Uchaguzi 2020 Polepole: Kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni. CCM tunafanya kampeni za kisayansi

Uchaguzi 2020 Polepole: Kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni. CCM tunafanya kampeni za kisayansi

ccm anaongea polepole,chadema kila kitu anaongea lissu ndio mana anafanya makosa ya kitoto anaonekana mbabaishaji
 
Nasubiria kusikia Lissu akitangazwa mshindi ama serikali ya mseto ama wakae meza moja ccm na upinzan kuyajenga kuna hoja mfumo kubadilika katiba mpya muhimu sana
 
Ni ujinga kuweka wagombea wa Urais katika kipindi hiki ambapo CCM inakubalika kila Kona ya nchi ukiwaondoa wezi wa mitihani na wanunuzi wa majina bandia pia waliokuwa wakiishi maisha ya ujanjaujanja na kitapeli

Hao siwazuu kumchukia Magufuli
 
Ccm mwaka huu mambo ni marahisi kabisa.
IMG-20200911-WA0020.jpg
 
Kiuhalisia kinachofanyika sasa na Ccm ni kutafuta ushindi wa kishindo.

Wananchi wengi walishaamua muda mrefu nani wa kumpa kura. 10% undecided ndiyo wanagombaniwa na vyama vyote

Lissu hawezi shinda Urais.
 
Chadema walishtukia mpango wa CCM wa kumtumia Membe kua mgombea pekee wa urais kupitia Upinzani ili baadae akimbie katikati ya kampeni kama alivyofanya sasa hivi.

Mwana CCM Membe aenda kupumzika Dubai baada ya kuifanyia kazi nzuri CCM.
 
Eti Polepole anadai anamzidi Lissu kuzungumza kingereza ..... Ooh my Gosh....!!
 
Jaribu kumtetea mwenyekiti wako kwa kujibu hoja za Lisu, tofauti na hapo. Hata mkutano wako huo hauna maana. Tunahitaji vita ya hoja na sio ujinga.

Maendeleo hayana chama. Miaka mitano jamaa hakuna airtime kwao, bado mpaka dakika hii hujui hata unachokiongelea!.

Ukweli humfanya mtu kuwa huru. Kama si kuchumia tumbo basi elimu yako ingekuwa msaada kwa taifa. #polepole bado tunatafakari
 
Ndio na hiyo ndio maana ya kampeni, lazima ujiuze ww na kutoa mapungufu ya mpinzani wako. Hoja ya Magufuli kuongezewa muda inaongelewa hadharani na hata bungeni. Kwenye kampeni ndio platform sahihi ya kuaddres hatari hiyo. Kama kuongezewa muda wa kukaa madarakani sio hoja ya msingi, mzee Mwinyi na mzee Pinda wasingetaka aongezewe muda, na huko bungeni lisingeongelewa zaidi ya mara moja, tena hadi kufikia kuzungumzwa na spika ndani ya bunge.
Sasa hili litampatia vipi kura? Mpaka wewe ushupae kuwa analeta challenge kwa JPM? Hujui kuwa wananchi wengi wanataka aongezewe muda ili akamilishe haya mazuri anayokufanyia wewe na watanzania kwa ujumla? Yeye ameshasema hataongeza na atafuata katiba ya JMT. Sasa huyu analeta uongo gani majukwaani.
 
Natamani niweke invoice toka MSD hapa muone uongo wa polepole.
Kuwatisha wapiga kura ndio kampani ya kisayansi?
 
JANA TUMEAMBIWA NA MZEE MAKAMBA KUWA UWANJA WA NDEGE WA CHATO HAUJAJENGWA NA SERIKALI YA MAGUFULI BALI UMEJENGWA NA CCM.
CCM wanahamisha magoli tu .......!!

Magufuli anadai achaguliwe ili tusirudi tulikotoka. Sijui kule tulikotoka anamaanisha kwa Mkoloni 1960!!

Kikwete anadai amani tuliyonayo ni kwa sababu ya sera za CCM ..... sijui hapo hazungumzii kule tulikotoka!!

Sasa huyu naye anazungumzia uwanja wa ndege wa Mzee kuwa umejengwa na CCM .... Anajikomba ili mtoto wake aonewe huruma!!
 
@
Tanzania waandishi wa habari ni wawili au watatu.

Jenerali Ulimwengu.
Hamza Kassongo.
Dotto Bulendu.

Uandishi wa habari kwa sasa hauna tofauti na upolisi.
Zero na daraja la 4 la mwisho ndio wanakimbilia upolisi na uandishi wa habari.
Atakayepinga aweke ushahidi.
Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom