Pongezi kwa CDF Jenerali Venance Salvatory Mabeyo

Pongezi kwa CDF Jenerali Venance Salvatory Mabeyo

Huyo ni General mpaka anakufa atabaki kuwa General,huyo sio bwana, daktari,profesa au mchungaji, yeye ni General tena wa halali,POPOTE anapojitambulisha hilo neno General lazima liwemo maana ni HAKI yake.
Kwa hiyo hata huko mbinguni atafufuka akiwa Jenerali
 
Siyo Kosa Kwa CDF kuandika kitabu Kumhusu Bwana Yesu Kristo

Kwa Maana hata Siku anaapa alishika Biblia na kuapa akisema Ee mwenyezi Mungu nisaidie

Kwa Maana nyingine kupitia kiapo chake alikiri Kuhitaji na kutegemea Msaada wa Mungu ambaye Biblia Ni kitabu chake yaani Kristo.
Kama ambavyo hata Waislamu wamekuwa wakifanya...

Na Siyo Mara ya Kwaza kwani Hata Raisi Alhaj Alli Hassan Mwinyi Neno 'Alhaj' Ni Cheo Cha Heshima Ambacho Ni Cha kidini.
 
Ni kosa? Kama ni kosa, ni kosa kwa mujibu wa nini? Katiba? Sheria?

Imekatazwa wapi kufanya alichokifanya?
Unafiki ni ugonjwa.Mama Samia alipositisha kuongea na mama aliyemletea shida yake,wanafiki walifanya ni tukio kubwa.
 
Hivyo ni vya Colombia au Mexico?

Hao ni wakuu wa majeshi? Majenerali?

Unaelewa Chaplain ni nini katika jeshi la Marekani?

Tanzania tuna Chaplain?

Kuna mtu kataja Yesu katika covers za hivyo vitabu?
Mkuu ukiamuaga kuvuruga mada huwa unanikosha sana😆😁
Hapa Uzi utatembea Kwa ajili ya hizi critics na wenye mihemko watademka!
 
Alitakiwa atumia jina lake tu bila kuweka jenerali kwenye vitabu vyake vya kuendelea kuwapoteza Wagalatia wasio na akili
 
Mkuu ukiamuaga kuvuruga mada huwa unanikosha sana[emoji38][emoji16]
Hapa Uzi utatembea Kwa ajili ya hizi critics na wenye mihemko watademka!
Halafu mtu anashindwa kujibu maswali, anakuambia una chuki!
 
Anachanganya kazi na dini inaweza kumletea matatizo.

U Jenerali ni cheo chake kikazi, habari za Kristo ni dini yake binafsi, kwa nini anaweka U Jenerali kwenye kitabu cha Kristo, habari za imani yake binafsi?

Kwani na yeye ni Jenerali wa jina kama Jenerali Ulimwengu?
Hata Mungu ni wa majeshi!
 
Vyeo vyao ni vya maisha hata akifariki ataandikwa jina kwa cheo chake kwenye msalaba na kaburi. Yaani maofisa wote inakuwa hivyo. Hivyo hata kanisani ataitwa hivyo.
 
Vyeo vyao ni vya maisha hata akifariki ataandikwa jina kwa cheo chake kwenye msalaba na kaburi. Yaani maofisa wote inakuwa hivyo. Hivyo hata kanisani ataitwa hivyo.
Kwani nani kasema cheo si cha maisha?

Unaelewa hoja ninayozungumzia hapa?

Unaelewa kwamba raus wa nchi ni Mama na atabaki kuwa Mama maisha yake yote, lakini akisaini miswada hasaini kama Mama, anasaibi kama Rais?
 
Ni kama mwalimu, hata akistaafu anabaki kuwa mwalimu tu
Hoja kwamba yule si Jenerali.

Hoja katumia cheo cha Ujenerali kwenye kitabu cha dini.

Anachanganya Ujenerali na dini.
 
Siyo Kosa Kwa CDF kuandika kitabu Kumhusu Bwana Yesu Kristo

Kwa Maana hata Siku anaapa alishika Biblia na kuapa akisema Ee mwenyezi Mungu nisaidie

Kwa Maana nyingine kupitia kiapo chake alikiri Kuhitaji na kutegemea Msaada wa Mungu ambaye Biblia Ni kitabu chake yaani Kristo.
Kama ambavyo hata Waislamu wamekuwa wakifanya...

Na Siyo Mara ya Kwaza kwani Hata Raisi Alhaj Alli Hassan Mwinyi Neno 'Alhaj' Ni Cheo Cha Heshima Ambacho Ni Cha kidini.
Alhaji sio cheo cha kidini.Maana yake ni mhujaji yaani mtu aliyekwenda kuhiji Makka.
Akiwa wa kiume anaitwa Alhaji akiwa wa kike anaitwa Hajjah.
 
Hoja kwamba yule si Jenerali.

Hoja katumia cheo cha Ujenerali kwenye kitabu cha dini.

Anachanganya Ujenerali na dini.
Tatizo ni uelewa, rais akiingia kanisani au msikitini anaugua urais kwanza? Jenerali kaandika kitabu kuhusu dini yake, tatizo si yeye bali ni nyie
 
Back
Top Bottom