Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Tanzania haina utaifa bali unafiki. Mara mzozo na Wazanzibari, mara CDF adai wageni wako kwenye nafasi za maamuzi, mara Sukuma Gang, mara Kaskazini au Wachaga kamwe hawawezi kuruhusiwa nafasi ya uRais, mara huko maendeleo yametosha sasa zamu ya wengine. Kauli zinazotolewa na viongozi wenye dhamana. Kinachoshikamanisha Tanzania ni utawala wa kiimla na matumizi ya vyombo vya dola kwa uwazi na kificho kudhibiti waleta chokochoko dhidi ya watawala. Tanzania hata upinzani rasmi (official opposition) ni uadui au usaliti.Kwa mimi ambaye siangalii mambo kwa lens ya wao na wale au huku na kule..., nilishasema na ninasema kila siku USA kutokana na division iliyopo ina a soft underbelly ni rahisi kupata an enemy within katika nchi yenyewe tofauti na sehemu kama Russia na China hata mambo yakiwa mabaya / mabovu kiasi gani watu wote ni rahisi ku-PERSEVERE....
Ndio maana nasema kila siku Tanzania tuna mtaji mkubwa sana ambao duniani wengi hawana (nao ni Utaifa) tatizo tu ni walamba asali na wapuuzi wachache wanaotaka kuondoa hilo kwa kutugawa kwa vijitofauti vyetu (ambavyo waasisi walijaribu kuviondoa) badala ya kuunganika kwa our common goals....
Anyway binafsi am all for Justice haijalishi injustice kaifanya nani lazima nitalaani...
Nyerere alidai kuwa enzi zake ukabila waliuzima LAKINI akatoa tahadhari kuwa lazima siku zote tuchukue hatua kuhakikisha haujitokezi. Kwamba tusijidanganye huku kwetu ukabila uko juu juu tu ukikwaruza ngozi kidogo tu unatokeza kama damu.
USA ni open global society. Watu wengi duniani wanatafuta uraia wa Marekani. Hilo ndilo changamoto lake kubwa; pia ndipo ilipo nguvu yake kubwa. Best brains za dunia zinaelekea huko. USA imeweka utawala makini wa sheria na taasisi imara kila nyanja kudhibiti maadui wa taifa na wamefanikiwa sana. Ingekuwa rahisi sana kuisambaratisha USA enzi za cold war lakini madikteta na magaidi wakuu duniani walishindwa. USA iko macho full-time kuimarisha mifumo yake na kufuatilia maadui wa ndani na nje 24/7. Wanajua demokrasia ni mapambano ya kudumu.
Hiyo unayoiita soft-underbelly ukimaanisha mgawanyiko nchini iko kila nchi. Hakuna nchi iliyopona hapo. Wengine wanatumia udikteka na vyombo vya dola (kama sisi) kuudhibiti. US wanatumia demokrasia, sheria na taasisi kuweka mambo sawa. Na kukuonyesha uimara wa mfumo wa USA, miaka ya 80-90 waliisambaratisha dola ya kiimla ya USSR na kuvutia (influence) mageuzi makubwa ya kisera nchini China kuingiza uchumi wa soko, umiliki binafsi wa mitaji, na uwekezaji wa nje yote chini ya udhibiti wa dola (command economy).
