha kuwa haikuwa wao.

Mfano, uvamizi kwenye nyumba ya mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali hapo jana.

Watu hao wakiwa wanavamia, hujitambulisha kama polisi.

Wakishamaliza hiyo kazi yao, Polisi [hivi Kiswahili cha polisi ni nini?] Tanzania hukanusha kuwa hawakuwa wao.

Sasa ni hivi, kwa ujumla haya majeshi yetu, polisi, magereza, wanajeshi, n.k., huwa si watu wenye akili kivile.

Kuanzia juu mpaka chini, naweza kusema karibu wote ni vilaza tu.

Ni watu wasio na ubunifu wowote ule.

Wanachoweza ni kutumia nguvu za silaha. Nguvu za mwili hawawezi kuzitumia maana wengi wao hawana hizo nguvu.

Sasa basi, ili kuwa hatua kadhaa mbele yao, nashauri hivi:

Wanaharakati wote waliopo nchini kufunga kamera kwenye makazi na ofisi zao.

Hizi si zama za ujima. Ni zama zama za kidijitali.

Kuna kamera za kila aina siku hizi. Funga kamera ndani ya nyumba kwenye sehemu-mkakati, funga nje ya nyumba, weka ring doorbell camera pia.

Na wala haigharimu hela nyingi. Kama mtu hali yake ya kiuchumi si nzuri, crowdfund. Nenda GoFundMe huko ukachangishe. Ikibidi weka hata sababu ya uongo.

Cha muhimu ni kuchangisha fedha ili upate hela za kujipatia nyenzo za usalama wako.

Sina hakika, ila sidhani kama nyumba ya Mdude ilikuwa imefungwa kamera.

Kama kungekuwa na kamera, ingekuwa ni rahisi sana kujua kama hao walioenda kumteka na kumpiga, ni polisi kweli au la.

Sura zao zingekuwepo kila mahala na wananchi wangeweza kuwatambua ni akina nani.

Polisi wanakanusha si wao kwa sababu wanadhani hakuna picha za hao watu. Ukosefu wa picha unawarahisishia kazi ya kukana kuwa si wao.

Imagine hapo nyumbani kwa Mdude kungekuwepo na kamera halafu zirekodi tukio lote….halafu baada ya polisi kukana, watu wanatoa video iliyozinasa sura na sauti za hao watu.

CHADEMA na wanaharakati wengine ni lazima muwe wabunifu. Ni lazima muwe hatua nyingi mbele dhidi ya serikali na dola zake.

Hakuna ugumu wowote ule kui outsmart serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya dola kwa sababu ni vilaza.

Muda wa unyonge ukome sasa. Enough is enough.
Mara nyingi matukio hayo yanakuwa planned and executed na TISS agents. Hiyo idara imekuwa ikitumiwa vibaya na watawala. Kwa kifupi, wale ndiyo majambazi rasmi wa Serikali.
 
Diaspora kazi yao ni kushauri kisha wala vumbi muingie field kutekeleza.

Mdude angechanganya na zake diaspora wasingemponza.

Diaspora wanakujza hasira unaingia kupambana na dola unapoteza uhai wako wao wanarudi mitandaoni kuonesha wamesikitika sana.
 
Soon itakuja sheria kudhibiti matumizi ya camera za usalama majumbani kama ilivyoletwa kwenye drones!

Mpaka kibali cha mamlaka na leseni ulipie kila mwaka hivyo watajua kabla hawajakufuata,kama umeweka wanakuvizia barabarani kama yule kada wa CCM kule Mwanza mwenye CCTV nyumbani kakamatwa barabarani akitoka jogging.
 
Back
Top Bottom