GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naam, na kwakua wananchi bado tumelala tukipata mitano ijayo, tutakua katika position nzuri zaidi. Hivi anavyoongea polepole hakuna jipya alilolisema, vingi ni vitu vilikua vinatajwa muda wote.

kinachotakiwa hapa ni wengi. washuhudie tu hii 2025 kwa umakini, kama 2020 ilianzisha safari hii 2025 itamaliza safari
 
Akili hii nayo ni matope. Unalinfanishaje malalamiko ya akina Slaa na Mrema na hiki alichosema Polepole? Wewe ulikuwa unajua m kwamba mfumo wa NIDA umeunganishwa na CCM?
 

Ninakazia:



Hawa watu ni wahaini!
 
Hapo umechemka ndugu. Umejionyesha kuwa hujui kitu kuhusu mifumo ila ndo unajifanya much know.

Tofautisha kudukua na mifumo kuunganishwa ni vitu tofauti.

Kudukua ni "fishing" au "sniffing" na kuunganisha mifumo ni "systems integration".

Kudukua ni uhalifu. System integration siyo uhalifu.

Walichofanya ccm na tume ya uchaguzi ni kuunganisha mfumo wa tume na wa CCM pamoja na NIDA kwa ajili ya kuchukua data kutoka mfumo wa CCM kurahisisha uchakachuaji kwa akili zaidi. CCM wanatumia akili kuiba kura kwa kushirikiana na tume.
 
Una hoja Sana ila wanavyojibu ndo maana tunaitwa nyumbu

Hata Mimi nimebaki kujiuliza how mfumo uibe wakati kura zinahesabiwa ndani ya chumba mbele ya mawakala
Najua CCM wanaibaga kura Ila labda uniambie kwavituo hewa,rushwa kwa mawakala n.k

Hili la inec na NIDA sijalielewa
 
Dah, wewe ni mtu mwenye subira sana.
Unataka mitano mingine chini ya Samia na Genge lake?

Hapa tulipo fikia imetosha mkuu, hiyo mitano mingine ya kushuhudia ni kuliumiza taifa hili bila ya sababu muhimu.

Samia na genge lake mwisho wao ni 2025; siyo 2030.
 
Ccm hamuwezi, kusafishika, kwa, dhambi zenu,hata kwa, damu, ya kristo!
Kama, bado upo kwenye denial kuhusu uovu wa ccm, inabidi wakuwaishe hospital ya vichaa milembe
 
Hahaha, duh kwahiyo hicho ndio kipimo cha akili??
 
Si huwa nawaambia msishiriki chaguzi zinazoendeshwa na kuratibiwa na tume ya uchaguzi iliyoundwa na CCM lakini huwa mnaniona hamnazo!

Hadi aseme Polepole ndo muamini kwamba mnajisumbua?

Where is your common sense?
Their common sense is at rest.
 
Pole pole ni kiboko aisee naona wakikaa watamuachia yule jamaa yao waliedhani kuwa ni hatari kwao hii inanikumbusha SA walimuua Stive Biko akatokeza John Mahlangu akawa hatari zaidi kuliko Biko nae wakamnyonga hapo Tswane ndio wakajitokeza watu wengi zaidi Mbeki,Mandela,Zuma,Sesulu na Mzee Oliver Tambo ambae yeye alikua anasafiri sana nje kusaka amani ya Nchi yake na ndio kisa cha uwanja wao wa ndege wakampa jina lake Oliver Tambo International Airport.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…