Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya mapema leo polisi kuzuia msafara wa Tundu Lissu eneo la Kiluvya, hatimae wameondoka na kuacha uendelee na safari na Lissu amesema ataendelea na safari yake kama ilivyopangwa na atakutana na wanachama usiku huu. Baada ya polisi kuondoka, Lissu ameongea yafuatayo.
LISSU: Nasikia hata siku moja imewashinda na wameondoka, sasa kwa sababu walikuwa wametuzuia na lengo letu lilikuwa kwenda kukutana na wanachama wetu Mlandizi, sasa tunaelekea Mlandizi, lazima twende Mlandizi na tumemwambia mheshimiwa mbunge wetu, Kinabo awaambie watu wake ambao walikuwa wanatusubiri tangu asubuhi kwamba, sasa tunaelekea Mlandizi kukutana na wanachama wetu.
Sheria haisemi kwamba, kama ilivyo sheria ya uchaguzi, haisemi mikutano ya wanachama nayo lazima ianze saa kumi na mbili mpaka saa kumi na mbili, tutafanya usiku na wanachama wetu.
Naomba niseme mambo mawili, la kwanza ni kumshukuru sana baba askofu Mwemakula kwa kuja kutuunga mkono hapa, Askofu Mwamakula amejidhihirisha katika kipindi hiki kigumu katika historia ya nchi yetu kwamba ni kiongozi wa kiroho kwelikweli, kiongozi ambae yuko tayari kusimamia ukweli wa imani yake. Sasa askofu Mwamakula ni Desmond Tutu wa kwetu, tunahitaji viongozi wa kiroho ambao hawana hofu ya hizi mamlaka za kutisha tisha za utawala wa aina hii.
Tumekaa hapa tangu saa tano asubuhi, kuna watu wanafikiri tumepotezewa muda, hatujapotezewa muda. Unapopigania haki, ukweli lazima uwe tayari kupigania masuala ya msingi. Kama huruhusiwi kuonana na wanachama wako kwenye kikao cha ndani, anaambiwa uombe kibali cha mapolisi, kama hiyo huwezi kusimamia utasimamia kitu gani?
Kwa hiyo tulikuwa tuna haki ya kwenda tunapotaka ili mradi hatuvunji sheria, tusije tuka-negotiate kwenye masuala ya principle.
MLANDIZI
Baada ya kufika Mlandizi, makamu mwenyekiti, Tundu Lissu amefanya kikao cha ndani ambapo eneo hilo lipo ndani ya jimbo la Kibaha vijijini, nako akasema yafuatayo katika mengi,
LISSU: Kuna baadhi ya watu walishaanza kuniambia, sasa unajua mheshimiwa, message sent sijui nini.. Nawaambia message sent waondoke, wakiondoka ndio message sent sio sisi tugeuze tulikotoka. Mnafahamu mbwa akipigwa? Mkia huwa anauweka wapi? Enhe tuufyate turudi Dar es Salaam wakati haki yetu, hiyo mimi sikubaliani na mambo kama hayo.
PIA SOMA,
CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wa CHADEMA Tundu Lissu ukielekea Kibaha
RPC Pwani Wankyo Nyigesa: Tutakesha na Tundu Lissu, ndiyo kazi yetu
Askofu Mwamakula aenda alipozuiliwa Lissu kumtia nguvu