Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

On the way to Nairorbi
sema muhimbili
 
Utaipata tanzania polisi wanasubiri taarifa kwa wananchi na wananchi wanasubjiri taarifa kamili polisi..MHUDUMU ONGEZA KASI..
 
Ndugu zangu, nimejaribu kufuatilia yanayojili hususani jaribio la kutaka kumwua Mh. Tundu Lissu kama lilivyo-repotiwa na vyombo vya habari na response ya Jeshi la Police la Tanzania, division ya Dodoma...nilichojifunza ni kwamba hakuna jeshi la police bali kundi la wahuni waliovaa sare zinazofanana na za jeshi la Police....
Tunajua mapungufu ya Police na tunajua kuwa jaribio hili lina harufu ya kisiasa na huenda haki isitendeke, unless we join hands ili hawo waharifu wapatikane. ningependekeza yafuatayo...
  1. Tu-engage watu wa mitandao ya simu.nijuavyo mimi, mitandao ya simu hutumia satellite na hivyo ni rahisi kujua watu waliokuwa wanamfuatilia Lissu. kwa mfano, tukianzia Bungeni Dodoma wakati Lissu anaondoka, mpaka anafika nyumbani...kupitia network providers utaweza kuona namba za simu zilizokuwa karibu na eneo la Tukio...hivyo basi inaweza kuwa one of the leading step of investigation
  2. baada ya tukio, Gps ilionyesha hizo simu zikienda wapi....hapa namaanisha kuwa kutaonekana movement (pings)...
  3. watu gani walipigiwa simu kwa muda huo na hawo watu wako wapi? kwa ku-consider Radius ya eneo la tukio na ku-detect namba za simu itakuwa rahisi sana kuwapata hawo waharifu
  4. Namba zote zinazoonekana kwenye GPS, watu hawo watafute, wahojiwe na haki ichukue mkondo wake.
wandugu, mwenye mbinu zaidi za kiupepelezi atupie...
 
Mimi kama Mtanzania naungana na wenzangu kumtakia afya njema T.L. kufuatia shambulio dhidi yake mijini Dodoma.
Leo tumeambiwa wazi na Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli, wakati akikabidhiwa ripoti za kamati mbili za kuchunguza madini ya Almas na Tanzanite kuwa, majadiliano kati ya Serikali na Barrick ni yanaendelea na ni magumu na kwamba Barrick walilazimika kuongeza timu ya pili kwa ajili ya majadiliano licha ya sisi kubakia na Wajumbe walewale.
Sasa, je mnadhani hao jamaa walikuja kwa ajili ya mazungumzo tu ama mikakati ya kumkatisha tamaa Rais ili achukiwe na wananchi wake? Mimi nina uhakika wa madhaka kuwa, Barrick na Acacia watakuwa na mkono wao dhidi ya jaribio la kumuua Tundu Lissu. Wanajua wakimuua Lissu, kila mtu atainyooshea kidole Serikali.
Tusijidanganye, Dola ina uwezo wa kumuua tena kwa urahisi sana bila kutumia njia zilizotumika. Hiyo njia wabaya wa Serikali walitaka kuipublicise kipindi cha Bunge. Serikali isingesubiri wakati wa Bunge never. Ninaamini Barrick na Acacia wana mkono wao.
Na kwa kuwa kuna tuhuma pia za Lissu kushirikiana nao inawezekana majamaa yamemtumia na yanataka kumgeuka. Kama ni kweli, basi Lissu bado ana hatari ya kuvamiwa tena ili kummmaliza ili asitoe siri wakati atakapopona (hapo hata akijua ni wao hawezi kutoa Siri kwa kuwa itammaliza mwenyewe kisiasa).
Si wanataka mwenye taarifa, ebu kawambie polisi hilo basi tuone.
 
Back
Top Bottom