Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Hawa polisi wetu huwa wanabadilika na kuwa hao wasiojulikana...nashangaa hizi movie zinavyoenda,
Baada ya office za Immma kulipuliwa mashahidi walisema waliofanya hilo tukio walionekana kuvalia sare za polisi kaki...lkn badae tukaambiwa watu wasiojulikana...
Lissu alishasema vijana Wa Sirro na Tissss wanamfatilia na Toyota Premio kila kona aendako,na Sirro+Tissss hawajakanusha hilo swala...
So finally ktk conclusion ni kwamba,Watu wasiojulikana ni hawa hawa polisi wetu na tixxx wetu waliopo ktk jamii yetu
Nape..watu wasiojulikana..
Kibiti....wasiojulikana
IMMA...WASIOJULIKANA
BEN SA8...WASIOJULIKANA
ROMA....WASIOJULIKANA
LISU...WASIOJULIKANA
MAITI MTO RUVU...WASIOJULIKANA
MAITI KUNDUCHI..WASIOJULIKANA

NIMECHOKA...NI HERI KUWA KICHAA UKAE MAJALALANI KULIKO KUWA NAAKILI TIMAMU HUKU UKIONA JINSI AMANI INAVYO CHEZEWA NA HAWA WATU.......WASIOJULIKANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wenye madaraka wanajiona wamepewa na mungu, basi wajue shetani ndiye anawasimamia kucha. Yeye hushindwa kwa hila na ufidhuli wake. Lisu anasimamiwa na Mungu na sio makinikia
 
There were multiple shooters
The numbers of bullets (25) has got the hidden message for those with active brain
The truth is that the multiple shooting was just a camouflage

Lets pray for Our beloved hero.
 
Mungu akuhurumie sio akili yako.............. Nimeomba rehema kwa ajili yako
Mungu awahurumie pia wale wote wasiojielewa na wenye ubinafsi uliopitiliza....asiwasahau wale wote wenye akili na nia mbaya ya kuliingiza taifa kwenye matatizo kwa sababu zao binafsi na kutumia udhaifu wa watanzania.... hawa ni pamoja na wale wote;
1) Wanaopenda kujipendekeza kwa MATAIFA na International community waiwekee VIKWAZO vya UCHUMI na wakate MISAADA yote kwa NCHI yetu.
2)Wale wote waliohusika na Kuyashawishi na kushirikiana na Makampuni ya Kibeberu kuzuia Mali za serikali zilizolipiwa
3)Wale wote ambao toka October 2015; Wamekuwa wanahamasisha uvunjivu wa amani kwa makusudi ikiwemo kuanzisha UKUTU.
4)Wale wote waliokuwa wanashabikia Mauaji ya POLISI na Viongozi huko Kibiti, Mkuranga, Mkiu na Ikwiriri.
 
Na wewe umeanzisha uzi tena lugha mubashara ya malkia
 
There were multiple shooters
The numbers of bullets (25) has got the hidden message for those with active brain
The truth is that the multiple shooting was just a camouflage

Lets pray for Our beloved hero.
funguka zaidi mkuu
 
Kugeuza tukio baya na Unyama aliofanyiwa Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa MTAJI WA KISIASA ni mtindio wa Akili na Upuuzi unaopaswa kupingwa na kila anayejitambua.

Lissu sio Chadema tu Lissu ni Mtanzania na kila mtanzania atakayeonewa na kufanyiwa dhulma awe mwanasiasa asiwe mwanasiasa wote wanastahili huruma yetu na sauti zetu kuwalilia , na kuwapigania katika uzito sawa.

Lissu anatetea maslahi ya Tanzania yote kwa Ujumla hivyo ni haki ya kila mtanzania kumlilia na kumuombea. Kuleta chuki zenu au tofauti zenu za Vyama kipindi ambacho taifa limeungana kumlipa fadhila mtu aliyejitolea muda na maisha yake kulipigania ni Ujinga na Upumbavu unaokera sana.

Tukio la Lissu linapaswa kuchukuliwa kama chachu ya mapambano dhidi ya Waovu na Madhalimu wa haki za Binadamu na utu kokote kule walikojificha.

Unyama huu haukuanza na LISSU wengi tumewazika waliuawa kwa dhulma na kwa kuonewa tu bila kosa lolote.

Watu wengi ndani ya taifa hili wamepotea, wameuawa, wametekwa, wamefungwa Jela kwa dhuluma na Uonevu, na wengine maiti zao zimeokotwa kando kando ya mito, maziwa nk baadhi yenu hamkutaka kabisa kuongea na mliona hayawahusu.

