Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Kwakuwa Jeshi la Polisi limealika uwasilishwaji wa taarifa kuhusu kushambuliwa kwa risasi kwa Lissu,mimi VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa naanza safari ya kuzisaka taarifa. Natoka hapa Kibiti,Pwani kwenda Dodoma.

Risasi 32 si jambo la kawaida. Kwa uzoefu,historia na fani yangu naamini nitapata la kulipata na kuliwasilisha polisi. Nakwenda Dodoma kwa kazi maalum. Ikinipasa,nitakwenda Singida,Dar na kwingineko. Naanza na Dodoma

Wasiojulikana watajulikana tu. Tuwe na subira. Mpunga hufukiwa lakini wakati muafaka unapofika huchomoza. Hakuna siri ya milele

Smg ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
Yule mganga wa Kenya akitumika, waliopiga risasi watajipele wenyewe.
 
Kugeuza tukio baya na Unyama aliofanyiwa Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa MTAJI WA KISIASA ni mtindio wa Akili na Upuuzi unaopaswa kupingwa na kila anayejitambua.

Lissu sio Chadema tu Lissu ni Mtanzania na kila mtanzania atakayeonewa na kufanyiwa dhulma awe mwanasiasa asiwe mwanasiasa wote wanastahili huruma yetu na sauti zetu kuwalilia , na kuwapigania katika uzito sawa.

Lissu anatetea maslahi ya Tanzania yote kwa Ujumla hivyo ni haki ya kila mtanzania kumlilia na kumuombea. Kuleta chuki zenu au tofauti zenu za Vyama kipindi ambacho taifa limeungana kumlipa fadhila mtu aliyejitolea muda na maisha yake kulipigania ni Ujinga na Upumbavu unaokera sana.

Tukio la Lissu linapaswa kuchukuliwa kama chachu ya mapambano dhidi ya Waovu na Madhalimu wa haki za Binadamu na utu kokote kule walikojificha.

Unyama huu haukuanza na LISSU wengi tumewazika waliuawa kwa dhulma na kwa kuonewa tu bila kosa lolote.

Watu wengi ndani ya taifa hili wamepotea, wameuawa, wametekwa, wamefungwa Jela kwa dhuluma na Uonevu, na wengine maiti zao zimeokotwa kando kando ya mito, maziwa nk baadhi yenu hamkutaka kabisa kuongea na mliona hayawahusu.

Tulichukulie tukio hili kama kengere ya kuamsha mapambano dhidi ya Wahuni waliogeuza Taifa hili kuwa ni sehemu ambayo ukifumbua mdomo kuisemea haki unatafunwa. Tupambane na Wahuni wawe katika kichaka chochote walikojificha tukichome moto watoke angalau nasisi tuwe tunajiamini katika taifa letu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari njema kiongozi wasiojulikana wanaweza kuwa ni wale wanaojulikana
 
Kwakuwa Jeshi la Polisi limealika uwasilishwaji wa taarifa kuhusu kushambuliwa kwa risasi kwa Lissu,mimi VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa naanza safari ya kuzisaka taarifa. Natoka hapa Kibiti,Pwani kwenda Dodoma.

Risasi 32 si jambo la kawaida. Kwa uzoefu,historia na fani yangu naamini nitapata la kulipata na kuliwasilisha polisi. Nakwenda Dodoma kwa kazi maalum. Ikinipasa,nitakwenda Singida,Dar na kwingineko. Naanza na Dodoma

Wasiojulikana watajulikana tu. Tuwe na subira. Mpunga hufukiwa lakini wakati muafaka unapofika huchomoza. Hakuna siri ya milele

Smg ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)

Kwa kawaida ni RAHISI sana kumondoa panya kwenye nyumba kama hana mazalia,akiwa na mazalia basi utatumia nguvu kubwa kumuondoa panya huyo na familia yake.

Maana mwisho wa siku Familia ya panya itakuwa na wajukuu,watukuu na vitukuu.Kazi mnayo,Kinyago mlichotuchongea watanzania kiondoeni
 
WATU WASIOJULIKANA.

Nimekaa nikijifikiria juu watu hawa ambao tumekuwa tukiwaita ama wakijiita "watu wasiojulikana"

Inasikitisha kuona kwamba pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia lakini bado tumeendelea kuandamwa na kuumizwa na watu hawa "wasiojulikana"

Hawa watu wasiojulikana wamefanya matukio mengi, wameua ,kujeruhi na kufanya uharibifu mkubwa lakini cha kusikitisha ni kwamba jeshi na serikali kiujumla limeshindwa kuwachukulia hatua kwa kisingizio kwamba ni "watu wasiojulikana"

Watu wasiojulikana umekuwa ni msamiati unaopendwa sana na jeshi letu la Polisi lakini tujiulize hao watu hawajulikani kwa nini?, watajulikana lini? Pamoja na jeshi kuwa na vifaa mbalimbali vyenye kuliwezesha kuwabaini wahalifu mbali mbali lakini linegonga mwamba kwa watu hawa wasiojulikana.

