Kugeuza tukio baya na Unyama aliofanyiwa Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa MTAJI WA KISIASA ni mtindio wa Akili na Upuuzi unaopaswa kupingwa na kila anayejitambua.
Lissu sio Chadema tu Lissu ni Mtanzania na kila mtanzania atakayeonewa na kufanyiwa dhulma awe mwanasiasa asiwe mwanasiasa wote wanastahili huruma yetu na sauti zetu kuwalilia , na kuwapigania katika uzito sawa.
Lissu anatetea maslahi ya Tanzania yote kwa Ujumla hivyo ni haki ya kila mtanzania kumlilia na kumuombea. Kuleta chuki zenu au tofauti zenu za Vyama kipindi ambacho taifa limeungana kumlipa fadhila mtu aliyejitolea muda na maisha yake kulipigania ni Ujinga na Upumbavu unaokera sana.
Tukio la Lissu linapaswa kuchukuliwa kama chachu ya mapambano dhidi ya Waovu na Madhalimu wa haki za Binadamu na utu kokote kule walikojificha.
Unyama huu haukuanza na LISSU wengi tumewazika waliuawa kwa dhulma na kwa kuonewa tu bila kosa lolote.
Watu wengi ndani ya taifa hili wamepotea, wameuawa, wametekwa, wamefungwa Jela kwa dhuluma na Uonevu, na wengine maiti zao zimeokotwa kando kando ya mito, maziwa nk baadhi yenu hamkutaka kabisa kuongea na mliona hayawahusu.
Tulichukulie tukio hili kama kengere ya kuamsha mapambano dhidi ya Wahuni waliogeuza Taifa hili kuwa ni sehemu ambayo ukifumbua mdomo kuisemea haki unatafunwa. Tupambane na Wahuni wawe katika kichaka chochote walikojificha tukichome moto watoke angalau nasisi tuwe tunajiamini katika taifa letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Sent using
Jamii Forums mobile app