Poleni sana jobless, ila na sisi ndugu zenu wa halmashauri hali ni mbaya

Poleni sana jobless, ila na sisi ndugu zenu wa halmashauri hali ni mbaya

Naelewa magumu wanayo pitia wanao tafuta ajira, kula yao tu MUNGU anasimamia.

ila kuna ndugu zenu wamepata ajira halmashauri nao kichwa kinapasuka kwa madeni, stress na uduchu wa mishahara.

Hela ya kujikimu tu haipatikani licha ya serikali kuu kulikemea swala hili kila mara lakini wapii.

Rais samia tukumbuke huku halmashauri maslahi yetu ni hafifu sana na hela za kujikimu hazipatikani
Naungana na wewe katika hili,huku Halmashauri tunapauka sana,hali ni mbaya sana.
 
Acha kabisa mzee, Ndio maana watu wakipata mwanya wa kupiga wanapiga kwelikweli.

Maisha ya Halmashauri changamoto sana.
Huku watumishi wengi nyuso zao zimepoteza nuru, zimepoteza furaha ,zinahuzunisha sana daah.
 
Hata wizarani uko ukiyasikia utaakaa kimya

Halmashauri uko uko kuna watu wapo km heaven wale Ellites

Niliwai kuona mfanyakazi wa TRA analalamika kichizi

Wakati ukisikia TRA unachowaza akilini pesa nje nje
 
Back
Top Bottom