Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Katika sakata hili la shambulio la Lissu wengi wanaamini kuwa limefanywa na watu wa serikali, hasa kutokana na uhusiano aliokuwa nao Lissu dhidi ya serikali.
Hali imepelekea kuongezeka kwa chuki dhidi ya serikali, na hata uchunguzi na upelelezi unaofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi ukija na majibu gani bado watu wataendelea kuamini kuwa kuna mkono wa watawala kwenye sakata hili.

Hivyo basi kuondoa dhana hii na kwa vile tayari serikali inatuhumiwa na mtuhumiwa hawezi kujichunguza na kujipeleleza, vyombo vyote vya serikali linavyofanya uchunguzi kuhusu jambo hili vijitoe na baadala yake kwa gharama ya serikali kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) watafutwe wataalamu kutoka nje kwa ajili kufanya uchunguzi wa sakata hili.au uindwe kamati huru yenye wataalamu kutokana makundi mbalimbali kwa ajili ya kuchunguza sakata hili lenye lengo la kututumbukiza kwenye machafuko na umwagaji damu.

Kwa kufanya hivyo serikali kama haihusiki itakuwa imejisafisha na kurudisha imani kwa wananchi kuwa haijahusika na jaribio la kutaka kumuua Tundu Lissu.
 
Utapimwa mkojo, nani kasema serikali inatuhumiwa? achana na kitu hicho ndugu
 
Acha bangi wewe....tukio Hilo Ni jinai iliyofanyika katika Ardhi ya Tanzania Na Jeshi la Polisi Lina mamlaka kamili ya kuchunguza. Why do you chadema want to make a mountain out of a hill?
 
Kazi kubwa ya polisi ni upelelezi. Ni bahati mbaya muda huo kwa sasa hawana. Ni wakati mwafaka wa kuwa na wapelelezi binafsi, ambayo pia ni njia ya kuongeza ajira kwa vijana wetu.
 
Kwenu Police..
Napenda kutoa angalizo,mazingira rafiki yanazidi kupotea,Wananchi imani yao inazidi kupotea,matukio makubwa kama hili liliomkuta Mh Tundu Lissu,linaleta watu pamoja na kuwaangalia nyie walinzi wetu kama wakombozi.
Tukio hili sio kama matukio mengine,tukio hili linaweka tofauti zetu pembeni nakutuleta pamoja,jitihada zenu zisipo onekana kwenye hili,imani yetu kwenu itazidi kupungua,mtaongeza chuki,mazingira yenu yakazi yatakuwa magumu,tunajua mlipishana baadhi ya mambo na Lissu lakini tuhakikishieni justice inapatikana kwa walifanya hili,
[HASHTAG]#justiceforlissu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#letsprayforlissu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#godsavelissu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#tanzaniawithlissu[/HASHTAG]
 
Nimekuwa nikifuatilia kauli zilizotolewa na Kamanda Sirro juu ya tukio la jana la Tundu Lissu kujeruhiwa risasi. Kamanda Sirro amewahakkikishia wananchi kuwa wahalifu watapatikana endapo tu wananchi watatoa ushirikiano. Kauli hii imenipa wasiwasi mkubwa kwa vile mafanikio anayowahakikishia wananchi juu ya kukamata wahalifu kumbe ni kwa kutegemea kuwa apewe taarifa na wananchi. Kwa maneno mengine, Jeshi lake halina namna yeyote ya kufanya na kufanikisha endapo wananchi hawatatoa taarifa. Napata shaka na uwezo wa Jeshi kama sio kauli ya kinafiki hii. Pamoja na hayo nimewaza matukio ya nyuma yanayofanana na hili na kipi Jeshi limefanikiwa naona hakuna kitu. Swala la Ben Saanane walisema wanashughulikia, hamna kitu. Maiti za mto Ruvu wakasema hivyo hivyo, hamna kitu. Maiti za 15 zilizookotwa katika viroba wanasema hivyo hivyo, hamna kitu. Ofisi za mawakili wa IMMMA wakasema wanafuatilia, hakuna kitu! Sasa na hili la Lissu ndio lishawekewa kingingi cha kutegemea taarifa za wasamaria wema. Nalo litapita hakuna kitu. Kwa kifupi watanzania Jeshi hatuna. Sioni kwa nini liliamini Jeshi hili wakati huu katika jambo hili wakati wameshashindwa kabla hawajaanza. Jeshi letu haliaminiki.
 
Wasaalam wadau!
Kwanza nachukua fursa hii kulaani hawa mabedui,maharamia,mashetani wenye sura Za kibinadamu na wapumbavu wenye degree za juu za upumbavu,waliojaribu kumua Tindu Lusu lakini kwasababu ni wapumbavu hata wameshindwa kufikia malengo.

Ndungu zangu kutokana na kuumizwa na hili swala na Sina imani Kama hawa watu watawekwe nguvuni,bora twendeni Mombasa tukawaloge wakamatwe na yule nyoka aliyewakamata wale wahizi walio iba gari Kenya!..
 
Tukio la kusikitisha sana nchini kwetu Kupigwa Risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki (Tundu A Lissu) ndani ya eneo la Makazi yake ambalo ni makazi ya wabunge spika na wanaofanya kazi Dodoma.

Tukio hili na tukio la Nape kutolewa bastola hadharani, Roma Mkatoliki kutekwa, Ben Saanane kupotea ni kati ya matukio mengi ambayo yametokea nchini yasiyo na majibu.

Matukio haya yana sura za kisiasa - sio ujambazi - ni siasa .

