Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma
  1. Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
  2. Rais wa TEC, Askofu Pisa apingana na polisi, asema taarifa yao kuwa Padri Kitima alikuwa anapata kinywaji wakati anashambuliwa ni Upotoshaji
😆😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom