Uchaguzi 2020 Polepole: Kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni. CCM tunafanya kampeni za kisayansi

Uchaguzi 2020 Polepole: Kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni. CCM tunafanya kampeni za kisayansi

Slow Slow anaongelea viwanja vya ndege viivyojengwa lakini anazunguka zunguka tu anashindwa kuutaja uwanja wa Chato ......!!
 
Tanzania waandishi wa habari ni wawili au watatu.

Jenerali Ulimwengu.
Hamza Kassongo.
Dotto Bulendu.

Uandishi wa habari kwa sasa hauna tofauti na upolisi.
Zero na daraja la 4 la mwisho ndio wanakimbilia upolisi na uandishi wa habari.
Atakayepinga aweke ushahidi.

Yule wa 'kura 1' ameshajiengua?
 
We dogo tumia common sense. Lissu analeta upinzani gani kwa JPM? Kwa mkutano kama wa Bagamoyo jana unaweza kusema analeta challenge zozote.
Mkutano usio na fiesta, watoto wa shule Wala watumishi, bila kusomba na Malori na mabasi, bila kutoa hela na t-shirt bure

Mkutano ambao watu wanaalikana kwa wasap
 
Kwa kuwa hamtumii chopa basi ni figisu kwa wengine!
 
Polepole aache kusaka pointi za mezani, huyo Membe hajawahi kuwa mshindani wa kweli wa Magufuli. Mshindani wa kweli wa Magufuli ni Lisu. Kama Membe alishindana na Magufuli, basi ni wakati akiwa ccm sio nje ya hapo. Huyo Membe hata angekuwa anapiga kampeni usiku na mchana hana lolote jipya, hivyo asijifanye eti kakimbia kwa kuwaogopa ccm.
MGUFULI hana Mpinzani Yani Haka Ka Lissu kawe Kapinzani ka MAGUFULI kah Acheni Dharau
 
Hoja gani za msingi ambazo anazitoa huyu mgombea wa chama cha Mbowe? Inaingia akilini kuwaambia wananchi kuwa wasimchague JPM kisa atabadili katiba ili aongeze muda wa kukaa madarakani?

Ndio na hiyo ndio maana ya kampeni, lazima ujiuze ww na kutoa mapungufu ya mpinzani wako. Hoja ya Magufuli kuongezewa muda inaongelewa hadharani na hata bungeni. Kwenye kampeni ndio platform sahihi ya kuaddres hatari hiyo. Kama kuongezewa muda wa kukaa madarakani sio hoja ya msingi, mzee Mwinyi na mzee Pinda wasingetaka aongezewe muda, na huko bungeni lisingeongelewa zaidi ya mara moja, tena hadi kufikia kuzungumzwa na spika ndani ya bunge.
 
Barabara nijenge mimi halafu wapite humo huku wakinitukana!
 


Kampeni za CCM 2020 tunazifanya kisayansi, tumegawanya viongozi waandamizi wa chama kwenye maeneo tofauti. Msafara mkuu unaongozwa na Dkt. Magufuli, msafara mwingine wa Mhe. Samia Suluhu, na mwingine unaongozwa na Kassim Majaliwa, sisi hatutumii chopa." - Humphrey Polepole.

Mzee Jakaya Kikwete yupo Ukanda wa Kusini kule anavuruga, Mzee Pinda na Spika Job Ndugai nao wanaendelea. Muziki ni mzito mpaka sasa tunapozungumza kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni, tunafanya kampenzi za kisayansi." -Humphrey Polepole

Tangu Mhe. Magufuli aingie madarakani hakujawa na mfumuko wa bei, tumefanya kazi nzuri mno, bidhaa haiongezeki, Mhe. Magufuli amefuta kodi kwa wenye mishara midogo, hawa wanaosema ni wapotoshaji, tumelazimika kuwajibu, tunawaambia wasifanye siasa na hivyo." - Humphrey Polepole.

"Ukisema kushuka kwa Diplomasia ni uongo, Mhe Magufuli ameingia tu madarakani akapewa Uenyekiti wa EAC, ameendeleza mwendo wa kubana matumizi, miradi mikubwa imefanyika, ameacha alama, SADC amefanya mambo makubwa, MSD inapeleka dawa nchi zote za SADC." - Humphrey Polepole.

Tumefuatilia na kujiridhisha kwamba ni uongo mtupu, na TCAA imeshatoa ufafanuzi, lakini unajiuliza nini dhamira ya kusema uongo, kwamba mmezuiliwa kwenda kufanya kampeni maana yake unataka kupandikiza chuki, na hata hakukuwa na mpango wa safari"

NAOMBA NIMSAIDIE POLEPOLE JAMBO MOJA, KUHUSU MAGUFULI KUPEWA UENYEKITI WA SADC NI KUWA ILIKUWA NI ZAMU YA TANZANIA KWANI UENYEKITI WA SADC HUSHIKWA KWA MZUNGUKO WA NCHI WANACHAMA. HATA KAMA INGEKUWA KIBAJAJI NDIYE ANGEKUWA RAIS WA TANZANIA ANGEPEWA HUO ENYEKITI
 
Slow Slow anaongelea viwanja vya ndege viivyojengwa lakini anazunguka zunguka tu anashindwa kuutaja uwanja wa Chato ......!!
JANA TUMEAMBIWA NA MZEE MAKAMBA KUWA UWANJA WA NDEGE WA CHATO HAUJAJENGWA NA SERIKALI YA MAGUFULI BALI UMEJENGWA NA CCM.
 
Mkutano usio na fiesta, watoto wa shule Wala watumishi, bila kusomba na Malori na mabasi, bila kutoa hela na t-shirt bure

Mkutano ambao watu wanaalikana kwa wasap
Msiwe na hofu na kura za watumishi. Acha walazimishwe tu 'kuongeza idadi ya vichwa' Ila kwenye chumba cha kupigia kura hawatosindikizwa na greenguard.
 
Hivi kuna watu wanaweza kupoteza muda kumsikiliza Polepole?
Ndugai atafanya kampeni jimbo gani? Nani anamjua? kwa lipi? Wangekuwepo Mh. Sitta hapo sawa.
Sasa usipomsikiliza unawezaje kusema hafai?
 
Back
Top Bottom