Tulichukulie tukio hili kama kengere ya kuamsha mapambano dhidi ya Wahuni waliogeuza Taifa hili kuwa ni sehemu ambayo ukifumbua mdomo kuisemea haki unatafunwa. Tupambane na Wahuni wawe katika kichaka chochote walikojificha tukichome moto watoke angalau nasisi tuwe tunajiamini katika taifa letu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaani siyo siri nilipatwa na uchungu sana jana na usiku wa leo. Nilijiuliza mambo mengi mengi sana lakini nikawa sipati majibu. Na kilichokuwa kina nisumbua mpaka sasa ni kwamba serikali ilikuwa Dodoma kwenye kikao cha bunge, halafu bungeni kuna ulinzi wa kutosha, hiyo bunduki iliyotumika haikutoa mlio? Au ilikuwa kama mshale? Milio ya bunduki inafahamika ni aina gani na maaskari wanajua.

Swali: Iweje mtu aingie eneo hilo la bunge na kufetua risasi kama mvua asikamatwe? Huyo mtu alijiamini vipi? Au wabunge wetu hawana ulinzi? Hao watu wanaojitetea nao waliingia je eneo la bunge wakati magari yanakaguliwa? Bado kichwa kinapata moto.
 
Yaani siyo siri nilipatwa na uchungu sana jana na usiku wa leo. Nilijiuliza mambo mengi mengi sana lakini nikawa sipati majibu. Na kilichokuwa kina nisumbua mpaka sasa ni kwamba serikali ilikuwa Dodoma kwenye kikao cha bunge, halafu bungeni kuna ulinzi wa kutosha, hiyo bunduki iliyotumika haikutoa mlio? Au ilikuwa kama mshale? Milio ya bunduki inafahamika ni aina gani na maaskari wanajua.

Swali: Iweje mtu aingie eneo hilo la bunge na kufetua risasi kama mvua asikamatwe? Huyo mtu alijiamini vipi? Au wabunge wetu hawana ulinzi? Hao watu wanaojitetea nao waliingia je eneo la bunge wakati magari yanakaguliwa? Bado kichwa kinapata moto.
Haikuwa eneo la Bunge ilikuwa ni Nyumbani kwa Mh. Lissu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Worst move by magu, ccm itachukiwa mara elfu moja zaidi ya sasa.
 
WANAOUZA SURA TBC NDO WATU WASIO JULIKANA

VNGOZI WANYAMA IN WAY HATUWAJUI WETHER NI AKINA JOHN AU POMBE TU
 
Polisi ya bongo bwana...

Ingelikuwa ni wenzetu kwa kutumia vidhibiti vidogo vidogo tu kama ukubwa wa matundu ya risasi, maganda ya risasi n.k

Sasa hivi tungekuwa tushajua angalau silaha ilinunuliwa au ilosajiliwa kwa nani, mpigaji au wapigaji wanatumia mikono gani n.k...

Lakini sasa bongo kama kawaida yao upelelezi unategemea umbea umbea tu...

Hahahaha........Mkuu umenikumbusha mbali! Mbona watumishi wengi wa umma huendaga nje ya nchi kuongeza maarifa kwenye taaluma yao lakini hakuna maarifa mapya wanayokujaga nayo! Tatizo ni nini? Ni hawaelewagi kitu wanapoendaga short courses? Wamezoea business as asual? wale wenye taaluma nzuri hawapewi nafasi za kuchunguza matukio ya msingi kama haya? Wataalam hawajiamini kiasi kwamba wanapelekeshwa na wanasiasa au mabosi ambao wanatumika kisiasa?
 
HABARI MPYA: Kamanda wa Polisi Dodoma amesema yeyote mwenye taarifa kuhusu wahusika waliompiga risasi Tundu Lissu waiwasilishe polisi.

Kwa sasa wamepata taarifa kuwa gari iliyoonekana ni gari nyeupe aina ya Nissan.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema polisi wameshaanza kufanya upelelezi kuhusu wahusika na kusema watu waendelee kusubiri taarifa kutoka kwenye jeshi hilo

Amesema hawatapenda kuona mikusanyiko sehemu yoyote ya Dodoma mjini kwa sababu jeshi la polisi bado linafuatilia asili ya tukio lenyewe na mikusanyiko ya watu inaweza kutumika vibaya.
Pia wataendelea kuwafaamisha raia kwenye kila hatua watakayofikia



adc7684e7b5f47745028ccb004d3f1db.jpg


[HASHTAG]#Mwananchileo[/HASHTAG]

Sasa kazi Yao ni nini? Kama hawana taarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom