Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Kwahiyo wewe ukienda kuandikisha kupiga kura utakubali kupima stool kama mwandikishaji atakutaka?
Irrelevant argument...ukienda kujiandikisha halafu ukawa unabwabwaja na ukakamatwa na kuhisiwa umelewa ni muhimu kupimwa ili tujue umetumia kinywaji au dawa za hospitali kwani sio jambo la kawaida.
 
Hili ni jambo la kushangaza sana!

Ni kwa nini lissu aogope kupimwa mkojo ikiwa ni utaratibu wa kawaida sana kwa mtu anayehisiwa kuwa under influence of medication?

Gwajima alipimwa mkojo bila mtafaruku na akaachiwa bila shida.

Je lissu anaficha nini?

Kwa wataalamu wa afya watakubaliana na mimi kuwa mtu yoyote anayebwabwaja kiasi cha kukamatwa na polisi ni lazima apimwe ili kuondoa uwezekano wa yeye kuwa na chembechembe za ulevi.

Inashangaza sana kwa lissu kugomea kipimo cha kawaida kabisa ili kujisafisha na kuondoa doubts.

Nashauri Polisi wampeleke kwa mtaalamu wa afya ya akili ...psychiatrist ili kuondoa uwezekano wa ukichaa wa lissu...huku nako asije akagomea kwani itakuwa ni the so called "denial" au poor insight
23e67344965d626fa527fcf4b5bb713d.jpg
 
Amelala mahabusu, wanasheria wake wamezuiwa kumwona, chakula na maji kapewa na akiwa mahabusu. Ni mahakama zetu tu zitakazokubaliana na matokeo ya vipimo hivo. Kama si jambo la kupanga ili kumshughulikia, police makini wangempeleka kwa mkemia tangu walipomshika airport.
 
Gwajima na wale wengine walisingiziwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati Lissu amezushiwa kesi ya uchochezi, sasa mkojo na uchochezi wapi na wapi
Soma bandiko langu vizuri ili uhusianishe uchochezi na ulevi
 
Hivi kuna sheria inayompa DPP/Jeshi la Polisi mamlaka ya kumpima mtu yoyote mkojo ambae hajakutwa na madawa ya kulevya au kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya?

Polisi/DPP anaweza tu kwa utashi wake kuamua mtu fulani apimwe kama anatumia madawa ya kulevya?

DMtu ambae si teja na wala hajakutwa na madawa ya kulevya,unampimaje mkojo kama wewe sio daktari?

Sheria hapa inasemaje?
 
Yaani kesi ya uchochezi imehamia kweye kupima mkojo? Kweli sasa nimeshaamini kumbe walioko magereza sio wote ni wahalifu!
 
Itatoka tu amri ya mahakama apimwe; na atuambie hao wanaomuuzia ni kina nani. kukataa means kuja jambo anataka kulificha.
Tumia akili, tangu lini umesikia Lissu ameshitakiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya? Mahakama inawezaje kutoa maelekezo kwa kesi ambayo hawana mbele yao? Yaani mtu atuhumiwe wizi, halafu mahakama iamrishe apimwe VVU?
Umechanganyikiwa Dogo.
 
Heheheh angekubali tu ungesikia anapewa kesi ya kutumia madawa ya kulevya
 
Hivi kuna sheria inayompa DPP/Jeshi la Polisi mamlaka ya kumpima mtu yoyote mkojo ambae hajakutwa na madawa ya kulevya au kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya?

Polisi/DPP anaweza tu kwa utashi wake kuamua mtu fulani apimwe kama anatumia madawa ya kulevya?

DMtu ambae si teja na wala hajakutwa na madawa ya kulevya,unampimaje mkojo kama wewe sio daktari?

Sheria hapa inasemaje?
Kama ni mlevi wa pombe je?na kama alikuwa na harufu ya pombe je?
 
Hiyo ni hatua mojawapo ya upepelezi wa Polisi! Siku hizi wamegundua kuwa kuna vimelea vya uchochezi vinapatikana kwenye mkojo kwa hiyo ni hatua mojawapo ya kukusanya ushahidi wao dhidi ya uchochezi
 
Back
Top Bottom