Polisi: Dereva wa Basi la SATCO alitishiwa na silaha bandia (Toyi), aliyetishia akamatwa

Namba bandia zinabandikwa kwa kuchomekwa na zipo wazi dah ila ... au basi tu.
 
POLISI HAMUAMINIKI KATU
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, kwani kufanya hivyo ni kuficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Cover ya spare tyre ina nembo hii




Huku nembo ya TPDF inafanana kidogo na ya landcruiser spare tyre




LINGANISHA NEMBO HIZO MBILI
 
Jambo ambalo huenda watu wengi hawalijui ni kwamba kila gari ya serikali ina namba za kiraia ambazo usajili wake unakoma haraka pindi linapopata nambari ya kiserikali lakini namba zile huhifafhiwa kwasababu dharura huweza kutokea ili zitumike.
Ila kama jamaa aliweka tu za kuchonga msala wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ila kama alitumia zile za awali si issue kubwa
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Sath John Masawa (31), baada ya kubainika kutumia bastola ya kuchezea (toyi) kumtishia dereva wa basi la abiria, huku akiwa ametumia namba za usajili za kughushi kwenye gari la Serikali.

Tukio hilo lilimhusisha dereva wa basi la Kampuni ya Satco lenye namba za usajili T 308 EME, Said Fadhil (54), linalofanya safari zake hapa nchini.

Akizungumza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo leo, Septemba 22, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, ameeleza kuwa uchunguzi wa kina wa Jeshi la Polisi ulibaini chombo alichokitumia mtuhumiwa huyo hakikuwa silaha halisi ya moto.

"Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kitu hicho hakikuwa bastola halisi kama ilivyodhaniwa awali, bali kilikuwa ni bastola ya kuchezea (toyi)," amebainisha Kamanda Hyera.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limebaini kuwa wakati wa tukio hilo, gari hilo la TARURA lilikuwa likitumia namba za usajili T 881 ENZ badala ya namba zake halisi za usajili wa Serikali ambazo ni STM 5806, huku namba hizo za bandia zikigundulika kuwa ni mali ya mtu mwingine.

Kufuatia kubainika kwa ukiukaji huo wa sheria, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kali kwa madereva na wamiliki wote wa vyombo vya moto nchini kujiepusha na matumizi ya namba za usajili zisizo halali.

#SasaLive #PolisiDodoma #TARURA #GallusHyera #SatcoBus UsalamaBarabarani Dodoma Tanzania
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, kwani kufanya hivyo ni kuficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Cover ya spare tyre ina nembo hii
Cover ya spare tyre ina nembo hii


View attachment 3675769

Huku nembo ya TPDF inafanana kidogo na ya landcruiser spare tyre

View attachment 3675776


LINGANISHA NEMBO HIZO MBILI

Nini jeshi la polisi na TPDF watu wake wa utambuzi intellejensia wanatufafanulia matumizi ya TARURA kutumia nembo inayofanana ya jeshi la ulinzi ?




 
Director amepuyanga..arudi kuandika script upya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…