Jeshi la Polisi limetoa tamko kufuatia taarifa za watu kupotea, kutekwa au kukamatwa na wanaodaiwa kuwa askari. Polisi wamesema hufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuthibitisha ukweli wa tukio, na haiwezi kusemwa moja kwa moja mtu amepotea bila ushahidi.
Kwa mujibu wa sheria, mtu hutambulika kuwa amepotea rasmi baada ya miezi mitano kupita na mahakama kuthibitisha. Jeshi hilo limewahakikishia wananchi kuwa linachukua kwa uzito kila taarifa, huku likitoa wito kwa ndugu wa wahusika kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.
Aidha, Polisi limeonya kuwa kusambaza taarifa za uongo ni kosa la jinai linaloweza kupelekea faini ya hadi milioni tano au kifungo cha miaka mitano.