Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Kwahiyo wewe ukienda kuandikisha kupiga kura utakubali kupima stool kama mwandikishaji atakutaka?
Irrelevant argument...ukienda kujiandikisha halafu ukawa unabwabwaja na ukakamatwa na kuhisiwa umelewa ni muhimu kupimwa ili tujue umetumia kinywaji au dawa za hospitali kwani sio jambo la kawaida.
 
 
Amelala mahabusu, wanasheria wake wamezuiwa kumwona, chakula na maji kapewa na akiwa mahabusu. Ni mahakama zetu tu zitakazokubaliana na matokeo ya vipimo hivo. Kama si jambo la kupanga ili kumshughulikia, police makini wangempeleka kwa mkemia tangu walipomshika airport.
 
Gwajima na wale wengine walisingiziwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati Lissu amezushiwa kesi ya uchochezi, sasa mkojo na uchochezi wapi na wapi
Soma bandiko langu vizuri ili uhusianishe uchochezi na ulevi
 
Hivi kuna sheria inayompa DPP/Jeshi la Polisi mamlaka ya kumpima mtu yoyote mkojo ambae hajakutwa na madawa ya kulevya au kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya?

Polisi/DPP anaweza tu kwa utashi wake kuamua mtu fulani apimwe kama anatumia madawa ya kulevya?

DMtu ambae si teja na wala hajakutwa na madawa ya kulevya,unampimaje mkojo kama wewe sio daktari?

Sheria hapa inasemaje?
 
Irrelevant argument...ukienda kujiandikisha halafu ukawa unabwabwaja na ukakamatwa na kuhisiwa umelewa ni muhimu kupimwa ili tujue umetumia kinywaji au dawa za hospitali kwani sio jambo la kawaida.
 
Yaani kesi ya uchochezi imehamia kweye kupima mkojo? Kweli sasa nimeshaamini kumbe walioko magereza sio wote ni wahalifu!
 
Itatoka tu amri ya mahakama apimwe; na atuambie hao wanaomuuzia ni kina nani. kukataa means kuja jambo anataka kulificha.
Tumia akili, tangu lini umesikia Lissu ameshitakiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya? Mahakama inawezaje kutoa maelekezo kwa kesi ambayo hawana mbele yao? Yaani mtu atuhumiwe wizi, halafu mahakama iamrishe apimwe VVU?
Umechanganyikiwa Dogo.
 
Heheheh angekubali tu ungesikia anapewa kesi ya kutumia madawa ya kulevya
 
Kama ni mlevi wa pombe je?na kama alikuwa na harufu ya pombe je?
 
Wanampima mkojo ili wajue kama anatumia yale madude waweze kumpa akiwa ndani. Wasipompa wakati amezoea kuyatumia ataathirika zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni hatua mojawapo ya upepelezi wa Polisi! Siku hizi wamegundua kuwa kuna vimelea vya uchochezi vinapatikana kwenye mkojo kwa hiyo ni hatua mojawapo ya kukusanya ushahidi wao dhidi ya uchochezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…