Poleni sana jobless, ila na sisi ndugu zenu wa halmashauri hali ni mbaya

Mipango.
Pia issue sio idara, issue ni uko halmashauri ipi mkoa upi.
Kuna wakati nilikuwa Manispaa fulani kubwa kuliko Manispaa zote Tanzania, lakini maslahi yake hayakuti baadhi ya Halmashauri za wilaya nchini.

Mfano Manispaa ya Iringa huwezi linganisha na Halmashauri ya Mufindi au Njombe kwa maslahi.

Ni akili ya mtu na bahati tu
 
Oya nikimpata huyo tubadirishane aje huku Halmshauri.
Simaanishi kwamba ni mtu mmoja yaani wengi wao.

Mfano, Afisa Maendeleo wa Halmashauri ana muda mwingi wa kuingiza kipato cha ziada kuliko Afisa Maendeleo wa Mkoa.
 
Vipi kuhusu mafinga Kaka? Vipi pia maslahi ya architect halmashauri
 
Vipi kuhusu mafinga Kaka? Vipi pia maslahi ya architect halmashauri
Kwa upande wa wataalam sijajua; ila ubora wa halmashauri huwa ninaupima kwa mapato ambayo ndiyo hutoa picha halisi ya mzunguko wa fedha.

So bila shaka arcticture inaweza ikawa inalipa japo sijawahi kufika huko.

Mafinga ninadhani kuko poa. Ninavyofahamu, miji ya Njombe, Makambako na Mafinga haichani sana na ni miji inayokuwa kwa kasi kuliko hata Moshi na Songea.

Kwa hiyo eneo lile ni nzuri kwa mtu anayeona mbali.
 
Abadili aende huo uafisa usafiri bila kujiuliza mara mbili
 
Thanks for info
 
Pole sana dogo.
 
Iko hivi. Halmashauri waweka hazina ni wezi wezi wezi wezi wakishirikiana na maafisa mapato ni wezi wezi wezi, so makusanyo yanaibwa ila wakikaribia kufunga mwaka wanakusanya kufikia malengo. Yaani hakuna mfumo mbovu wa utoaji wa hela kama halmashauri yaani kuna rushwa, ngono, etc ili mradi tu mweka hazina aridhike. Dawa ni kufanya kila kitu kiwe online yaani pasiwe na maamuzi ya kulipa kulingana na mweka hazina anavyojisikia.
 
Utaongezaje experience wakati mtu hanayo? Ina maana utaweka uongo kwenye CV. Kama ni kunyoosha au format hizo zinapatikana online tena bure! Just google and you get CV foumarts free!
 
Hii inakuwaje hebu tia nyama
Yaani ukiwa mfano unadai hela fulani let’s say ni stahiki yako kabisa kisheria, mweka hazina anayo mamlaka ya kusema hela kwenye hicho kifungu haipo wakati kwenye bajeti ipo maana yake ujiongeze ugongwe ili upate hiyo hela, yaani kwa ufupi halmashauri zimejaa uchafu na wajinga wengi hasa idara ya fedha ni miungu watu na ndiyo wanaokwamisha hasa maendeleo
Maana wao ni kuiba kwenda mbele. Wakute hao idara ya fedha wapo kama wajinga ila wanahela kuzidi hao wa TRA, na hawajioneshi ila aseti walizonazo balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…