Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole is just a mere loser. Wala taarifa zake siyo "breaking news kihivyo" maana anayoongea ni majungu ya mtu aliyepotezwa kwenye ramani.

Samia anachukua fomu kesho INEC na Oktoba TUNATIKI
Muache achukue hiyo fomu tujue ukweli. Je ni nani huyo aliyetajwa kama tax driver?? Je ni nani aliyekuwa akimtuma?? Je alikuwa akitumwa wapi?? Je ni kina nani na wana nguvu gani walio nyuma ya HP??
 
Nimemaliza kumsikiliza pole pole naona taifa linaandaliwa vema kisaikolojia kujisimamia mwaka huu.

Nukuu za Pole pole.

1/ Mama ukichukua form na kugombea Urais utakuwa umetutukana watanzania wote.

2/Mama unataka kugombea na Salum Mwalimu wa chauma, Mama unataka kugombea na Mpina wa Act. Kweli mama unataka kugombea na hawa na moyo wako una amani kabisa?

3/ Kwani Act sisi ccm hatuijuhi? Pole pole anatufumbua macho na kututhibitishia jambo hapa kuhusu Act.

4/ Pole Pole anashauri mama amuachie Mh Lissu bila masharti aende kwenye familia yake. Kisha aitishe muafaka wa kitaifa kabla ya kuingia kwenye uchaguzi. Amesema vyombo vya dola vitajipanga kutokana na maamuzi ya wananchi ambao ndio wenye nchi. Hapa maana yake tume isituambie muda umekwisha. Kila jambo linawezekana waamuzi wa mwisho ni wananchi sio ratiba za serikali na vyombo vyake.

5/ Kuhusu Hayati magufuli sizumgumzii chochote kila mmoja ameelewa code za Pole pole.

6/ Kuhusu Ndugai na kobe wa uvvccm kupandishwa juu ya mti ili kumtukana Ndugai na kumlazimisha ajiuzulu pia sisemi.Mtu yule kutoka kundi la mtandao anayeogopeka na kutisha. Aliyekwenda Dodoma kwa Ndugai na kumwambia jiuzulu na kisha mzee akasema.Nimekosa mimi...Nimekosa sana..Nisameewe huyo naye simzungumzii.Pole pole Amesema kundi hilo linatisha sana.

Hamphrey Pole pole you made my day.

Chadema wako sawa tukatae wahuni kwanza ndipo twende kwenye uchaguzi.This is our country.

Wale mnaodharau msimamo wa chadema muwe na adabu mmeelewa sasa nchi iko wapi.

Wale mnaosema wana chadema wanamezwa na hoja za pole pole muwe na adabu.Huyu jamaa ametujengea nguvu ya mapambano leo kiasi kwamba tunaona kabisa huu ndio mwaka wa mabadiliko.

Kataa wahuni ponyesha Tanzania.
 
Mkuu ukimsikiliza mange kimambi akitoboa mtumbwi huwa TZ inasimama, Ila polepole hapana kwa KWELI kama hatobadilika atanza KUKAA kikao peke yake. Fikiria kombora la mange kimambi KUHUSU ZILE bilioni zilizo PIGWA alafu muheshimiwa akajichanganya KWENYE kujibu YANI alikubali KUWA ni kweli zimepigwa na wasio wazalendo wametoa Siri, na karatasi zilionekana. Polepole ajifunze hilo bomu moja TU wanapoteana na ushahidi JUU. NAMBIE ushahidi WA kile kilicho somwa na dereva tax kikowapi? Mange alionesha



Kwishaaaaa
 
Kila jambo lina wakati na nafasi yake mkuu. Kwa akili yako unataka kusema kuwa kipindi hicho angeamka tu ghafla na kusema hayo aliyoyasema?

Nadhani utakua hufikirii vizuri.
NAMI NAKUTANDIKA SWALI MKUU KUONYESHA HUFIKIRII NJE YA BOX. JE SAMIA ASINGE CHUKUA FOMU UNAONA HUYU POLEPOLE ANGEONGEA CHOCHOTE? KAMA ANA NIA NJEMA NA TAIFA KWA NINI ASUBIRIE SAMIA KISA KUCHUKUA FOMU NDO AJITOKEZE JE SAMIA ASINGE CHUKUA FOMU? INA MAANA KUSINGE KUWA NA HAJA YA KUONGEA HAYO. JE HUO NDO UZALENDO?



Kwishaaaaaa
 
Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​
Polepole aendelee kumnyoosha huyu kikaragosi cha wahuni, OIL CHAFU ni lazima imwagwe sasa.
 
Bodaboda wanapewa mambo mengi mzazito bila wao kujua wala kustukiwa
Mimi nashangaa watu wanamuona jamaa kama anatunga .. hawajui hizo ni codes na Zaid nashangaa watu wanawadharau Hawa matex driver na boda,,Mimi kati ya watu naowaheshim nikienda mahali papya ni boda boda na teksi drivers ...na wazee wale wanaokaaga kucheza bao na kunywa kahawa muda wote ...imeshaniokoa nisipate ukimwi...nyie acheni bwana ..ujasusi una mambo mengi anatumiwa mtu yoyote ambaye wewe humdhanii kabisa ...
 
Acheni kupoteza muda na polepole ni project ya kitengo kuwatoa kwenye reli ishu ya NO REFORMS NO ELECTION
Si mpaka akili ya mtu iwe sharp ndo aelewe ulichoandika..
We kwa akili ya kawaida eti kulikuwa na list kwenye bahasha ya majina nalake likiwepo.
Halafu wakaweza kumuua Rais mwenye ulinzi mkali wakashindwa muua yeye mpaka leo yupo tu..
Na amefanikiwa kuwatoa watu kwenye reli wakishtuka uchaguzi huu hapa.
 
Back
Top Bottom