[HASHTAG]#ButWhatDoIKnow[/HASHTAG]
1. Nyumba ya Tundu Lissu pale area D ipo pembeni, karibu sana na nyumba ya Naibu Spika wa bunge.., Je, hawa watu waliweza vipi kufunguliwa geti kuingia na kutoka ASAP baada ya tukio?
2. Walinzi wa Nyumba ya Naibu Spika wa bunge, Je, hawakusikia milio ya risasi zaidi ya 32 na hata kuimarisha ulinzi mara moja? Ikawa vipi watu hawa wakapita getini tena baada ya shambulizi!?
3. Labda Tundu Lissu aliamini usalama wake ni kwenda area D (sensitive restricted area), Je, hawa watu (wahalifu) walionesha vitambulisho hadi kufunguliwa lango wakati wa kutoka—kuingia?
4. Gari iliyozibwa namba za usajili (plate number), inaruhusiwa vipi kupita kwenye lango lenye ulinzi wa polisi kwenda kwa
Naibu Spika wa bunge? ningependa kufahamu walieleza nini hadi kuruhusiwa kuingia ndani ya lane..
5. Tundu Lissu (labda) alifikiri sehemu salama ni kwenda eneo hilo (area D), ghafla kutahamaki, Nissan Patrol imeruhusiwa kupita Langoni kama kawaida, waliruhusiwa vipi watu wale?
6. Tundu Lissu asingeweza kushuka kwenye gari lake baada ya Nissan Patrol kuegesha pembeni yake (upande wake), tena kwa kuruhusiwa kupita Langoni., baada ya tukio, hawa watu waliondoka vipi hata baada ya milio ya risasi?
7. Je, wahalifu hao walikuwa na bunduki zenye viambata vya kuzuia sauti za risasi 'silencer' hata walinzi wasiweze kusikia mirindimo ya risasi zaidi ya 38, najaribu kujiuliza bila kupata majibu.
8. Kwa umakini wa Tundu Lissu, nataka kujaribu kuamini kwamba atakuwa lazima aliwasiliana na watu kadhaa (wa karibu) kutoa taarifa kuhusu kufuatiliwa na gari hilo, Nissan Patrol kutoka bungeni..
Anyways.., nilikuwa najaribu kujiuliza Maswali bila majibu, Tundu Lissu and his burden driver, survived the fraught skirmish (death—match) to tell tale, atatueleza ukweli wote kiumbe huyu... Let's Wait!
————————————
[emoji767]..., MMM
Sent using
Jamii Forums mobile app