Mimi kama Mtanzania naungana na wenzangu kumtakia afya njema T.L. kufuatia shambulio dhidi yake mijini Dodoma.
Leo tumeambiwa wazi na Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli, wakati akikabidhiwa ripoti za kamati mbili za kuchunguza madini ya Almas na Tanzanite kuwa, majadiliano kati ya Serikali na Barrick ni yanaendelea na ni magumu na kwamba Barrick walilazimika kuongeza timu ya pili kwa ajili ya majadiliano licha ya sisi kubakia na Wajumbe walewale.
Sasa, je mnadhani hao jamaa walikuja kwa ajili ya mazungumzo tu ama mikakati ya kumkatisha tamaa Rais ili achukiwe na wananchi wake? Mimi nina uhakika wa madhaka kuwa, Barrick na Acacia watakuwa na mkono wao dhidi ya jaribio la kumuua Tundu Lissu. Wanajua wakimuua Lissu, kila mtu atainyooshea kidole Serikali.
Tusijidanganye, Dola ina uwezo wa kumuua tena kwa urahisi sana bila kutumia njia zilizotumika. Hiyo njia wabaya wa Serikali walitaka kuipublicise kipindi cha Bunge. Serikali isingesubiri wakati wa Bunge never. Ninaamini Barrick na Acacia wana mkono wao.
Na kwa kuwa kuna tuhuma pia za Lissu kushirikiana nao inawezekana majamaa yamemtumia na yanataka kumgeuka. Kama ni kweli, basi Lissu bado ana hatari ya kuvamiwa tena ili kummmaliza ili asitoe siri wakati atakapopona (hapo hata akijua ni wao hawezi kutoa Siri kwa kuwa itammaliza mwenyewe kisiasa).