Uchaguzi 2020 Polisi waondoa kizuizi alichowekewa Tundu Lissu Kiluvya. Asema anaendelea na safari yake

Uchaguzi 2020 Polisi waondoa kizuizi alichowekewa Tundu Lissu Kiluvya. Asema anaendelea na safari yake

Ndio ..siko familiar na member wengi humu ..wengine nawafahamu kwenye topic kama hizi kwa hisia na mihemko. But unfortunately Mimi huwa napenda mijadala iliyonyooka sipendi kutanguliza hisia na mapenzi katika hoja zangu.
Shukuru Mungu umemjua sasa huyo
 
Baada ya mapema leo polisi kuzuia msafara wa Tundu Lissu eneo la Kiluvya, hatimae wameondoka na kuacha uendelee na safari na Lissu amesema ataendelea na safari yake kama ilivyopangwa na atakutana na wanachama usiku huu. Baada ya polisi kuondoka, Lissu ameongea yafuatayo.

LISSU: Nasikia hata siku moja imewashinda na wameondoka, sasa kwa sababu walikuwa wametuzuia na lengo letu lilikuwa kwenda kukutana na wanachama wetu Mlandizi, sasa tunaelekea Mlandizi, lazima twende Mlandizi na tumemwambia mheshimiwa mbunge wetu, Kinabo awaambie watu wake ambao walikuwa wanatusubiri tangu asubuhi kwamba, sasa tunaelekea Mlandizi kukutana na wanachama wetu.

Sheria haisemi kwamba, kama ilivyo sheria ya uchaguzi, haisemi mikutano ya wanachama nayo lazima ianze saa kumi na mbili mpaka saa kumi na mbili, tutafanya usiku na wanachama wetu.

Naomba niseme mambo mawili, la kwanza ni kumshukuru sana baba askofu Mwemakula kwa kuja kutuunga mkono hapa, Askofu Mwamakula amejidhihirisha katika kipindi hiki kigumu katika historia ya nchi yetu kwamba ni kiongozi wa kiroho kwelikweli, kiongozi ambae yuko tayari kusimamia ukweli wa imani yake. Sasa askofu Mwamakula ni Desmond Tutu wa kwetu, tunahitaji viongozi wa kiroho ambao hawana hofu ya hizi mamlaka za kutisha tisha za utawala wa aina hii.

Tumekaa hapa tangu saa tano asubuhi, kuna watu wanafikiri tumepotezewa muda, hatujapotezewa muda. Unapopigania haki, ukweli lazima uwe tayari kupigania masuala ya msingi. Kama huruhusiwi kuonana na wanachama wako kwenye kikao cha ndani, anaambiwa uombe kibali cha mapolisi, kama hiyo huwezi kusimamia utasimamia kitu gani?

Kwa hiyo tulikuwa tuna haki ya kwenda tunapotaka ili mradi hatuvunji sheria, tusije tuka-negotiate kwenye masuala ya principle.

PIA SOMA,
CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wa CHADEMA Tundu Lissu ukielekea Kibaha

RPC Pwani Wankyo Nyigesa: Tutakesha na Tundu Lissu, ndiyo kazi yetu


Askofu Mwamakula aenda alipozuiliwa Lissu kumtia nguvu
Kwa Tundu Lissu kila goti litapigwa. Kila mahali wanabana wanaachia.

Huyu ndiye Lissu bwana.
 
Kwa uelewa wako kwa case ya Leo kulikuwa na urazima wa kuingia barabarani?
Au waingie barabarani kwa sababu gani?
Wewe ulitaka waingie barabarani ili iwe mini na je wameambiwa na kipngozi wao waingie barabarani ikiwa lipi likitokea?
😂😂😂 Mmeanza tena kumtetea na kujifanya mashujaa huku mtandaoni??
Wabongo sijui mtaacha lini unafiki.
 
Wananchi wapi mkuu.?

Polisi wameona usiku huu Lisu anaweza kubondwa hata jiwe la kichwa tukaahirisha uchaguzi wakati sisi tunahamu ya kumla kwenye box la kura tarehe 28.

Hivi ile mikwara yenu huwa ya nini hasa? Maana Lisu kakalishwa masaa 8 hakuna hata nzi kasogea hapo
Unabadirisha vilio kama mwanamke anayepigwa m.iti....
 
Upinzani wa bongo|Tanzania bwana!.

Ukiachiwa huru|ukipewa haki yako uongozi unakua umelegea..Haha.

Sawa,Endeleeni kuvunja sheria tu kwa kutafuta political violence.

Itafika mahali itabidi kila mtu mwenye madaraka atimize wajibu wake ipasavyo.
Huyu Ndio mpinzani. Sababu walizomzuia zimeisha?? Polisi tunajua hawana kosa na hawana mamlaka ya kukaidi order za bosi wao. Hili jeshi na lenyewe linateseka kuwa mikononi mwa madilitata uchwara.
 
😂😂😂 Mmeanza tena kumtetea na kujifanya mashujaa huku mtandaoni??
Wabongo sijui mtaacha lini unafiki.
Sisi mashujaa .......mmebana mmeachia. Huyo ndie Lissu bwana. Mtatema ndoano mwaka huu. Na kumtangaza Ushindi itakuwa hivi hivi.
 
Upinzani wa bongo|Tanzania bwana!.

Ukiachiwa huru|ukipewa haki yako uongozi unakua umelegea..Haha.

Sawa,Endeleeni kuvunja sheria tu kwa kutafuta political violence.

Itafika mahali itabidi kila mtu mwenye madaraka atimize wajibu wake ipasavyo.
Mbona unaji contradict? Itakuwaje wapewe haki yao kwa kuachiwa huru na wakati huo huo wawe wamevunja sheria?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Mmeanza tena kumtetea na kujifanya mashujaa huku mtandaoni??
Wabongo sijui mtaacha lini unafiki.
Mkuu..unanifahamu vizuri au unanifuatilia vizuri?

Katika post zangu mbona nishasema Mimi sins chama..nipo huru kukososa au kukubaliana na chama Fulani katika jambo Fulani..ila siko binding na chama kama watu walio wengi.

Na katika post yangu sidhani kama nimetaja chama..

#kumbuka ;

* Great mind discuss idea

* Average mind discuss event

*Low mind discuss people

So jiangalie upo kundi gani.
 
Back
Top Bottom