Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 11,936
- 15,196
Zinanunuliwa kama zinavyonunuliwa huko USA?Ukienda duka la Tanganyika Arm zinapatikana mkuu hata silaha zinauzwa hapo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zinanunuliwa kama zinavyonunuliwa huko USA?Ukienda duka la Tanganyika Arm zinapatikana mkuu hata silaha zinauzwa hapo.
Picha zao please Ili wale waliokuwa wanaeneza picha za uongo Twitter washughulikiwe nao.
Good question, ukijibiwa ni-tag tafadhali.Mnaowajua wale walioonekana kwenye video, ni kweli wametajwa hapa?
Kongole kwa Jeshi la polisi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na operasheni maalum kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Kwa ujumla hali ya usalama Dar es Salaam inaendelea vizuri.
Tarehe 11 Novemba, 2024 eneo la Kiluvya Ubungo Dar es Salaam lilitokea tukio la kutekwa kwa Bw. Deogratius Tarimo, mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani. Kufuatia tukio hilo na mengine ya nyuma Polisi Dar es salaam imekuwa ikiendelea kuchunguza na kufuatilia taarifa mbalimbali pia kukusanya ushahidi wa kisheria kuhusiana na matukio hayo ili kuyazuia.
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imefanikiwa kukamata kundi la wahalifu wanane wanaotuhumiwa kula njama kwa pamoja na baadae kufanya tukio la kumteka Deogratius Tarimo. Wat uhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti Dar es salaam, Songea Ruvuma na eneo la Mbingu Mlimba Morogoro. Pia lilipatikana gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa tukio hilo huku ikitumia namba isiyo halisi T 237 EGE na baada ufuatiliaji namba halisi ya gari hiyo ni T237 ECF.
Watuhumiwa hao ni :-
1. Bato Bahati Tweve, Bondia, Miaka 32, Mkazi wa Kimara Bunyokwa na Songwe Mbozi
II. Yusuph Abdallah, Miaka 32, Mkazi wa Mbingu - Mlimba Morogoro
III. Fredrick Juma, Miaka 31, Mkazi wa Kibamba
IV. Nelson Elimusa msela, Dereva Tax, Miaka 24, Mkazi wa Mbezi Luguluni
V. Benk Daniel Mwakalebela@tall, Miaka 40, Mkazi wa Mbezi Makabe na Kyela Ipinda
Rusungo Mbeya
VI. Thomas Ephraim Mwakagile @ baba mage Bunyokwa na Kyela Ngonga Ndiali Mbeya Miaka 45, Mkazi wa Kinyerezi
VII. Anitha Alfred Temba, Miaka 27, Mkazi wa Mbezi Mwisho.
VIII. Isack Mwaifani, @ boxer, Mkazi wa Kimara Tembo Salanga na Bujonde Isanga Kyela Mbeya
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi ya kuzuia vitendo vya kihalifu lakini pia kuwakamata na kutokuwa na huruma kwa watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria kwa kuwapeleka kwenye mamlaka zingine za haki.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za kweli ili Jeshi lichukuwe hatua za kisheria kwa watu wanaopanga kufanya matukio ya kihalifu ili washughulikiwe mapema kabla ya matukio.
Imetolewa na;
Muliro J. Muliro -SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam
www.polisi.go.tz
www.twitter.com/tanpol
Nafikiri kuna process ya umilikajiZinanunuliwa kama zinavyonunuliwa huko USA?
Hata majambazi hupata silaha piasasa wewe pingu unadhani ni kitu kigumu kukipata, wakati huko dark market kilakitu haramu kinauzwa.
Kweli zipoNafikiri kuna process ya umilikaji
Unafikiri bila Ile video kuna mtu angekamatwa?😔Mmmh ngoja tuone!! Vipi na watekaji wa mzee kibao na akina Soka hii ya juzi juzi naona fasta!!!
Yawezekana ni imani za ajabu ajabuSababu ya utekaji mbona haikutajwa
Ili na Mzee Kibao ionekane alitekwa na wahalifu. Hii picha imebuma😔Kuna mtu alisema kuwa lile jaribio ni mchongo ili kubalance story.
Naanza kuziona dalili hizo.
Na wamzee wa Tanga je?Watu wanane wamekatwa;
Bahati Tweve
Yusuf Abdallah
Frederick Juma
Nelson Eli Musa
Frank Daniel Mwakelebela
Thomas Ephraim
Anita Temba
Isaac Mwaifani.
Tukio la Kilivya,Kibaha
ZipoKweli zipo
🤣🤣🤣🤣 Nimeona nikasema hizi mbwembwe vipi,?. Ni kama MTU aliekuwa anaongea uongo huku akiaminisha watu kuwa ni kweli. Drama.Kamanda Murilo kalielezea hili tukio kwa mbwembwe sana
Wamo kabisaMbona katika hao waliokamatwa sioni hata sura moja ya wale waliokuwa kwenye ile video?
Yeah, inamaana hao wataenda kotini kutoa sababu za mapenzi, au kudhulumiana hela za madawa ya kulevya.Ili na Mzee Kibao ionekane alitekwa na wahalifu. Hii picha imebuma😔