Mpaka Leo hii hatujui alipo kada wa CDM Beni saanane kisa alitekwa na watu wasiojulikana.
Ofisi za IMMA zililipuliwa na watu wasiojulikana, miili ya watu imekuwa ikiopolewa mara kadhaa baharini ikiwa kwenye viroba , Msanii Roma mkatoliki alitekwa na kuteswa na watu wasiojulikana,

Leo hii mh. Tundu Lissu amepigwa risasi na hao hao ambao polisi huwaita watu wasiojulikana.Ikumbukwe mh Lissu ameshawahi kulalamika kufuatiliwa na vijana wanaokuwa kwenye gari ambalo hadi plate number alizitaja ,, je Leo hii anapigwa risasi mnasemaje no watu wasiojulikana?

Kwa nini hawa watu wasiojulikana wamekuwa wakiwaandama wakosoaji wa serikali na si watu wengine ? Aliyemnyooshea bastola mh.Nape Nnauye amefanywa nini au hajulikani ilihali tukio alilifanya hadharani?
Kwa nini watu hawa wasiojulikana wamekazana sana awamu hii ya uongoz na sio hapo kabla? Imefikia mahali nchi ina watu wengi wasiojulikana kuliko wanaojulikana. So sad.

Kwa kumalizia tu niseme kwamba hao wanaojiita wasiojulikana pamoja na washirika wao watambue kwamba nothing last forever na mwisho was ubaya ni aibu. Vilio na majonzi ya wapenda amani nchi nzima havitaenda Bure
 
Hawa polisi wetu huwa wanabadilika na kuwa hao wasiojulikana...nashangaa hizi movie zinavyoenda,
Baada ya office za Immma kulipuliwa mashahidi walisema waliofanya hilo tukio walionekana kuvalia sare za polisi kaki...lkn badae tukaambiwa watu wasiojulikana...
Lissu alishasema vijana Wa Sirro na Tissss wanamfatilia na Toyota Premio kila kona aendako,na Sirro+Tissss hawajakanusha hilo swala...
So finally ktk conclusion ni kwamba,Watu wasiojulikana ni hawa hawa polisi wetu na tixxx wetu waliopo ktk jamii yetu
 
Nina uzoefu wa miaka 7 katika uchunguzi. na niko partners na Wakenya.... tupeni hiyo kazi within three weeks tunatoa majibu complete
 
Kweli Mkuu,,cha msingi tumuombee dua Mungu amjaalie Afya,
Mm na imani na serikali yetu hii na jeshi la polisi
Tena kutokana na Mh Rais wetu alivotoa agizo kali kwa vyombo vya sheria kuhus kukamatwa kwa hao waliofanya tendo hilo la kinyama,,Na imani watadakwa tu.iwe isiwe
Mungu amjaalie Mh Lissu na Ampe Afya njema
"Ameen"
 
Nina uzoefu wa miaka 7 katika uchunguzi. na niko partners na Wakenya.... tupeni hiyo kazi within three weeks tunatoa majibu complete
safi sana.. Haya Chadema kuna sehemu ya kuanzia.. mpeni kijana kazi
 
safi sana.. Haya Chadema kuna sehemu ya kuanzia.. mpeni kijana kazi

Unadhani hizo kazi mtu anapewa kama keki.....

Wewe umemuamini kwa kuwa kaaandika mtandaoni na FAKE ID......,!!??

What if na yeye ni mwanausalama wa tiss...!!?

Acha mihemko
 
Unadhani hizo kazi mtu anapewa kama keki.....

Wewe umemuamini kwa kuwa kaaandika mtandaoni na FAKE ID......,!!??

What if na yeye ni mwanausalama wa tiss...!!?

Acha mihemko
Siko kama unavyofikiri... tena kwa sasa niko Kenya kwa kazi a namna hiyo....... nimefanya kazi sa investigation kwa muda sasa.....
 
Msipoteze muda kusubiri jeshi la police lifanye uchunguzi..
uko wapi uchunguzi wa Roma alivyotekwa.. Ben Saanane.. Mawazo alivyouawa.. Nape kutolewa Bastola.. Ofisi za Imma Advocate kurushiwa bomu.. wako wapi uchunguzi wa kuvamia Clouds kwa mitutu ya binduki.. uko wapi uchanguzi wa kuvamiwa kwa mikutano ya CUF na waandishi wa habari.. wako wapi walioshtakiwa kumuua dr Mvungi?
Chadema stuka.. tunachanga pesa kwa ajili ya matibabu ya Lissu na vile vile kwa ajili ya private investigator
Hivi hatuna spy drone camera air raiders
 
Back
Top Bottom