Pombe ndio chanzo kikuu cha Waislam na Wasabato kula kitimoto

Pombe ndio chanzo kikuu cha Waislam na Wasabato kula kitimoto

Wasabato msingi mkuu wa imani yao ni Biblia.
Hilo ndio jambo la kwanza unatakiwa uliweke kichwani.

Wasabato wanaamini Biblia ni kitabu kitakatifu kilichoandikwa na watumishi wa Mungu, manabii, mitume na wafalme waliovuviwa kile kiitwacho Roho mtakatifu.

Katika Biblia, upande wa Torati.

Mungu anatoa amri ya vitu ambavyo watu wanatakiwa Wale(hivi huitwa vyakula) na vitu ambavyo havitakiwi kuliwa(huitwa visivyoliwa).

Nguruwe ni mojawapo ya wanyama walioharamishwa wasiliwe kwa mujibu wa Biblia. Kwa namna hiyo Wasabato hawamli Nguruwe kwa sababu ipo amri inayomzuia Nguruwe asiliwe.

Hata hivyo sio Nguruwe tu ambaye haliwi.
Wapo viumbe na wanyama wengine ambao sio chakula kwa mtu, mfano
Mbwa, sungura, ngamia, nyoka, binadamu n.k. wote hao waliharamishwa wasiliwe
Vipi kuhusu agano jipya? Maono aliyopata Petro kuhusu kuchinja na kula, na kukatazwa kuita najisi vilivyokwisha takaswa?
 
WhatsApp Image 2024-10-16 at 19.49.43.jpeg
 
Back
Top Bottom