Wana JF,
Tunajua kuwa mara baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi kumekuwa na dhana tofauti na hata baadhi ya watu kutuhumu wengine. Kwa kuwa hapa ni pahala pa GT, tunaweza kusukuma fikra na mazungumzo katika hatua ya pili. Hii ni hatua muhimu ya kusaidia kuibua hoja/clue ya kusaidia/kuwezesha vyombo vya dola/upelelezi kufuatilia tukio husika kwa ufanisi.
Tunapendekeza GT wenye hoja/clue musharabu zinazoweza kusaidia upepelezi wa sakata la Tundu Lissu waziweke hapa bila mawaa wala matusi na kukashifiana. Tunaomba JF Moderator(s) kutounganisha uzi huu na nyuzi nyingine. Aidha tunawapa mandate ya kuondoa/kufuta comments zozote zinazojikita kutukana, kukejeli au kutuhumu yeyote bila ushahidi wowote.
Kwa kuanzia, katika upelelezi tunapendekeza wapelelezi kuzingatia haya
1. [Kwamba Mbowe alikuwa mtu wa mwisho kukutana na Tundu Lissu kabla ya Lissu kushambuliwa kwa risasi, maana walipatachakua cha mchana pamoja]. Tunapendekeza upelelezi usaidie kupata na kutathmini taarifa zifuatazo;
i. Mahali ambapo Lissu na Mbowe walikula chakula cha mchana siku hiyo.
ii. Baada ya kuachana Mbowe aliongea na nani na aliongea nini kwenye simu yake.
iii. Lissu aliongea na nani na aliongea nini kwenye simu yake.
iv. Dreva wa Lissu aliongea na nani na aliongea nini kwenye simu yake.
v. Mtu wa kwanza kutoa taarifa za Tundu Lissu kupigwa risasa na alimtaarifu nani.
vi. Mtu wa kwanza kutoa taarifa za Tundu Lissu kupigwa risasi kwa umma (vyombo vya habari, mitandao ya kijamii).
2. [Kwamba dreva wa Tundu Lissu aliona na kuonya kuwa kulikuwa na gari likiwatuatilia, kisha kumuonya Lissu asitoke kwenye gari]. Tunapendekeza upelelezi usaidie kupata na kutathmini taarifa zifuatazo;
i. Dreva alijuaje kuwa kulikuwa na gari likiwafuatilia (ikiashiria hali ya shari/hatari).
ii. Dreva aeleze iwapo hilo gari analiweza kulielewa, analikumbuka na iwapo anaweza kutambua specific features (make, rangi, namba za usajili na feature nyingine kama ipo).
iii. Wakati washambuliaji wakipiga risasi gari la Lissu dreva alikuwa wapi; alijificha/alikimbia.
iv. Dreva alifanya kitendo gani kwanza, mara baada ya kufanya uhalifu huo; kama alipiga simu kutoa taarifa alimpigia nani na alisema maneno gani, na kama alianza kum-attend Lissu kwa kumpatia huduma ya kwanza, alifanya kitendo gani.
3. [Kwamba, kwa mujibu wa taarifa ya Mbowe (10/09), dreva wa Lissu naye yuko Nairobi akipata matibabu kumwondolea trauma]. Tunapendekeza upelelezi usaidie kupata na kutathmini taarifa zifuatazo;
i. Dreva wa Lissu alikwenda Nairobi lini na alitumia usafiri gani.
ii. Anapata matibabu hayo katika hospitali gani na kwa utaratibu gani.
iii. Nani anagharimia matibatu hayo na kwa nini,
iv. Iwapo dreva ana- referral ya matibabu yake kufanyika Nairobi, ilitolewa na mamlaka gani na lini.