Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

kwa hiyoo asifanye ziara mkuu??? asionyee mawaziriii???
Sio asionye mawaziri, aishie kwenye kusisitiza utekelezaji wa ilani, hawezi kum summon Waziri Mkuu au mawaziri kwasababu yeye sio mamlaka yao ya nidhamu. Waziri Mkuu wa JMT hawezi kupewa maelekezo ya chama na mwenezi kwasababu PM ni mjumbe wa CC ya CCM. Huwezi kuwapigia simu mawaziri na kuwapa maelekezo kwasababu wewe sio rais wa JMT. Magufuli alikuwa anafanya hivyo kwasababu yeye ndio bosi wao!, Makonda asijifanye Magufuli!, huku ni kumu outshine his boss!.
P
 
Je kama boss ndo kamtuma??? kwani boss wake huwa anaonya wangapi?? mbona kwa hili hajasema nenoooo... kama mtu mzima ni rahisi kuelewa why makonda kateuliwa baada ya kukaa bench miaka lakini karudi na jeurii kubwa mnoo.
 
Makonda ni kama alijiandaa kwa nafasi aliyopewa. Kwa anachokifanya kanda ya ziwa ni sahihi kabisa maana kinazima mijadala iliyoanza 2021 na ambayo iliwaacha na simanzi wengi wao. Anatumia nguvu kubwa sehemu sahihi. Sitegemei atatumia mbinu hizo hizo zaidi ya miezi mitatu na akategemea kupata attention anayopata yeye binafsi na chama. Analeta amsha amsha kwenye serikali kwa kutumia mwamvuli wa chama,anasafisha reputation yake na anarejesha imani ya wananchi kwa chama. Si kazi ndogo.
 
Makonda ni jasiri, mpiga kazi ila ni sikio la kufa.
 
Yaani ukitaka kujua kuwa CCM walishaishiwa miaka mingi ni hizi hoja hapa. Hivi Bashite ana credibility gani hata za kusimama jukwaani?. Mmeamua kuleta wahuni ili kuimarisha uhuni.
 
Ila mkuu elimu unayosema hatuna tunahitaj 60 yrs ijayo ndio hio hio uliyopewa na chama.
Kismat cha mtu cha mtu tu
.napoleon bonaparte alikua kipenz cha watu,josip stalin
 
KIfupi kura hazikutosha labda kama mchezo ulichezwa eti labda 2015 lakini 2020 aahaa hakukuwa na kitu jamaa aliswaga mwendo bure!
Thubutu, sio kwa ushenzi ule wa 2020. Hakuna ccm ya kuweza kupata kura Zaidi ya 51%, na haitakaa iweze. Kama idadi ya wapiga kura wanasema ilikuwa 29m+, hapo unataka ushahidi gani kuwa ule ulikuwa ni uhuni? Watanzania baada ya sensa tuko 61m, inawezekana vipi nusu ya watanzania wawe wamejiandikisha kupiga kura? Kwahiyo watu wenye umri wa miaka 18+ wako sawa kwa idadi ya walio chini yake?
 
Pascal Mayalla

Hakuna amsha amsha ni kutafuta umaarufu kwasababu maalumu, kuficha maouvu
Publicity unaoyoiona si kwa ajili ya chama ni kujisafisha akijua ananuka dhulma na mikono imejaa damu!

Huyu bwana anafahamu aliumiza Umma, hakuna alichokifanya kikafanikiwa isipokuwa kusimamia mabaya. Amejaza vijana mitandaoni wana post upuuzi ili umma usahau au afiche maovu aliyotenda zama zile

Pili, anafanya kazi bila kufikiri kwasababu tu ya kutafuta umaarufu. Si mara ya kwanza kumbuka!

Mfano, juzi kaambiwa kuna maiti imezuiliwa Hospitali ya Sekotoure.
Bila kuuliza au kuwasiliana na Hospitali, mwenezi akaagiza ambulance ikachukue mwili kwenda kuzika

Hospitali ni institution (Taasisi) inaongozwa kwa procedures na guidelines. Maiti kuzuiliwa kuna sababu.

Inawezekana kuna deni la matibabu linalopaswa kulipwa. Mambo ya hovyo kama haya yanaua taasisi kwasababu zinashindwa kujiendesha. Ndiyo yale ya amri za kutoa pesa za mwenge kwenye mashirika, yakafa

Ningemuelewa kama angesema atalipia gharama hizo , mwili utolewe.
Kutoa amri tu ni kukurupuka na kuitia taasisi hasara. Nani atafidia deni hilo kama lipo?

Unaweza kuona hajabadilika, ndio yale ya wanaume kutelekeza watoto, madawa ya kulevya mkoa mmoja kana kwamba Dar ni kisiwa n.k.

