Hamjambo wote!
Mwanzoni wa Mwaka huu nilisikia Clip Moja ambayo ilikuwa ni Sauti ya Nabii Mmoja akijaribu kueleza maono aliyoonyeshwa na miungu yake.
Yule mtu aliyejitambulisha kama Nabii akawa anaeleza kuwa mwaka huu kuna msiba wa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa ameuona.
Hakusema ni mwenyekiti yupo, hakusema ni mstaafu au aliyepo madarakani.
Akaendelea kusema watu waombe Sana lakini hata hivyo maono yake yakamuomyesha haitawezekana atakufa.
Baada ya kusikia Maneno hayo, nami nikasema isiwe kesi Acha niangalie na kuuliza uliza kuhusu habari hizo kama zina ukweli kiasi gani.
Ripoti yangu ikanionyesha kuwa ni kweli huenda Jambo hilo linaweza kutokea. Lakini ripoti Ile nilipoifuatilia zaidi ikanionyesha kuwa Jambo hilo linaweza kutokea ikiwa kuna mtu ndani ya CHADEMA atadhulumiwa kwenye Uchaguzi uliokuwa bado haujafanyika.
Sasa huyo mtu ripoti haikumtaja kuwa ni nani wala huyo Mwenyekiti hakutajwa. Ila kulikuwa na Lugha za picha na michoro.
Sasa mimi kwa akili zangu ndogo nikajua mtu aliyekuwa kwenye Ile ripoti na mwenye hatihati ya kudhulumiwa nafasi yake nikajua atakuwa ni Lisu.
Ripoti inaeleza kuwa mtu huyo anaalama ya miungu.
Ndipo nikaandika huu uzi
Tahadhari: Tatizo la Lissu ana "MUKU" ya MIUNGU Ukimdhulumu lazima ufe.
Ingawaje wapo waliosema natumia Mbinu ya vitisho lakini ukweli ni kuwa nilieleza Yale yaliyomo kwenye ripoti
Zingatia, sio kila ninachoandika kinatokana na ripoti hizo.
Mengine ni maoni na mitazamo yangu binafsi, mengine ni just for funny, mengine kutaka kujadiliana na kuwasiliana na watu.
Ripoti inaeleza kuwa, mtu huyo asiye na jina(hakutajwa jina) alikuwa na Sababu ya kuishi (reason to Live) Mimi bado Kura yangu ikawa inamuangukia LISU.
Nikaandika Mada Ile nikilenga isitokee dhulma kwa mtu huyo ili kuepusha Kifo cha Mwenyekiti ambaye hakutajwa jina.
Lakini ripoti chini Kabisa inaeleza, ikiwa mtu huyo ambaye anachapa ya reason to Live akakengeuka basi kuna Hatari ya yeye mwenyewe Kufa. Nikasema eeh!
Kifo chake kwenye ripoti kinaelezwa kuwa kitakuwa cha ghafla Sana. Atakutwa amelala kitandani amekufa. Hiyo ni ripoti hiyo. Yaani hakitakuwa kifo cha kuuawa Wala kufanyiwa hila Wala Njama. Atakufa paap! Bila Mkono WA binadamu kuhusika.
Yule Nabii ametabiri yake. Mimi kama Mtibeli nimezuia utabiri huo lakini nimeona nitoe sehemu ya kilichopo kwenye Ile ripoti. Labda kwa sehemu itasaidia.
Nitatafuta kiambatanisho cha Sauti ya huyo Nabii nikiweke hapa. Pia kama kuna mtu anacho anaweza kuiweka kwa Sababu sio kwamba nilitumiwa Mimi Bali Mimi mwenyewe nilikisikia mtandaoni.
Nawatakia siku Njema