Poleni sana jobless, ila na sisi ndugu zenu wa halmashauri hali ni mbaya

Poleni sana jobless, ila na sisi ndugu zenu wa halmashauri hali ni mbaya

Ualimu ana tgts ipi na uafisa usafiri tgs c1 Kwa dip!

Atapata chenji ya mafuta ya misiba, misafara ya mwenge na mitihani.
Atashirikiana na wauza mafuta kuandika Lita hewa.
Atakuja kuwa mchepuko wa dereva wa mkurugenzi au dt
Ualimu na usafiri vyote alisomea dip anasema atabaki na mshahara wake uleule wa ualimu ngazi ya diploma

Kama vichenji vyenyewe ndiyo hivyo ataishia kupata vihela vya kula, nauli na vocha
 
Huyu atakuwa yupo DC moja Chaka sanaa, mapato hakuna na njaa Kali..
Watumishi wa DC za kama..
Mpimbwe
Tanganyika
Ileje
Momba
Ukerewe
Rombo
Kigoma
Tabora
N.k
Lazima walie njaaa

Mwambie atafute shavu la kuhamia halmashauri kama Kinondoni, Mwanza Jiji, Arusha Jiji, Kigamboni, Mufindi N.K ili akalambe asali kwa urefu wa field yake.

#YNWA
 
Naelewa magumu wanayo pitia wanao tafuta ajira, kula yao tu MUNGU anasimamia.

ila kuna ndugu zenu wamepata ajira halmashauri nao kichwa kinapasuka kwa madeni, stress na uduchu wa mishahara.

Hela ya kujikimu tu haipatikani licha ya serikali kuu kulikemea swala hili kila mara lakini wapii.

Rais samia tukumbuke huku halmashauri maslahi yetu ni hafifu sana na hela za kujikimu hazipatikani
Sasa wewe braza unaajiliwa Ukerewe, Rombo, Tabora, Kigoma, Momba, Ileje, Mpimbwe, Sumbawanga KWANINI USILIE NJAA?

#YNWA
 
Hawana huo muda.

Yaani pesa ya kujikimu tu tatizo, sijui huwa wanawazaga nini?
Tafuteni mashavu huko kwenye Halmashauri zenye akili.
Hata kama mshahara mdogo ila fursa ni nyingi.

Naamini ukiajiriwa Mfano Kinondoni pale wewe ndio mtendaji au mwalimu unakufaje njaa na nyomi lile la raia.

Ila sasa umeajiriwa Ileje huko ndani ndani, Mpimbwe huko mwisho wa lami, Ukerewe huko kwenye maji, Rombo chakaa kwa wachaga UMASIKINI LAZIMA.

#YNWA
 
Acheni kulialia. Sisi tunaofanya biashara tunakutana na machungu mengi sana sema tuna ujasiri kuliko makundi mengine. Imagine mimi niliagiza mzigo niuze krismas na mwaka mpya ila nimeupata juzi tarehe 24. Mzigo ulifika tangu tarehe 16 December ila process za Bandari ni mwezi na zaidi. Ishi kulingana na kipato chako. Kama uwezo wako ni kula mlenda acha kutamani kuku choma.
 
Kazi iendelee samia kaleta waarabu naona bandari inafanya kazi kwa weredi sana.
 
Back
Top Bottom