Polisi kuhusu taarifa za watu kutekwa: Ni kujiteka, wivu wa mapenzi na kugombea mali

Yaan bora wangeendelea kumute.....kafri wanavyoleta hizi ngonjera ndo tunapata kujua uhalusia wao zaid
 
Hivi hawa watu (mapolisi) wanatuona mambumbumbu kiasi hiki kweli?
Hizi ni taarifa za kuleta kwa watu wenye akili kweli?
Hii ni dharau sana sana kwa Watanzania na ni bora wangekaa kimya!
 
Tumepikea taarifa. Tunaomba ziwe zinatoka mapema kuondoa sintofahamu.
 
Unawezai kuwapumbaza watu wachache kwa muda wote lakini siyo watu wote kwa muda wote

Polisi wameshindwa kukomesha utekaji Tanzania, watanzania wengi wamepotezwa wengi wao wakishuhudiwa kupotezwa na wanaojitambulisha kama polisi

Haiwezekani watu wapotezwe ionekane wamepotea kama kuku yaani iwe ni kitu cha kawaida tu ni sawa na kifo ni kifo tu
 
Kule UN alikuwepo Possi akiuhadaa ulimwengu, ati kuna demokrasia, hapa napo propaganda ika tawala, lakini wana jisahau kwamba kila kitu kiko wazi
 
Sikusoma yote, Kuna sehemu wameeleza kama yule kada wa ccm aliyemtishia Dr Kitima kishakamatwa?
hawezi kukamatwa wala kutiwa hatiani. sasa hivi yupo mtaani anakula bata na huwezi jua huenda anatembele V9 sio V8
 
Umoja wa mataifa hauwezi kukubaliana na hiyo ripoti niko pale!
 
Hiyo speech anaeweza labda kuwaelewa ni mtoto wa KG I pekee, mimi sijawaelewa hata msitari mmoja.
 
Mtu Mweusi anamatatizo makubwa sana ya kutojitambua. Nchi nyingi Afrika zina dosari nyingi za kuto jielewa, kutojiamini, kutojijali.
Sasa taarifa kama hii ni kwa kumfuraisha nani? Ndiyo maana hata Black diaspora hawataki kujiusisha ni Bara hili lilo jaa dhuluma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…