Polisi: Tumewakamata watuhumiwa waliokula njama ya kutaka kumteka Tarimo - Kiluvya

Hahababaa 2qtqnzania banaa.....tunachezewa sana akili z4tu wengi ni ..........wote wale wanajulikana na majina yao na vitengo vyao....wanahamisha magoli...hahaha khaaaa acha nicheke
 
Siku 23 tangu video za jaribio la kutaka kumteka Deogratius Tarimo, mkazi wa Kiluvya jijini Dar es Salaam zisambae, hatimaye Jeshi la Polisi limesema linawashikilia watuhumiwa wanane wa tukio hilo.

Taarifa ya kushikiliwa kwa watu hao imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro leo Jumanne, Desemba 4, 2024.

"Tarehe 11 Novemba, 2024 eneo la Kiluvya, Ubungo Dar es Salaam lilitokea tukio la kutekwa kwa Deogratius Tarimo, mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha mkoani Pwani.

"Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imefanikiwa kukamata kundi la watu wanane wanaotuhumiwa kula njama kwa pamoja na baadaye kufanya tukio la kumteka Deogratius Tarimo. Watuhumiwa wamekamatwa kwa nyakati tofauti Dar es salaam, Songea Ruvuma na eneo la Mbingu Mlimba, Morogoro,"imeeleza taarifa hiyo.

Pia imeongeza kuwa: "lilipatikana gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa tukio hilo, huku ikitumia namba isiyo halisi T 237 EGE na baada ufuatiliaji namba halisi ya gari hiyo ni T237 ECF."

Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa hao kuwa ni Bato Bahati Tweve (32), Bondia, mkazi wa Kimara Bunyokwa na Songwe Mbozi, Yusuph Abdallah (32), mkazi wa Mbingu Mlimba, Morogoro, Fredrick Juma (31), mkazi wa Kibamba na Nelson Elimusa (24) maarufu msela, dereva teksi, mkazi wa Mbezi Luguluni.

Wengine ni Benk Daniel Mwakalebela (40) maarufu tall, mkazi wa Mbezi -Makabe na Kyela Ipinda, Rusungo Mbeya, Thomas Ephraim Mwakagile (45) maarufu Baba Mage, mkazi wa Bunyokwa na Kyela Ngonga Ndiali- Mbeya, Anitha Alfred Temba (27), mkazi wa Mbezi Mwisho na Isack Mwaifani, maarufu boxer, mkazi wa Kimara Tembo Salanga na Bujonde Isanga Kyela, Mbeya.
 
Kazi nzuri kama ni kweli. Isije ikawa mmechukuwa watu mahabusu na kuwabebesha hii kesi maana ndio michezo yenu
 

Kutoka hapa sijui picha linaepekea wapi, naahindwa kulitabiri
 
Huwa wana kawaida ya kuwapiga picha na kuwaweka hadharani basi tunaomba hata hao wapigwe picha na kuwekwa hadharani ili raia wawatambue kama watu hatari iwapo wataonekana mtaani
 
Polisi imesema imewakamata Watu 8 kufuatia tukio la kutaka kumteka Mh Tarimo Bonge wa Kiluvya

Source: Ayo TV
 
Watu wanane wamekatwa;
Bahati Tweve
Yusuf Abdallah
Frederick Juma
Nelson Eli Musa
Frank Daniel Mwakelebela
Thomas Ephraim
Anita Temba
Isaac Mwaifani.
Tukio la Kilivya,Kibaha
Yule white ni nani kati ya hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…