Demokrasia inaendana na uvumilivu - Tukiachia Taifa lijengwe na watu wasio na uwezo kuhoji kisa wanaogopa wakihoji maswali magumu watapotezwa, pigwa risasi tutaangamia wote.

Hakuna ubaya Taifa kuwa na watu wadadisi - Kila darasa huwa linakuwa na wanafunzi waliozidi wenzao akili na mara nyingi waalimu huwaona wasumbufu kwani kuna wakati mwanafunzi anamzidi mwalimu kuelewa - ila mwalimu makini anatumia wanafunzi wenye uelewa wa kasi kusaidia wengine na yeye mwenyewe.

Kosa la Lissu ni uwezo wake wa akili na udadis,Kosa la Nape lilikuwa ni uthubutu wake - Kosa la Roma ni akili zake nyingi kwenye utunzi wa nyimbo zake - Kosa la Saanane ni akili yake ya udadisi na wengine wengi sana.

Badala ya kuogopa watu wenye uwezo mkubwa washirikishe wapewe majukumu makubwa waweze kutumia akili na udadisi wao.

Yanayotokea kwa sasa nchini ni kuwadharau wenye uwezo na kuwakumbatia vilaza- sasa tunapata watekaje, wapiga risasi na wauaji.

Ni akili za ajabu kufikiri kuna uwezekano wa kutisha watu milioni 50 kwa kuwateka, kupiga, kuwauwa au kuwafanya lolote baya.

Binadamu ameumbwa kuzoea mazingira yawe ya amani au vita, mateso au amani, raha au karaha- unapomlazimisha binadamu aone maisha yake ni yahatari wanageuka kuwa wanyama.

Huu sio muda wa kushabikia - Tanzania ni nchi yetu wote - vitendo vya kinyama haviwajahi kumwacha mtu, utawala, kikundi, jamii salama.

Tunataka majibu kutoka serikali hawa wauji ni akina nani- minong'ono imekuwa mingi na ni hatari sana kwa amani ya nchi - wananchi wasiachwe wakajitafutia mbaya wao au wabaya wao itakuwa dark war.

Tume ya Kijaji huru iundwe kuchunguza haya matukio - Haiwezekani mtu apigwe Risasi saa saba mchana halafu zitoke lugha nyepesi, Nape alitolewa bastola mchana mbele ya Camera na mtuhumiwa mpaka leo hakuna kimetokea- sasa wamepiga Risasi saa saba mchana ndani ya Gari bila kujali wangapi wangekufa - ni mambo hatari sana haya.

Tukiyafumbia macho hili neno la watu wasiojulikana litakuja kuwa mwiba kwetu wote.

Iwe ni siasa, visa, chuki, au kitu chochote kile sio jambo jema kulishangilia - Nchi ina katiba, polisi, mahakama, jela na magera kwa sababu ya kutokufanya mambo kama haya. Tusiruhusu haya matukio ndio yawe namna ya kutoa haki.

Hakuna atakayebaki salama mto ukitibuka.
 
duh[emoji22][emoji22][emoji22]....very sad aki ya nan tupo bongo Bahati mbaya,

Sent using Jamii Forums mobile app
Jalibuni kua na weredi..wako sawa,sasa kama kuna raia aliona au ana hisi watu/mtu fulani why asipeleke taarifa?mbona ni kitu cha kawaida tu na ni msaada tosha

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Nimemssikia IGP Sirro akiongea na media jana akisema Jeshi la Polisi liko serious(makini)kwenye kuchunguza nani waliohusika na shambulio la mauaji kwa Mbunge Tundu Antipas Lissu.
Ahadi za IGP kwamba wako makini na watawakamata waliohusika na shmabulio hilo zinaonesha hammanishi anachokisema. Nitaeleza.

Kuna habari za kuaminika kwamba gari lililokuwa likimfutilia Tundu Lissu toka Bungeni akielekea nyumbani kwake mchana huo ni GARI LINAJULIKANA na ndiyo hilo hilo ambalo hata Mbunge wa MTAMA(CCM) Nnape Nnauye amelitaja jana alipohojiwa na media. Nnape Nauye amesema alipoongea na BBC kwamba kwa nchi ambayo inaheshimu Utawala wa Sheria haiwezekaqni watu wawe wana toa taarifa kwa Polisi Nnape akiwa mmoja wao kwamba kuna GARI LINAWAFUATILIA na ni gari hilohilo lilimewahi kumfutilia Lissu alipolitaja kwa rangi na namba zake. Gari hilo ni T460CQV aina ya Toyota Premio la vijana wa TISS. Angalia Link hii ni ushahidi tosha: Youtube
Tundu Lissu alitoa taarifa hizi kwa IGP Sirro na Kamanda Kipilimba akiwatuhumu kuwatuma watu wa Usalama wa Taifa kumfuatilia TL badala ya kufanya kazi ya kufuatilia wahalifu.

Kama IGP Sirro yuko serious basi aanze na hili gari T460 CQV linaloendeshwa na vijana wa TISS. Watu hawa ndio walio mnyoshea bastola/bunduki Nnape Nnauye alipofukuzwa Uwaziri alipounda Tume ya kuchunguza sakata la RC Paulo Makonda baada ya kuvamia Clouds TV akiwa na Polisi. Hivo IGP Sirro anza na usajili wa gari hilo kujua nani mmiliki wake,anakaa wapi ana kazi gani na ana uhusiano gani na TISS. Nina hakika akipatikana mwenye gari hilo basi waliotaka kumwangamiza Tundu Lissu nao watapatikana.
Kazi kwako Kamanda Sirro if and only if you mean serious about this business.
Nje ya hayo IGP Sirro anaenda kuwa IGP ZIRO(0).
 
Back
Top Bottom