September 21, mwaka 1972, Jaji Mkuu wa Uganda kipindi cha utawala wa dikteta Idi Amin, alitekwa ndani ya vyumba vya mahakama kuu ya Uganda na kupotea kwa siku 4 hadi pale serikali ya Uganda ilipoanza yenyewe kusambaza taarifa za uongo kuwa mwili wa Dr.Kiwanuka ulikuwa umeonekana ukielea juu ya mto Nile, na serikali ilijitia kuagiza kuwa wauaji/watekaji wa Dr.Kiwanuka wangetafutwa popote walipo na kukabiliana na hatua za kisheria.
Lakini ukweli ni kuwa Idi Amin mwenyewe kwa mkono wake mwenyewe alikuwa amemwua Dr Kiwanuka baada ya Jaji huyo kuwa amechukizwa na kukosa utawala wa Amin kwa kukiuka wazi wazi utawala wa sheria.
Ajabu baada ya mauaji, Idi Amin alihifadhi mwili wake katika mafriji ya Ikulu ya nchi hiyo na akawa akipita hospitali moja baada ya nyengine eti akitafuta mwili wa Dr Kiwanuka. Pia alikuwa akitema mkwara mzito kwamba yeyote ambaye angekamatwa kwa mauaji ya Dr Kiwanuka angekiona cha mtema kuni...
Watawala wa Kiafrika wana mambo sana duh!