Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!

Vile mwili wa marehem sio ndugu yako mkuu.tumesikiliza wote aliyetoa ombi kasema mwil umekwama unadaiwa mil 2 utoke. Imetoka ambulance kwend kubeba sasa hapo procedure gani zaid ya kwend kulipa na ni kitu ambacho kimefanyika maana hueez kwend kubeba mwili bila kulipa gharama za matibabu. Hivi sisi huwa tuna shida gani
 
Rule No. 1. Never Outshine Your Boss

Rule No. 2. You Must Observe Rule No. 1
 
Na huko Hospitali ya Handeni amefariki mama mjamzito kwa kukosa pesa ya kufanyiwa operesheni ili atolewe mtoto!
Wanaona pesa ni zaidi ya uhai wa mama na mwanaye !!
Makonda fuatilia hiyo ya Handeni bado ni ya moto moto !!
 
Rudi kasilikilize ile clip kwa umakini

Msemaji anasema '' Tumepata misiba miwili...............na kijana mmoja mwili upo mortuary zinahitajika milioni 2 na laki moja pale Sekoutoure'' Maana yake zinahitaji pesa ili kutoa mwili Hospitali, si kusafirisha mwili

Makonda anatoa amri ambulance ikachukue mwili bila kuwasiliana na taasisi husika ambayo ni Sekoutoure.
Kuna uwezekano yapo malipo yanahitaji, hakuna shida kama angesema atalipia , alichofanya ni kutoa amri kwa Taasisi au Hospitali kutafuta umaarufu na si suluhu ya jambo.

Leo kuna uwezekano Hospitali imeruhusu mwili, lakini je huo ndio utaratibu?

Kwa kiongozi anayejua wajibu, kuwajibika na taratibu za kazi jambo la kwanza lilikuwa kuwasiliana na Hospitali kufahamu tatizo ni nini, halafu atoes suluhu siyo kukimbilia 'toa ambulance ' na bla bla . Huo si uongozi ni ukurupukaji
 
Hili ni suala la Wizara ya Afya siyo Makonda!

Makonda ni mwenezi tu yaani mpiga projo, hana mamlaka yoyote isipokuwa kwa wasiojua.
Hawezi kumwajibisha hata mfagizi wa Hospitali katika sakata hilo.
 
Utaambiwa uwaziri Mkuu wake unatokana na kukubalika kwa Ilani y CCM kwa wananchi kisha wananchi kuweka CCM madarakani, Na CCM kutengeneza Serikali, na serikali kuundwa huku Waziri Mkuu akiwa ndiye mtendaji Mkuu wa serikali hiyo chini ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama.

Kwa kifupi Chama kipo juu ya serikali!!
Na Makonda anakisemea Chama. Anaye"summon" si Makonda bali ni Chama.

Binafsi, sijamsikia Makonda anasema ninakuagiza, bali anasema Chama kinakuagiza...!!!

Hata hivyo, Nina uhakika 100% unayajua haya mleta mada.
 
Leo kuna uwezekano Hospitali imeruhusu mwili, lakini je huo ndio utaratibu?
Binafsi, napenda utaratibu ufuatwe, sikufurahishwa na kupanda "roli la mchanga" ambalo ni la mizigo si la kubeba watu. Vinginevyo, awe amepewa Kibali na askari wetu wa barabarani.

Hata hivyo, ieleweke Makonda anakisemea Chama, Chama ndicho kinaisimamia serikali, na Serikali ndiyo inasimamia hizo Taasisi zilizoagizwa na Chama kupitia msemaji.
 
Mkuu Nguruvi3, Konda Boy ni action oriented man, wananchi wanachotaka sio maneno, wanataka vitendo, actions, Konda Boy anafanya actions, hivyo kuwapa wananchi wanachotaka!, kiukweli CCM imekuja juu!.

Kwa CCM, hii ni sifa!, angalia nilisema nini kumhusu Makonda na sifa hii Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... nilisema Makonda ni populist leader anatumia system ya utawala ya populism kwa kuwa ni pragmatist anafanya pragmatism, na hiki ndicho wananchi wanachotaka, hivyo Makonda anawapa wananchi wanachotaka, CCM inazidi kupendwa na kupaa!.

P
 
Huyo ni mnafiki marehemu akishafariki kinachofuata ni kuzika mwili wake! Hapo mwananchi anaomba msaada ili mwili ulipiwe ukazikwe! Mwenezi kama chama akasema hilo limekwisha kwa maana anaenda kulipia na ambulance ilikuwepo hapo hapo kwenye msafara wake! Unafiki wa wabongo walitaka sijui atoe maelekezo gani ili kuonesha anafata utaratibu!
 


Roho mbaya zimetutawala.
 


Bado nimebaki kushangaa inakuwaje magwiji wa Siasa humu JF Kama mzee Nguruvi kushindwa kuelewa mtiririko mwepesi Kama huu?!


Ni kwamba kumbukumbu ya Mwenezi wa CCM 2010 mpaka 2014 imeshaondoka vichwani mara hii?



Ni lini mbwa alipanda juu ya mti bila kupandishwa?
 
Hili ni suala la Wizara ya Afya siyo Makonda!

Makonda ni mwenezi tu yaani mpiga projo, hana mamlaka yoyote isipokuwa kwa wasiojua.
Hawezi kumwajibisha hata mfagizi wa Hospitali katika sakata hilo.
Polical mileage huwa inatafutwa kwa namna yeyote ile !!
Yetu macho na masikio !
Ngoja tuone !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…