Hajui mipaka ya kazi au tofauti ya uenezi na u-RC wala hajui 'coordination and engagement''

JokaKuu
 
Bro raisi wa Naijeria wa sasa alifoji vyeti vya elimu. Kule kuna wasomi wengi sembuse Makonda aka Bashite
 
Maji yakifika shingoni kwenye siasa yeyote mwenye kuweza kukuongezea uaminifu kwa wapiga kura anahusika.

Hata huyo Rish Sunak huko uingereza bada ya kubaini atoboi uchaguzi ujao; katika desperation ya kujiongezea truth-worthiness ya wapiga kura kamteua David Cameron kama waziri
 
Never outshine your boss!.
Mwenezi ni No. 7 kwenye hierarchy ya chama, ana mabosi 6 juu yake M/Kiti, M/Kiti Bara, M/Kiti ZnZ, KM, NKM Bara, NKM ZnZ ndipo anakuja Mwenezi!.
P
Sio kwamba ana lengo la ku outshine mabosi wake, ni kwamba hajui mipaka na wigo wa kazi zake
Bosi wa zamani alimpoteza kwa kumfanya aamini kwamba yeye ni mtu mkubwa na muhimu sana nchini

Hajui kuchagua maneno ya kuongea . Mfano, majuzi amewashambulia wastaafu na tunajua alimshambulia Warioba.
Leo JK ambaye ni mstaafu anamwakilisha Rais huko Finland, sasa sijui alimaanisha wastaafu wapi wakae kimya

Anapenda sana kufungua kinywa bila kupima uzito wa maneno yake.
By the way hajui kiswahili vizuri, utamsikia ''afazali, tahazali n.k. ''
 
p,

Kwan makonda amevuma sasa? au umaarufu wa makonda wa sasa unatokana haswa na kile kilichofanyika kwak huko nyuma? kwangu naona kama ngoja tuamke maana hatukuwa na kitu Cha kuangalia kwenye media.. walao Sasa wenye Muji wameingia...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi tuhuma ulizoporomosha kwa kuwa mnawanasheria nguli na ni za uhakika bila chenga,nilitegemea kesi ziwe nyingi dhidi yake hasa amekaa benchi miaka mitatu bila kuwa na Godi faza,mkashindwa,mlijua mmemmaliza kisiasa


Kaibuka kwa upya mmeanza tena ngonjera zenu,
Watanzania sio mafala
 
mkuu ukiona watu wanasema magu mpya Kwa makonda ujue kunakitu kimekosekana sehem na ccm wanakijua hapo bado mtu 1 tu team ikamilike yuleee mtu wa migomban ck akitia timu hata wale wenye mawazo mpadala itabidi wakune kichwa...



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hiki cheo cha Publicity secretary zamani wakati wa party supremacy kiliitwa '' Mass propaganda and mobilization''
Hiyo ni definition halisi ya kazi za Bwana huyu, kufanya propaganda za kueneza sera na kueleza mema ya chama halafu kufanya mobilization ili wananchi wajiunge na wakipigie kura chama.

Tumeyaona haya wakati wa mzee Msekwa, Daudi Mwakawago, Kingunge Ngombale n.k.

Tatizo la huyu bwana, ipo siku atamburuza Bosi wake chini kwa kukusudia au kwa bahati mbaya, that's imminent

Huyu bwana alimburuza chini JPM bila kutarajia wakati wa kampeni ya vyeti feki. Umma ulipodai atoe vyeti vna majina halisi, JPM alijua ukweli na waziri wakati ule nadhani alikuwa Hawa Ghasia akahamisha goli eti vyeti hawahusiki ma RC na huo ukawa mwisho wa zoezi la vyeti feki. JPM akafeli kwa zoezi la maana sana!

Mnachokiona sasa hivi si publicity ni ' political stunt' kwa mambo kadhaa ikiwemo kuusahaulisha umma maovu.
Mtakumbuka akiwa RC alikuwa na ofisi Clouds kwa ajili ya publicity, sasa hivi nadhani kaajiri vijana mitandaoni.

Publicity ni ile ya Nape na Kinana, kwenda kuonana na kuwasikiliza wananchi, kueneza sera, kupanga n.k.
Huo ndio ukweli, haya ya kupanda basikeli na malori ukiwa na V8 pembeni ni 'mockery' kwa masikini.

JokaKuu
 
Unakumbuka Tume ya maadili na kesi ya x-mayor wa Ubungo. Unakumbuka mahakama ilivyomkingia kifua pale kinondoni. Tunaongelea uenezi kama unataka kuingia kwingine sidhani kama ni wazo zuri!

Tufukue makabri?
 
Wastaafu watulie wakihitajika watatumika,waache viherehere,

Kwanini wastaafu umewaona warioba na Jakaya pekee?,unafiki wa hali ya juu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…